Sunday, August 18, 2013

HII NDIO SABABU ILIYOFANYA AGNESS MASOGANGE KUSHTUKIWA NA POLISI NA HATIMAE KUKAMATWA NA UNGA AFRIKA KUSINI

Imebainika kwamba, Baada ya mpango madhubuti uliosukwa na wauza madawa ya kulevya hapa nchini wakishirikiana na baadhi ya watumishi wasio waaminifu wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam wa kuwasafirisha watuhumiwa hao Agnes Gerald maarufu kwa jina la Masogange na mwenzake Melisa Edward, mtandao huo ulikuwa pia umejipanga vyema nchini Afrika Kusini kuwapitisha watuhumiwa hao bila kukamatwa.

Kilichomponza Masogange kukamwatwa ni pale alipochelewa kutoka uwanjani hapo kutokana na kujiremba, kitu ambacho kilisababisha kufanyiwa upekuzi wa dharura na askari ambaye hakujua kuhusu mpango huo. Tembelea http://jambotz8.blogspot.com/ kila siku.

Taarifa zinabainisha kwamba, baada ya Masogange na wenzake kufanikiwa kupita katika maeneo ya ukaguzi ya uwanja wa ndege wa Oliver Tambo nchini Afrika Kusini, mwenzake waliyesafiri pamoja aliyetajwa kwa jina la Mangunga alifanikiwa kuondoka uwanjani hapo na mabegi matatu yenye jumla ya kilo 60 za madawa hayo ya kulevya bila kujulikana.

"Kilichomponza Masogange ni pale alivyokuwa anajiremba baada ya kuruhusiwa kupita katika vizuizi vyote. Kiuhakika hakukamatwa katika mashine, bali ulikuwa ni ukaguzi usio rasmi uliofanywa na Polisi. Nadhani huyu Askari aliyewashika hakujua kuhusu mpango huo." kilisema chanzo kimoja ndani ya jeshi la Polisi kama ilivyonukuliwa katika gazeti la Tanzania Daima la Tarehe 17/8/2013

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...