Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza
katika kikao cha baraza la ushauri la watumiaji wa nishati na maji
nchini na wadau wake walipotembelea Mkoani Rukwa kwa ajili ya shughuli
mbalimbali za baraza hilo. Mkuu huyo wa Mkoa alitoa pongezi kwa kazi
nzuri wanayofanya na kuahidi kuwachukulia hatua walanguzi wa nishati ya
mafuta pamoja na wale wanasimamia kwa kushindwa kufanya kazi yao vizuri.
Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima.
Mwenyekiti wa baraza la ushauri watumiaji wa
maji na nishati nchini Eng. Profesa Katima akizungumza katika kikao
hicho ambapo alisema kazi kubwa ya baraza hilo ni kutetea na kulinda
haki za watumiaji wa maji na nishati ambayo ni maji safi na maji taka,
umeme, petroli na gesi asilia.
Baadhi ya wadau wa mkutano huo ambao ni
vyombo vya ulinzi na usalama, Tanesco, EWURA Mkoa wa Rukwa, wawakilishi
wa sheli za mafuta na shirika la Maji safi na Maji taka Mkoa wa Rukwa
(SUWASA)
Wawakilishi wa baraza hilo Mkoani Rukwa
Picha ya pamoja.
(Na Hamza Temba -Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Rukwa)
No comments:
Post a Comment