Klabu ya Yanga imepanga leo kuwasilisha malalamiko yao juu ya tukio
la kunyanyaswa kwa mshambuliaji wake Amissi Tambwe kwa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) lakini pia mchezaji husika amefafanua kwa kina juu
ya manyanyaso anayoyapata.
Akizungumza mchana wa leo katika makao makuu wa klabu hiyo Mkuu wa
Kitengo cha Habari Jerry Muro amesema uongozi wao unakusudia kuwasilisha
malalamiko yao hayo ambayo mengi yametokana na vitendo alivyofanyiwa
Tambwe wikiendi iliyopita katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambapo
wanataka mapendekezo yao manne yafanyiwe kazi.
Muro amesema kwanza Yanga ingwetaka kuona TFF inawachukulia hatua
kali wahusika wote waliomdhalilisha Tambwe huku pili wakilitaka
shirikisho hilo kutoa hadharani taarifa ya tathimini ya waamuzi wa
mchezo huo lengo likiwa ni kujua umakini wa waamuzi hao. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
“Tatu tungewaomba wenzetu wa TFF kwa kuwa wao wapo kimya pia
kuwachukulia hatua wahusika wote waliosimamia mchezo huo kwa kushindwa
kubaini haya ambayo vyombo vya habari imeyafichua lakini ikiwezekana
wafungiwe na Yanga hatuwataki kuwaona wanachezesha mechi zetu vinginevyo
tutagoma na hata Ruvu nao tungependa kuona wanapewa adhabu kwa viongozi
wao kushabikia maovu haya.
Aidha Tambwe mwenyewe amechukizwa na matukio hayo akisema
ameshangazwa kuona anafanyiwa vitendo vya kinyama ambapo mengine hawezi
kuyaweka hadharani.
“Mpira ni starehe mimi sikatai mchezaji anikabe lakini ni jinsi gani
unanikaba hapo ndiyo tatizo, naambiwa mimi mkimbizi hivi hawa wenzangu
wanajua maana na haya maneno yapo mengi ambayo nimedhalilishwa nayo
kiungwana siwezi kuyaweka wazi hapa lakini viongozi nitawaeleza,”alisema
Tambwe. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.