Sunday, May 17, 2015

RAIA WAPYA WAKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI...!!!

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi.

POLISI mkoani Katavi imewakamata raia wapya watatu waliokuwa wakimbizi kutoka Burundi kwa kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo.

Watu hao walikamatwa na nyara za Serikali zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 1.2. Nyara hizo za Serikali ni vipande vitatu vya meno ya tembo vikiwa sawa na jino moja la mnyama huyo vikiwa tayari kusafirishwa kwenda mjini Tabora.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi , Dhahiri Kidavashari amewataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Frank Hamis (18) , Steven Jonas (22) na Jackson Erasto ambao karibuni wamepewa uraia wa Tanzania. 

Kidavashari alibainisha kuwa watuhumiwa hao walikutwa juzi saa 3:00 asubuhi katika chumba alichopanga mwanafunzi wa kidato cha Nne katika shule ya sekondari Katumba, Ernest John (19) katika eneo la Mnyasi kijijini Katumba wilayani Mlele. 

“Mwanafunzi huyo ana uhusiano nao wa kindugu hivyo aliwakaribisha kulala chumbani kwake alimokuwa amepanga katika nyumba ambayo ni mali ya Felix Gado iliyopo eneo la Mnyasi kijijini Katumba.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...