Thursday, December 04, 2014

2014 NI MWAKA WA JOTO KALI DUNIANI

Viwanda vikitoa moshi angani na kuchafua mazingira
Mwaka huu unaoishia unasemekana kuwa na kiwango cha juu zaidi cha joto duniani na kwa Uingereza tangu kumbukumbu zianze kutunzwa.
Makadirio ya awali yanaonyesha kuwa katika miezi kumi ya kwanza ya mwaka 2014, wastani wa kiwango cha hali ya joto duniani kilikuwa 0.57C juu ya wastani uliokuwepo muda mrefu.
Dhoruba nchini Uingereza iliyosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi
Na miezi kumi na mmoja ya kwanza nchini Uingereza imezalisha wastani wa joto la 1.6C likiwa juu ya wastani uliokuwepo kwa muda mrefu.Utafiti mwingine uliofanywa na Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza umeonyesha kuwa ongezeko la viwango vya joto vilivyoshuhudiwa, visingetokea bila ya ongezeko la gesi zinazoharibu mazingira kutokana na shughuli za binadamu. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Mabadiliko ya tabia nchi yanayochochewa na shughuli za kibinadamu
Shirika la Hali ya Hewa la Umoja wa Mataifa, WMO, limeonya kuwa dunia inakabiliwa na mwaka wenye kiwango cha juu kabisa cha joto tangu rekodi zianze kuchukuliwa ambapo shirika hilo limesema, inathibitisha mwenendo wa ongezeko la joto likiendana na mabadiliko ya tabia nchi.Shirika hilo limesema kupanda kwa viwango vya joto katika uso wa bahari vilikuwa vinasababisha mvua zisizo za kawaida katika nchi za Morocco, Uturuki na nchi za Blakan, Ulaya mashariki na kusababisha ukame mkali katika maeneo mengine duniani. Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani, Michel Jarraud, amesema kuongezeka kwa utoaji wa gesi zinazoharibu mazingira na mgandamizo wake angani kunaisababishia dunia kutokuwa na uhakika wa hali ya hewa na hali mbaya ya baadaye. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...