Shahidi wa kwanza katika kesi ya
kubaka inayomkabili mwimbaji wa nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha,
ameieleza mahakama jinsi mshtakiwa alivyomkaba shingo na kumziba mdomo
kwa kutumia nguo, kisha kumbaka.
Shahidi huyo ambaye ni shemeji yake, mwenye umri
wa miaka 17, aliyasema hayo jana wakati akitoa ushahidi wake katika
Mahakama ya Wilaya ya Ilala.
Hata hivyo, kesi hiyo ilisikilizwa kwa
faragha (Chamber Cort) baada ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali Nassoro
Katuga kuiomba mahakama kesi hiyo kuendeshwa kwa faragha kwa kuwa
imefikia hatua ya kusikilizwa na sheria inaonyesha kuwa mtoto huyo yupo
chini ya miaka 18.
Ombi hilo lilikubaliwa na pande zote mbili na kesi
hiyo kuendeshwa katika mahakama ya faragha na Hakimu, Wilbaforce
Luhwago aliomba watu wote walikuwepo ndani ya mahakama hiyo kutoka nje
ili kupisha upande wa mashtaka kutoa ushahidi.
Akiongozwa na mwendesha Mashtaka wa Serikali
Nassoro Katuga, shahidi huyo alidai siku ya tukio, Mei 23, mwaka huu,
mshtakiwa aliondoka na mke wake kwenda kufuatilia mkanda wa video lakini
ghafla alirudi nyumbani kwake Tabata Kimanga akiwa peke yake.
Alidai siku hiyo ya tukio mshtakiwa alifanikiwa
kufanya mapenzi na binti huyo na kumwambia asimwambie mtu wakati mke
wake akiwa hayupo nyumbani hapo.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 12,2014. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na Mwananchi
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment