Monday, November 24, 2014

MDAHALO WA JAJI WARIOBA KESHO DAR

Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.PICHA|MAKTABA 
Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), imeandaa mdahalo maalumu wa Katiba utakaofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mlimani City ambao mzungumzaji mkuu atakuwa Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Joseph Butiku alisema jana kwamba mdahalo huo wa amani ni kwa ajili ya Watanzania wenye mapenzi mema na utakuwa wa wazi, ikiwa ni sehemu ya kuziba pengo la mdahalo wa Katiba uliovunjika Novemba 2 ambao ulifanyika kwenye Hoteli ya Blue Pearl.
Ulivunjika baada ya kutokea vurugu zinazodaiwa kuanzishwa na kikundi cha watu kwa lengo la kuvuruga uwasilishwaji wa ujumbe wa Katiba, huku Katibu wa Uhamasishaji wa UVCCM, Paul Makonda akitajwa kinara wa vurugu hizo. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Siku moja baada ya vurugu hizo, Makonda alitumia muda mwingi kujisafisha kuwa alichokifanya ni kumkinga Jaji Warioba asidhurike.
“Tunasema ni mdahalo wa amani na utakuwa wa wazi kwa watu wote wenye mapenzi mema. Tuna mambo mengi ya kujadili, pia tunazungumza kuhusu maadili… Tunaona namna watu wanavyojichukulia fedha za watu bila woga, mdahalo huu unatupa fursa za kujadili kuhusu umuhimu wa Katiba kulinda maadili ya viongozi na vifungu vingine muhimu,” alisema Butiku.
Aliongeza kuwa hiyo ni sehemu tu ya ushiriki wa mijadala na midahalo ya umma kuhusu Katiba Inayopendekezwa, ambayo kwa sasa inaendelea katika maeneo yote ya nchi, ikifanywa na viongozi wa kisiasa, mashirika ya kujamii na hata watu binafsi katika vyombo mbalimbali vya habari.
Alisema japokuwa sasa hivi wamepata ukumbi mdogo unaoweza kuingiza watu 350, watatoa fursa kwa watu kuuliza maswali na kupata majibu kuhusu vifungu na vipengele mbalimbali vyenye utata vinavyoyahusu makundi yote ya kijamii ambayo yamepata uwakilishi katika mapendekezo hayo ya Katiba.
Aliwataja wengine watakaoshiriki kutoa mada kwenye mdahalo huo kuwa ni waliokuwa makamishna wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Butiku mwenyewe, Mohamed Mshamba, Maria Kasonda, Profesa Mwesiga Baregu, Profesa Palamagamba Kabudi na Humphrey Polepole.
Alisema midahalo hiyo ya ndani ni sehemu tu ya mwendelezo wa mijadala inayoendeshwa na taasisi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1997 na kuzinduliwa na Rais wa Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa mjini Mwanza.
“Hawa vijana waliovuruga mkutano wetu wa awali pale Ubungo Plaza, ambao ni vijana wetu na tunawafahamu, hatutarajii kwamba watarudia tena vitendo vya kihuni kama vile. Kimsingi hawana sababu kwa kuwa hawakunyimwa fursa ya kujadili na kutoa mawazo yao, tulishawaonya,” alisema. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...