Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman
Masoud Othman akisindikizwa kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge Maalum leo mjini
Dodoma na Askari Polisi.
|
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud
Othman (mwenye Kaunda suti ya kijivu) akisindikizwa kutoka nje ya viwanja vya
Bunge Maalum la Katiba leo mjini Dodoma na Askari Polisi mara baada ya
kushutumiwa na baadhi ya Wajumbe wa Zanzibar. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
-
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE MAALUM
Kumekuwa na Taarifa potofu zinazosambazwa na
baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii ya kuwa “Mwanasheria Mkuu
Zanzibar Othman Masoud
Othman amekamatwa baada ya
kupiga kura ya hapana Bungeni leo”.
-
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE MAALUM
Tunapenda kuutarifu Umma wa Watanzania kuwa,
taarifa hizo sio sahihi na ni porojo zenye kutaka kuleta hisia potofu kwa
wananchi kuhusu kiongozi huyo.
Ukweli wa Jambo hili ni kuwa Mhe. Othman Masoud
Othman ametekeleza haki yake ya Kidemokrasia
ya kupigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekeza katika Bunge Maalum
leo. Ambapo katika kura alizopiga,
ameweza kuzikubali baadhi Ibara na kuzikataa ibara nyingine katika rasimu ya
Katiba inayopendekezwa.
Pengine hatua hiyo ya kuzikataa baadhi ya Ibara,
haikuwafurahisha baadhi ya Wajumbe na hivyo kuleta majibishano ndani ya Bunge
Maalum wakilalamikia uamuzi wake huo.
Kutokana na hofu hiyo ya baadhi ya Wajumbe
kuanza kupinga uamuzi wake huo ndani ya Bunge, Ofisi ya Bunge Maalum kama
ilivyokawaida kwa kila mjumbe, imeweza kumpatia Ulinzi Maalum wakati akitoka
Bungeni hadi alipoondoka katika viwanja vya Bunge ili asiweze kubugudhiwa kwa
namna yoyote ile kutokana na uamuzi wake
huo.
Suala hili limechukuliwa kipropaganda na kuanza
kueneza uongo katika mitandao ya kijamii kuwa Mhe. Othman amekamatwa baada ya
kupiga kura ya hapana.
Tunapenda kuwahakikishia Watanzania wote kuwa
Mhe. Othman hajakamatwa bali alipewa ulinzi katika Maeneo ya Bunge Maalum jambo
ambalo hufanyika kwa kila mjumbe ambaye kwa namna moja ama nyingine itaonekana
kuna dalili za kubugudhiwa katika Maeneo ya Bunge kutokana na uamuzi au kitendo
alichofanya. Na kutokana na hali ilivyo, ulinzi wake umeimarishwa pia mahali alipo
kwa hivi sasa mpaka atakapomaliza kazi yake hapa Dodoma.
Kanuni za Bunge Maalum zimempa madaraka Katibu
wa Bunge Maalum kusimamia masuala yote ya Ulinzi na Usalama kwa Wajumbe na
Maeneo yote ya Bunge Maalum.
Imetolewa na Idara ya Habari
Ofisi ya Bunge Maalum
Dodoma
1
Oktoba, 2014
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment