Winnie Madikizela-Mandela enzi za uhai wake.
Mwanasiasa na
mwanaharakati aliyepigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika
Kusini Winnie Madikizela-Mandela alifariki dunia Jumatatu akiwa na miaka
81.
Alikuwa mke wa zamani wa rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini
Nelson Mandela lakini alikuwa na msimamo mkali zaidi kumshinda hata Bw
Mandela mwenyewe. Winnie alifahamika sana na wengi kama Mama wa Taifa.
Winnie alikuwa
nembo kuu ya vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi, na ingawa sifa
zake ziliingia doa miaka ya baadaye, lakini bado alitambuliwa kama
mtetezi wa wanyonge.
Alisalia kuwa mwanachama wa chama tawala cha
African National Congress (ANC) ingawa nyakati za karibuni alikuwa
akikosoa uongozi wa chama hicho. Hizi hapa ni baadhi ya nukuu sita maarufu alizowahi kuzitoa.
"Miaka niliyofungwa gerezani ilinifanya kuwa mkakamavu...
Huwa sina tena hisia za woga ... Hakuna chochote ambacho naweza
kukiogopa. Hakuna kitu ambacho sijatendewa na serikali. Hakuna uchungu
ambao zijakumbana nao"
"Kwa viberiti vyetu na mikufu yetu tutaikomboa nchi hii"
"Nilikuwa na wakati mdogo sana kumpenda. Na upendo huo
umedumu miaka hii yote ambayo tulitenganishwa... pengine kama ningepewa
muda wa kutosha wa kumfahamu vyema zaidi pengine ningegundua kasoro
nyingi, lakini nilikuwa tu na wakati wa kumpenda na kumkosa sana wakati
wote"
"Mimi ni mazao ya wananchi wa taifa hili. Mimi ni mazao ya adui wangu mkuu."
"Wengi wa wanawake huupokea mfumo dume bila kuuliza maswali
na hata huutetea, kwa kuelekeza mahangaiko yao sio kwa wanaume bali
dhidi yao wenyewe wakishindania wanaume walio wana wao wa kiume, wapenzi
wao na waume zao. Kitamaduni, mke ambaye amedhalilishwa hujituliza na
kuelekeza ghadhabu zake kwa wakwe. Kwa hivyo, wanaume huishia kuwatawala
wanawake kupitia juhudi za wanawake wenyewe"
"Ninaamini kuna kitu ambacho ni kibaya sana katika historia ya taifa letu, na jinsi ambavyo tumeiharibu African National Congress"
No comments:
Post a Comment