Kiongozi wa Chama cha ACT - Wazalendo, Zitto Kabwe akizungumza na wahariri wa gazeti la Mwananchi alipotembelea makao makuu ya Mwananchi Communications Limited, yaliyopo Tabata Relini, Dar es Salaam jana.
Kiongozi wa Chama cha ACT -
Wazalendo, Zitto Kabwe amesema zaidi ya wabunge 50 wa vyama mbalimbali
vya siasa nchini watajiunga na chama hicho kipya na kugombea ubunge
katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Zitto ambaye alijivua ubunge wa Kigoma Kaskazini
baada ya kufukuzwa uanachama wa Chadema, amebainisha kuwa wabunge hao,
wakiwamo wa CCM na Chadema, ni miongoni mwa watu wanaokichangia fedha
chama hicho kilichopata usajili wa kudumu Mei, mwaka jana na kuzinduliwa
mwezi uliopita.
Pia, amewatangazia vita wabunge wa majimbo manane
ya Mkoa wa Kigoma, akijigamba kuwa ili waweze kuibuka na ushindi katika
uchaguzi huo ni lazima wakubali kujiunga na ACT kwa kuwa chama hicho
kimejipanga kuyabeba majimbo yote. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.