Friday, June 26, 2015

KAFULILA AKOMALIA MABEHEWA FEKI

Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila.

MBUNGE wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR Mageuzi) ameitaka Serikali kuwasilisha bungeni taarifa ya kashfa ya ununuzi wa mabehewa feki katika Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na kusababisha hasara ya Sh bilioni 230. 

Baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni jana, mbunge huyo alisimama kuomba muongoza wa Spika kwamba kutokana na unyeti wa jambo hilo, ikiwa ni pamoja na madai kwamba Kampuni iliyopewa zabuni ya kuagiza mabehewa hayo haikuwa na uwezo huo, kwa nini suala hilo lisipelekwe bungeni kujadiliwa.

WATOTO WALIWA NA FISI

Watoto wawili wenye umri wa kati ya miaka miwili na mitano wameuawa na fisi katika Kijiji cha Mnkola, Kata ya Ibihwa wilayani Bahi Mkoa wa Dodoma katika matukio mawili tofauti.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Teya Kata ya Ilindi wilayani hapa, Paul Mwaja alisema kuwa watoto hao wameuawa katika matukio mawili ndani ya kipindi cha wiki moja.

Mwaja alisema tukio la kwanza lilitokea juzi ambapo mtoto mmoja wa kiume mwenye aliuawa na fisi wakati akiwa na wenzie wawili wamelala.

AL-SHABAAB YASHAMBULIA KITUO CHA AMISOM

Kituo cha kijeshi cha wanajeshi wa kimatifa wa kulinda amani nchini Somalia Amisom. 

Takriban watu 30 wamepoteza maisha yao baada ya shambulizi la kigaidi katika kituo cha kijeshi cha wanajeshi wa kimatifa wa kulinda amani nchini Somalia Amisom.

Walioshuhudia wanasema kuwa mlipuaji wa kujitolea mhanga aliendesha gari lake moja kwa moja hadi kwenye lango kuu la kituo hicho .

Kituo hicho kiko katika eneo la Leego, barabara kuu inayounganisha mji mku wa Mogadishu na Baidoa.

BURUNDI KUENDELEA NA RATIBA YA UCHAGUZI

Gervais Rufyikiri aliyekuwa makamu wa rais wa Burundi amekimbilia Ubelgiji. 

Serikali ya Burundi imesema haitashiriki katika mazungumzo yaliyodhaminiwa na Umoja wa Mataifa yakilenga kupunguza hali ya uhasama uliopo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wenye utata.

MKWASA AWAOMBA MASHABIKI WA SIMBA WASIMZOMEE

Kocha wa timu ya soka ya Taifa ya Taifa Stars, Charles Mkwasa.

KOCHA mpya wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amewataka mashabiki wa Simba kutomzomea pindi watakapomuona kwenye mazoezi au mechi, kwa vile atakuwa pale kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya wachezaji wake wa timu ya taifa. 

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Mkwasa alisema mashabiki wanatakiwa kufahamu kuwa yeye ni kocha wa taifa, hivyo atakuwa akitembelea katika mechi za timu mbalimbali kuangalia wachezaji na maendeleo ya wale wanaocheza timu ya taifa.

“Mashabiki wa Simba mnaponiona kwenye mechi zenu msinikimbize kwa mawe mkadhani kuwa nimekuja kwa ajili ya Yanga, nitakuwa na utaratibu wa kutembelea timu kuangalia wachezaji, mnajua kazi ya kocha wa taifa ndio hiyo,” alisema Mkwasa ambaye pia ni Kocha Msaidizi wa Yanga.

TAMBWE AIPANIA KAGAME

Amissi Tambwe

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amissi Tambwe amesema anategemea kufanya vizuri zaidi katika michuano ijayo ya Kagame kuisaidia timu kuchukua taji katika michuano hiyo itakayofanyika nchini kuanzia mwezi ujao. 

Tambwe, ambaye aliwahi kufanya vizuri katika michuano hiyo iliyofanyika Sudan miaka miwili iliyopita kwa kuibuka mfungaji bora, aliliambia gazeti hili kuwa anajipanga kufanya vizuri zaidi.

Mchezaji huyo aliibuliwa na Simba katika michuano hiyo wakati akiichezea Vital’O ya Burundi iliyochukua ubingwa wakati huo, kutokana na kuisaidia timu yake kwa kiasi kikubwa na kufanya vizuri.

ENGLAND YATETEA WACHEZAJI CHIPUKIZI

Timu ya England U21 katika moja ya michezo yao ya michuano ya Ulaya

England imefanya uamuzi sahihi kuwaondoa katika michuano ya ubingwa wa Ulaya kwa wachezaji wa umri chini ya miaka 21, baadhi ya wachezaji wake ambao wanacheza ligi kuu ya nchi hiyo, amesema mkurugenzi wa chama cha soka wa maendeleo ya wachezaji Dan Ashworth.

Timu ya England chini ya kocha Gareth Southgate ilifuzu kucheza hatua ya makundi kwa kwenda Jamhuri ya Czech. "Tulifanya uamuzi na nautetea ," Ashworth amemwambia mwandishi mwandamizi wa BBC wa habari za mpira wa miguu Ian Dennis. 

"Timu za vijana zipo kusaidia kuwakuza wachezaji na kuwapa uzoefu kuingia katika timu ya wakubwa." Mchezaji wa ushambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling, kiungo wa Everton Ross Barkley, viungo wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain na Jack Wilshere na mlinzi wa Manchester United Phil Jones ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wakihitajika katika timu hiyo, lakini hawakuitwa.

England, ambayo ilikuwa na wachezaji wa ligi kuu, akiwemo mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, mlinzi wa Everton John Stones na mshambuliaji mpya wa Liverpool Danny Ings, ilipoteza kwa Ureno 1-0 , wakaifunga Sweden kwa idadi kama hiyo lakini ilipoteza 3-1 kwa Italia.

Wednesday, June 24, 2015

WAZIRI GHASIA, KAFULILA WATOFAUTIANA BUNGENI

Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila 

Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia jana walitofautiana bungeni kuhusu tuhuma za ubadhirifu wa fedha zinazomkabili Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Hadija Nyembo.

Tukio hilo lilitokea baada ya swali la nyongeza la mbunge huyo, aliyetaka kujua msimamo wa serikali kuhusu Nyembo aliyedai kutoa kauli ya kutaka Wabembe waende kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) iliyosababaisha Wabembe kukamatwa na kupelekwa ubalozini, ambapo ubalozi wa DRC , uliwakataa na kusababisha wanyanyasike kwa karibu wiki mbili. 

Pia Mbunge huyo alidai Mkuu huyo wa Wilaya aliondolewa wilayani Chato akihusishwa na ufisadi wa mbolea yenye thamani ya Sh bilioni 1.5 na kwamba sasa ana kesi katika Mahakama ya Wilaya ya Chato, hivyo serikali haioni aibu kuwa na Mkuu wa Wilaya wa aina hiyo, ambaye anashitakiwa na serikali yenyewe.

IS YAPATA WAFUASI WAPYA WA KANDA YAO

Mpiganaji wa IS

Kundi la kigaidi la wanamgambo wa kiislam, maarufu kama Islamic State limekubali ombi na ahadi ya wanamgambo wa kutoka kusini mashariki mwa Asia na Ulaya kusini magharibi katika maeneo ya Chechnya and Dagestan.

Hii ni mara ya kwanza kwa kundi hilo la IS kukaribisha rasmi kundi la wanajihadi kutoka katika kanda yao kuingia katika shirika lake. 

Na hii inaelezwa kwamba imekuja baada ya Vyombo vya habari vinavyotangaza kwa lugha ya lugha ya Kirusi mwishoni mwa wiki iliyopita, kurushwa kwa kipande cha video kinachomuonesha kiongozi mkuu wa kijeshi kutoka Chechnya akiapa na kuahidi kujitoa sadaka na kuwa kuwa mtii kwa IS.

Taarifa za awali zinaeleza kwamba kundi kubwa la kigaidi lenye kujitoa muhanga la Chechnya lilikuwa likipinga harakati za Is.

MTUNZI WA FILAMU YA TITANIC AFARIKI DUNIA

James Horner, enzi za uhai wake.

James Horner mtunzi nguli wa eneo maarufu kwa watu maarufu la Hollywood ambaye aliandika na kushinda katika tuzo za Oscar juu ya filamu maarufu ulimwenguni ya Titanic, amefariki dunia mjini California kutokana na ajali ya ndege akiwa na umri wa miaka 61. 

James alipata mafunzo ya urushaji wa ndege, inaarifiwa alikuwa peke yake wakati alipopata ajali hiyo, na ndege binafsi ndogo ambayo alipata nayo ajali eneo la Kusini mwa Santa Barbara mwanzoni mwa wiki hii.

Mwandishi huyu na mtunzi wa tungo mbali mbali ametia mkono wake katika kazi tatu tofauti za filamu za msanii James Cameron, pamoja na filamu ya A Beautiful Mind, Braveheart, Troy na ile ya Apollo 13.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...