Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo
POLISI mkoani Morogoro linamshikilia Jackson Mnyilemi (20), ambaye ni
muumini wa Kanisa la Moravian Tarafa ya Malinyi wilaya ya Ulanga mkoani
Morogoro kwa tuhuma za kuhusika kufanya fujo kanisani.
Fujo hizo zilisababisha kujeruhiwa kwa waumini wawili kwa kukatwa sehemu za usoni na mikononi na kitu chenye ncha kali.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo alisema jana
kuwa tukio hilo ni la Desemba 28, 2014 majira ya saa 10 : 40 asubuhi
katika kijiji cha Makelele na kuwataja waumini waliojeruhiwa kuwa ni
Maria Silumbwe (47) na Aron Silumbwe (20), wote wakazi wa Kijiji hicho
kilichopo Tarafa ya Malinyi wilayani Ulanga. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.