Jeshi la Polisi Tanzania, limekumbwa
na janga la tatu katika kipindi kisichozidi miezi saba baada ya watu
wanaosadikiwa kuwa majambazi kuvamia na kuua askari wake wawili katika
Kituo cha Ikwiriri wilayani Rufiji juzi na kisha kupora bunduki saba na
risasi 60.
Tukio hilo limefanya jumla ya askari waliouawa
kufikia watano huku bunduki 22 na risasi zaidi ya 120 zikiwa zimeporwa
baada ya kuvamiwa kwa vituo vitatu vya polisi tangu Juni 11 mwaka jana.
Mbali na Ikwiriri, vituo vingine vilivyovamiwa ni Mkamba Kimanzichana, Mkoa wa Pwani na Bukombe mkoani Geita.
Matukio hayo yametokea ikiwa ni mwaka mmoja na
wiki tatu tangu Ernest Mangu alipoanza kazi ya Inspekta Jenerali wa
Polisi (IGP) akimrithi mtangulizi wake, Said Mwema. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.