Tatizo: Loic Remy alikaribia kusajiliwa Liverpool kabla ya dili kushindikana.
MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Loic Remy amesema bado haelewi kwanini dili la kujiunga na Liverpool majira ya kiangazi lilivunjika.
Nyota
huyo mwenye miaka 27 alitazamiwa kujiunga Anfield kwa dau la paundi
milioni 8 kabla ya wekundu hao kulitupilia mbali dili hilo wakidai
mchezaji huyo ameshindwa kufuzu vipimo vya afya.
Remy alishindwa kufuzu vipimo vya afya kutokana na matatizo ya moyo na goti, lakini alishangazwa na tangazo hilo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
“Binafsi sikuelewa. Tatizo wakati wa vipimo vya afya? sijui. Walitengenezea, lazima itakuwa hivyo,” aliwaambia Daily Star.
Mfaransa
huyo alirejea QPR na alionekana katika mechi ya ligi kuu kabla ya
kujiunga na Chelsea wiki ya mwisho ya usajili ambapo atacheza kumsaidia
Diego Costa ambaye amepata majeraha ya nyama za paja katika majukumu ya
kimataifa.
Remy,
ambaye aliifungia Ufaransa bao la ushindi dhidi ya Hispania siku ya
alhamisi, alisema; “Kichwani mwangu, nilitaka kuendelea kukaa QPR,
lakini sikuogopa kwa sababu nyingi nilizonazo: Kwa jinsi
nilivyojiimarisha, kujiamini kwangu na kwa namna Chelsea
walivyonihitaji, nilikubali kwasababu hii ni moja ya klabu kubwa
duniani.
“Nina furaha ya kujiunga na klabu hii” Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment