Wednesday, May 15, 2013

BABY MADAHA: NAMTAFUTA MWISHO NAMIBIABABY MADAHA: NAMTAFUTA MWISHO NAMIBIA



LICHA ya Mwisho Mwampamba kuwa mume wa ndoa wa Meryl Shikwambane, msanii wa filamu na muziki Bongo, Baby Madaha amesema anajiandaa kwenda nchini Namibia wanapoishi wanandoa hao kwa lengo la kujumuika na Mwisho na kula bata.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Baby alisema bado ana uhusiano wa kimapenzi na Mwisho na kwamba yeye ndiye alimwalika aende Namibia wakafurahie penzi lao

“Nakwenda Namibia kwa Mwisho wangu. Simwogopi huyo Meryl, kwanza yeye ndiye aliyeingilia penzi langu. Mimi ndiye wa kwanza kuwa na Mwisho, hivyo ni halali yangu.

“Mwisho mwenyewe ndiye aliyeniambia niende na amesema nitafikia hotelini, nitafurahi naye kwa muda wote nitakaokuwa huko, mambo mengine mwenyewe ameshayapanga na atajua cha kufanya.”

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...