Baada ya kukaa mahabusu kwa siku saba na
kusherehekea sikuu ya Pasaka wakiwa gerezani, Mwenyekiti wa Chadema
Taifa Mhe. Freeman Mbowe pamoja na vigogo wengine sita wa chama hicho
leo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia kwa dhamana, baada ya
kukamilisha masharti.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka tisa yakiwemo ya
Uchochezi wa Uasi na kufanya mkusanyiko isivyo halali kinyume cha
sheria.
Mbali ya Mbowe washtakiwa wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini
Mhe. Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu
katibu Mkuu Bara na Mbunge wa kibamba Mhe. John Mnyika.
Wengine ni Mbunge wa Tarime Mjini Mhe. Esther Matiko na
Katibu wa chama hicho Dk. Vicenti Mashinji na Mbunge wa Kawe Halima
Mdee ambaye ameunganishwa na wenzake hao jana.
Mdee alikamatwa
Jumapili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea nchini
Afrika Kusini. Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana
kwa website ya jambotz.co.tz
No comments:
Post a Comment