Thursday, December 04, 2014

AFCON 2015 MAKUNDI YA TIMU 16 YATAJWA

Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, AFCON 
 
Upangaji wa makundi ya timu kumi na sita zilizofuzu kucheza fainali za mashindano ya 30 ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2015 yamefanyika katika mji mkuu wa Equatorial Guinea, Malabo.
Mashindano hayo yataanza Januari 17, 2015.
Upangaji wa makundi ulirudishwa wiki moja nyuma ili kuiwezesha Equatorial Guinea, kujiandaa baada ya kuchukua nafasi ya Morocco, iliyokuwa iandae mashindano hayo, lakini ilishindwa kufanya hivyo baada ya kutaka mashindano hayo yasogezwe mbele kuhofia ugonjwa wa Ebola ambao umeyakumba baadhi ya mataifa ya Afrika Magharibi, ambako zinatoka timu nyingi zinazoshiriki michuano hiyo.
Mabingwa watetezi Nigeria ni moja ya timu kubwa zilizoshindwa kufuzu kucheza fainali za mwakani, pamoja na Misri na Angola ambazo zote kwa mshangao hazitaweza kushiriki.
Haya hapa makundi manne ya AFCON 2015:

Kundi A Equatorial Guinea, Burkina Faso, Gabon, Congo
Kundi B Zambia, Tunisia, Cape Verde, DR Congo
Kundi C Ghana, Algeria, South Africa, Senegal
Kundi D Ivory Coast, Mali, Cameroon, Guinea

Wenyeji Equatorial Guinea na Congo zitacheza mechi ya ufunguzi wa michuano hiyo. Kundi D ndilo linaloonekana kuwa gumu zaidi kutokana na timu zilizopangwa kundi hilo. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...