Wagombea
wawili kati ya wanne waliojitokeza kuwania nafasi ya urais wa
shirikisho la vyama vya soka Duniani FIFA wamejitoka katika
kinyang'ang'anyiro hicho.
Nyota wa zamani wa soka huko Ureno ,
Luis Figo ambaye ni mmoja wa waliojitoa kuwania nafasi hiyo,amelalamikia
mfumo wa uendeshaji wa uchaguzi huo na kuiita kuwa ni wakinafiki.
Amesisitiza
kuwa kwa mtazamo wake anaona kuwa taratibu zilizowekwa zililenga
kumnufaisha mgombea mmoja tu na si kuelta usawa wa wote waliojitokeza
kuwania nafasi hiyo,ambapo inaonekana kuwa ni mpango uliowekwa kumpatia
nafasi ya ushindi Rais wa sasa Sepp Blatter ambaye anawania nafasi hiyo
kwa kipindi cha tano.
Hata hivyo Rais wa chama cha soka huko
Uholanzi , Michael van Praag , akijitoa. Huku wapinzani waliosalia ni Bw
Blatter ambaye ni Jordan Prince Ali Al Hussein ambaye ni mwanachama wa
kamati ya utendaji ya FIFA.
Mgombea mwingine aliyejitoa pia ni
Rais wa chama cha soka cha Uholanzi Michael van Praag na hivyo kuwaacha
Blatter na mtu anayedaiwa kuwa mpinzani wake wa karibu Prince Ali Al
Hussein ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya FIFA. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.