Rais Kikwete. Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia.
RAIS
Jakaya Kikwete amekubaliana na hoja ya Mbunge wa Kuteuliwa, James
Mbatia kuhusu kufanyiwa marekebisho kwa mitalaa ya elimu nchini ili
iendane na viwango vya elimu inayohitajika.
Rais
Kikwete alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na wenyeviti na
wamiliki wa shule na vyuo vya binafsi kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa,
Mbeya.
Katika
kikao cha Tano cha Bunge, Januari mwaka huu, Mbatia aliwasilisha hoja
binafsi kuhusu ubovu wa elimu na mitalaa, hoja aliyodai kufinyangwa na
Bunge kabla ya kupatiwa majibu stahiki na hata kuzua mjadala mkali
miongoni mwa wadau wa sekta hiyo.
Rais
ambaye alizipongeza shule binafsi kwa kufanya vizuri mara kwa mara, pia
aligusia Sera ya Elimu na kusema inaendelea kufanyiwa kazi pamoja na
kuimarisha idara za ukaguzi wa shule ili kuepuka kushuka kwa viwango vya
elimu.
Awali,
katika risala yao, wadau hao wa elimu walilalamikia kodi mbalimbali
zinazotozwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wakisema ndicho chanzo
cha wao kupandisha ada kila mwaka pamoja na mitalaa isiyo na
vigezo.Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamiliki wa Shule na Vyuo, Mahamoud
Mringo alisema:
“Mwaka jana shule 40 zilifungwa kutokana na kuelemewa na mzigo wa kodi mbalimbali na mwaka huu idadi hiyo inaweza kufikia 100.”
“Tunaiomba Serikali ituondolee kodi ya mshahara (Paye)... tutashindwa kuendesha shule kama tutabanwa kupandisha ada.
Serikali
inatubana kupandisha ada, lakini papo hapo inatubana kwenye kodi, kwa
hapa hatuwezi kuendesha shule, lazima tuongeze ada.”
Leo
Rais Kikwete anatarajiwa kuzungumza na wafanyakazi wa Tanzania kwenye
kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) Uwanja wa Sokoine.
http://www.mwananchi.co.tz
No comments:
Post a Comment