Wednesday, January 21, 2015

TAMBWE ASIMULIA ANAVYOTESWA, YANGA YASHITAKI

muro 2
Klabu ya Yanga imepanga leo kuwasilisha malalamiko yao juu ya tukio la kunyanyaswa kwa mshambuliaji wake Amissi Tambwe kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lakini pia mchezaji husika amefafanua kwa kina juu ya manyanyaso anayoyapata.
 
Akizungumza mchana wa leo katika makao makuu wa klabu hiyo Mkuu wa Kitengo cha Habari Jerry Muro amesema uongozi wao unakusudia kuwasilisha malalamiko yao hayo ambayo mengi yametokana na vitendo alivyofanyiwa Tambwe wikiendi iliyopita katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambapo wanataka mapendekezo yao manne yafanyiwe kazi.
Muro amesema kwanza Yanga ingwetaka kuona TFF inawachukulia hatua kali wahusika wote waliomdhalilisha Tambwe huku pili wakilitaka shirikisho hilo kutoa hadharani taarifa ya tathimini ya waamuzi wa mchezo huo lengo likiwa ni kujua umakini wa waamuzi hao. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
muro
“Tatu tungewaomba wenzetu wa TFF kwa kuwa wao wapo kimya pia kuwachukulia hatua wahusika wote waliosimamia mchezo huo kwa kushindwa kubaini haya ambayo vyombo vya habari imeyafichua lakini ikiwezekana wafungiwe na Yanga hatuwataki kuwaona wanachezesha mechi zetu vinginevyo tutagoma na hata Ruvu nao tungependa kuona wanapewa adhabu kwa viongozi wao kushabikia maovu haya.
Aidha Tambwe mwenyewe amechukizwa na matukio hayo akisema ameshangazwa kuona anafanyiwa vitendo vya kinyama ambapo mengine hawezi kuyaweka hadharani.
“Mpira ni starehe mimi sikatai mchezaji anikabe lakini ni jinsi gani unanikaba hapo ndiyo tatizo, naambiwa mimi mkimbizi hivi hawa wenzangu wanajua maana na haya maneno yapo mengi ambayo nimedhalilishwa nayo kiungwana siwezi kuyaweka wazi hapa lakini viongozi nitawaeleza,”alisema Tambwe. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

KLABU KUJIGHARAMIA HOTELI MICHUANO YA CAF

NGASA 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limefanyia marekebisho kanuni zake za michuano ya ngazi ya klabu kwa upande wa malazi ambapo sasa timu zitachagua na kujilipia zenyewe hoteli zinapokuwa kwenye mechi za ugenini. Kabla ya marekebisho ya kanuni hiyo, timu ngeni ilikuwa ikilipiwa hoteli na timu mwenyeji kwa msafara usiozidi watu 25. CAF ilikuwa imepitisha hoteli maalumu katika kila nchi ambapo mwenyeji alitakiwa kuziweka timu ngeni.
Kwa marekebisho hayo, Chama cha Mpira wa Miguu cha nchi mwenyeji kitakuwa na wajibu wa kuitafutia hoteli timu ngeni iwapo tu kitaombwa kufanya hivyo, lakini jukumu la kulipia malazi litakuwa la timu yenyewe.
Mwaka huu Tanzania inawakilishwa na timu mbili za Azam na Yanga katika michuano ya CAF. Azam inacheza Ligi ya Mabingwa (CL) ambapo itaanzia nyumbani Februari 15 mwaka huu kwa kuikaribisha El Merreikh ya Sudan kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Nayo Yanga itacheza michuano ya Kombe la Shirikisho (CC), na imepangiwa kucheza mechi ya kwanza nyumbani dhidi ya BDF IX ya Botswana. Mechi hiyo itafanyika Februari 14 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

GERVINHO AOMBA MSAMAHA KWA KADI NYEKUNDU

Gervinho
 
Mchezaji wa Ivory Coast Gervinho ameomba msamaha baada ya kupewa kadi nyekundu kwa kumpiga mlinzi wa timu ya Guinea Naby Keita katika mechi ya timu hizo mbili ilioisha 1-1.
''Nataka kuomba msamaha kwa taifa la Ivory Coast,wachezaji wenzangu na waandalizi wa michuano ya mataifa ya Afrika kwa kitendo hiki cha hasira'',aliandika katika mtandao wake wa Twitter.
''Haikuwa mimi na vitendo kama hivyo havina nafasi katika viwanja vya soka'',,aliongezea.
Kulingana na sheria za FIFA, mchezaji hukosa mechi moja anapopewa kadi nyekundu ,lakini shirikisho la Soka barani Afrika huenda likaongeza adhabu hiyo.
Kawaida mtu hupewa marufuku ya mechi mbili katika michuano ya Afrika,lakini adhabu hiyo inaweza kuongezwa na kufikia mechi nne iwapo kamati ya nidhamu itahisi mchezaji huyo anahitaji kupewa adhabu kali. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

BUKINA FASO YAAPA KUWASHINDA WENYEJI

Afcon 
 
Nahodha wa timu ya taifa ya Burkina Fasso Charles Kabore amesisitiza kuwa wataimarisha mchezo wao baada ya kushindwa na Gabon katika mechi yao ya kwanza.
''Mashindano haya hayajakamilika kwetu sisi.''Iwapo tutashinda dhidi ya wenyeji wa maandalizi haya basi kila kitu kitakuwa shwari''.
Mkufunzi wa timu ya Equitorial Guinea Esteban Becker anajua kwamba timu yake ni sharti ishinde mchuano huo dhidi ya Burkina Fasso ilio na washambuliaji mahiri.
Hatahivyo Equitorial Guinea ni sharti iimarishe safu yake ya Ulinzi,baada ya kushindwa kuweka rekodi ya kutofungwa katika mechi zake nne katika michuano hiyo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

ARSENAL YAMSAJILI KRYSTIAN BIELIK

Krystian Bielik aliyesajiliwa na Arsenal
Arsenal imekamilisha usajili wa kiungo wa kati Krystian Bielik mwenye umri wa miaka 17 kutoka kilabu ya Legia warsaw kwa kitita kisichojulikana.
Bielik aliichezea timu kubwa ya kilabu hiyo ya Poland mnamo mwezi Agosti akiwa na umri wa miaka 16.
Pia alishiriki katika mechi tano ya kilabu hiyo na mara moja katika ligi ya yuropa.Mchezaji huyo anayesifiwa na wengi anaweza kucheza katika safu ya kati na ile ya Ulinzi. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Sunday, January 18, 2015

MATOKEO YA MECHI ZA EPL LEO JUMAPILI HAYA HAPA


article-2915617-24D1DC2000000578-487_964x390 
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
 
EnglandPremier LeagueJanuary 18
FT West Ham United 3 – 0 Hull City
FT Manchester City 0 – 2 Arsenal

UPINZANI DRC: KATIBA IMEPINDULIWA

 
Wabunge wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo wamekubali mswada ambao wadadisi wanasema unakusudiwa kumpa Rais Joseph Kabila idhini ya kubaki madarakani, baada muhula wake wa pili kumalizika.
Mswada huo unapendekeza kufanywe sensa ya taifa kabla ya uchaguzi ambayo serikali inasema inaweza kuchukua miaka kadha kukamilisha.
Rais Kabila anamaliza muhula wa pili mwaka ujao.
Katiba ya nchi haimruhusu kugombea muhula wa tatu.
Mwandishi wa BBC mjini Kinshasa anasema wabunge wengi wa upinzani walisusia kura hiyo ya bunge, na kuielezea kuwa mapinduzi ya katiba. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

BOKO HARAM WAFANYA UVAMIZI CAMEROON

Askari jeshi wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wa kundi haramu Boko Haram wameteka watu zaidi ya 60 katika nchi jirani ya Cameroon imethibitika.
Inasemekana miongoni mwa mateka wengi wao ni watoto waliokamtwa mpakani mwa nchi mbili hizo.Na inaarifiwa kuwa watu kadhaa waliuawa wakati wa utekelezaji wa tukio hilo.
Boko Haram siku za hivi karibuni zimekamata udhibiti wa miji kadhaa na vijiji upande wa kaskazini Mashariki mwa Nigeria, na sasa wameanza kuwa tishio kwa nchi jirani wanazopakana na Nigeria .Katika shambulio hilo la siku ya Jumapili askari hao walivamia vijiji viwili vilivyoko eneo la Tourou .
Katika uvamizi huo nyumba kadhaa zilichomwa moto na idadi ya mateka ni themanini kati yao watu wazima ni thelathini,na watoto wapatao hamsini na walielekea upande wa Kaskazini mwa Cameroon .
Kundi hilo limepigana vita takribani miaka sita sasa, wakijaribu kuusimika utawala wa dola ya kiislam nchini humo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

ARSENAL YAWASHANGAZA MABINGWA WA EPL

 Santi Carzola alifunga bao moja na kutengeza jengine na kuisadia Arsenal kuicharaza Mancity mabao 2-0 nyumbani Manchester.
Ushindi huo wa Arsenal pia ulisitisha msururu wa kutofungwa wa Mancity wa mechi 12.
Mchezaji wa Uhispania Santi Carzola aliyekuwa moto wa kuotea mbali dhidi ya Mancity alifunga mkwaju wa penalty baada ya beki wa Arsenal Nacho Monreal kuangushwa katika eneo la hatari na beki Vincent Kompany.
 
Arsenal iliongeza bao la pili katika kipindi cha pili baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na Santi Carzola kuwekwa wavuni na Olivier Giroud.
Matokeo hayo yameiwacha City ikiwa na alama 5 chini ya viongozi wa ligi Chelsea.
City na Arsenal walitoka sare ya 2-2 wakati walipokutana kwa mara ya kwanza katika uga wa Emirates mnamo mwezi Septemba. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

VIWANJANI MWISHONI MWA WIKI

Ligi kuu ya England imeendelea kwa mechi mbili ambapo..Arsenal imeibamiza Man City ,Huku Westham Ikiibamiza Hull City bao 3-0
Nayo Michuano ya Kombe la Mataifa barani Afrika ikiwa imeng'oa nanga hapo jana kwa Gabon Kuilaza Burkina faso bao 2-0 Huku Pierre Emerick Aubemeyang aking'ara vilivyo.Nao wenyeji Equitorial Guinea wakishikwa shati na Congo Brazaville kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1.
Ligi kuu ya England ambapo Jumapili zimechezwa mechi mbili ,Katika mechi ya awali Westham United iliibamiza Hull City bao 3-0 mabao yaliyotiwa kambani na Andy Carrol katika dakika ya 49,Amalfitano katika dakika ya 69 na Stewart Downing aliyehitiisha ushindi huo mnono wa Westham katika ya 72 akimalizia pasi murua ya kiungo Mcameroun aliyeko kwenye Fomu Alexandre Song.
Kwa matokeo hayo Westham imefikisha Point 36 wakiwa nafasi ya 7,wakiwa pointi moja mbele ya Liverpool wenye pointi 35 walioko nafasi ya 8,huku timu hizo zikitaraji kukutana katika mechi ijayo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...