Wednesday, April 04, 2018

AGNES MASOGANGE AKWEPA KWENDA JELA BAADA YA KULIPA FAINI

Msanii wa kupamba video za muziki (Video Queen), Agnes Gerald ‘Masogange’ amekwepa kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kulipa faini ya Sh. milioni 1.5.

Msanii maarufu nchini, Agnes Gerald maarufu Masogange alikutwa na hatia ya kutumia dawa za kulevya na kuhukumiwa kwenda jela au kulipa faini.

 Hakimu wa Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, Wilbard Mashauri, ametoa hukumu hiyo leo Aprili 3 na kuieleza mahakama kuwa Masogange katika kosa la kwanza amekutwa na hatia ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin na kosa la pili kutumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.

“Hivyo katika kosa la kwanza, mahakama inamhukumu kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya Sh1 milioni na kwa kosa la pili, amehukumiwa kwenda jela miezi 12 au kulipa faini ya Sh 500, 000,” amesema Hakimu Mashauri.

Februari 17 mwaka jana, aliyekuwa Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwaeleza wanahabari kuwa Masogange amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kupimwa iwapo anatumia dawa hizo za kulevya.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...