Katibu wa Hamasa
wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Paul Makonda amesema
alitamani kuzungumza siku ya mdahalo ulioandaliwa na Kigoda cha Mwalimu
Nyerere Foundation lakini vurugu zikazima ndoto yake.
Makonda ambaye anatuhumiwa kuwa ndiye aliyepanga
vurugu hizo zilizosababisha aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko
ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba kushambuliwa, alikana na kudai
kuwa hata yeye alitamani kukisikia kile kilichopangwa kuzungumzwa na
wasemaji wakuu wa mdahalo huo ili ajibu hoja zao katika mkutano huo.
Akizungumza jana katika ofisi za gazeti hili,
Makonda alisema aliingia ukumbini akiwa na nakala ya Katiba
Inayopendekezwa kwa madai kuwa ingeweza kumsaidia kuainisha yale ambayo
yangejadiliwa na ikibidi achangie hoja kwa kutetea au kutoa ufafanuzi wa
kile kilichoandikwa ndani ya Katiba hiyo.
“Nasikitika kwa sababu malengo yangu hayakutimia
kutokana na vurugu zile. Lengo langu lilikuwa; nipate nafasi ya
kuzungumza ili nitoe hoja zangu na kufafanua uzuri wa Katiba
Inayopendekezwa,” alisema.
Hata hivyo, alisema yaliyosemwa na Jaji Warioba
kabla ya mdahalo kuvunjika, yalimpa fursa ya kujua ni vifungu vipi vina
kasoro na vipi viko sahihi. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz