Wednesday, June 12, 2013

SUGU AFUNGUKA KUHUSU WAUZA UNGA WANAVYO WATUMIA WANAMUZIKI KUBEBA UNGA


USHUHUDA WA SUGU 
Ukweli wa jinsi matajiri wauza unga wanavyowatumia wanamuziki wa Kitanzania kama punda, unapewa nguvu na ushuhuda aliowahi kuutoa Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’. Mbunge huyo ambaye anapewa heshima kwamba ni mmoja wa waasisi wa Bongo Fleva, alimweleza mwandishi wetu kuwa kabla hajawa memba wa jumba hilo la kutunga sheria, aliwahi kufuatwa na wauza unga kumshawishi awe anabeba mzigo kwenda nao nje ya nchi.
 
 “Jamaa waliniambia kwa sababu mimi nasafiri safiri sana, passport (hati ya kusafiria) yangu itakuwa imeshagongwagongwa sana, kwa hiyo ni rahisi kwenda nchi tofautitofauti kwa urahisi, kwa hiyo wakataka niwe nabeba unga. “Kigezo cha pili waliona kwa sababu mimi ni mwanamuziki,
kwa hiyo ni rahisi watu kuamini ziara zangu ni za kimuziki. Nilikataa, niliwaambia siwezi kufanya biashara hiyo kabisa,” alisema Sugu.
 
 Mwaka 2011, mbunge huyo aliwahi kugusia hilo, wakati akitoa hoja kuchangia bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuwa serikali ni lazima iwasaidie wanamuziki wa Kitanzania kwa sababu wanaibiwa sana, hivyo kuwafanya vijana kuona kimbilio rahisi la kutajirika ni kuuza madawa ya kulevya. “Mheshimiwa spika, serikali isifanye ili kijana wa Kitanzania afanikiwe lazima auze unga, madawa ya kulevya,” alisema Sugu na kueleza mfano huo wa jinsi alivyofuatwa kushawishiwa na matajiri wa unga ili naye awe punda.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...