Jaji Mkuu wa Uganda Mhe. Benjamin Odoki (kushoto) akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (alhamisi Feb. 14 2013) kuhusu uzoefu wake katika uandishi na utekelezaji wa Katiba. Jaji Odoki aliongoza Tume ya Katiba ya Uganda iliyoundwa mwaka 1989. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba.
Jaji Mkuu wa Uganda Mhe.
Benjamin Odoki (kulia) akiongea na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba
katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Jaji Odoki, ambaye aliongoza
Tume ya
Katiba ya Uganda iliyoundwa mwaka 1989, amekutana na Wajumbe wa Tume leo
(alhamisi Feb. 14, 2013) na kuzungumzia uzoefu wake kuhusu uandishi na
utekelezaji wa Katiba Mpya.
Katibu wa Tume ya Mabadiliko
ya Katiba, Bw. Assaa Rashid (kushoto) akimkaribisha Jaji Mkuu wa Uganda,
Mhe.
Benjamin Odoki (katikati) mara baada ya kuwasili katika ofisi za makao
makuu ya
Tume hiyo Jijini Dar es Salaam leo (alhamisi Feb 14, 2013) na kulia ni
Mjumbe wa
Sekretarieti ya Tume, Bw. Joseph Ndunguru. Jaji Odoki, ambaye aliongoza
Tume ya
Katiba ya Uganda iliyoundwa mwaka 1989, amekutana na Wajumbe wa Tume na
kuzungumzia uzoefu wake kuhusu uandishi na utekelezaji wa Katiba
Mpya
No comments:
Post a Comment