Saturday, November 08, 2014

WATU 10 WAUAWA KATIKA MLIPUKO NIGERIA

Mlipuko katika eneo la bauchi nchini Nigeria
Ripoti kutoka kaskazini mwa Nigeria zinasema kuwa watu kadhaa wameuawa na mlipuko wa bomu karibu na mashine ya kutoa pesa ya ATM.
Walioshuhdia walisema kuwa ,mwanamume mmoja alikaribia watu waliokuwa wamepanga foleni kwenye mashine hiyo kwenye mji wa Azare ulio katika jimbo la Bauchi .
Walisema kuwa mwanamme huyo alikuwa amebeba bahasha ambayo baadaye ililipuka.
Siku ya Jumatano watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la Boko Haram walivamia kiwanda kimoja cha saruji ambapo walichukua baruti wanayotumia kwenye milipuko. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...