Wednesday, June 12, 2013

WASTARA AKIRI KUTOKEWA NA MZIMU WA SAJUKI KITANDANI...!!

SIKU chache baada ya staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma kumaliza eda na kurejea Bongo akitokea Uarubuni ameanza kuona maruweruwe ndani ya chumba alichokuwa akilala na mumewe marehemu, Sadick Juma Kiwoloko  ‘Sajuki’, Risasi Mchanganyiko lina habari za uhakika.
 
 
Wastara Juma akiwa na mumewe Sadick Juma Kiwoloko ‘Sajuki’ enzi za uhai wake.
 
Kwa mujibu wa Wastara siku hiyo akiwa amelala chumbani humo, usiku wa manane alihisi uwepo wa Sajuki kitandani kwake.
“Niliongea naye kwa kweli siwezi kukumbuka haswa ni nini tulichoongea lakini tulikuwa katika hali ya furaha sana,” alisema Wastara.
Pia, Wastara alisema kuwa wakiwa katika maongezi yao, aliuchukua mkono wake na kuuweka juu ya mwili wa Sajuki katika hali ya mapenzi na akapitiwa na usingizi.


“Asubuhi nilipoamka nilihisi kama nilikuwa na Sajuki  pale kitandani, kuangalia vizuri, mkono wangu ulikuwa juu ya shuka badala ya mwili wa Sajuki,” aliongeza.
Hata hivyo, Wastara alisema kuwa alihisi ni ndoto lakini alipochunguza alihisi kama kulikuwa na mtu aliyekuwa amelala naye pale kitandani.
“Sijui kama ni maruweruwe, ndoto au Sajuki alikuja kweli kitandani kwangu, kikubwa ninachokiamini ni kwamba mapenzi kwa marehemu mume wangu ndiyo yamepelekea hali hiyo,” alisema

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...