Na Mtandao
Kwa
mujibu wa orodha ya FIFA ya ubora wa soka duniani iliyotolewa leo
nchini Uswizi, zile timu zilizopo 3 Bora, Spain, Germnay na Argentina
bado zimeshikilia nafasi zao.
Tanzania inayoongozwa na taifa stars chini ya kocha mkuu Kim Paulsen imepanda juu nafasi tatu na kujikita Nafasi ya 116.
Katika
miezi miwili, Tanzania imepanda kwa kasi kutoka nafasi ya 127 mwezi
machi na kwenda nafasi ya 119 mwezi Aprili na sasa imekalia nafasi ya
116 baada ya kushusha kipondo kwa Simba wasiofugika kutoka pwani ya
magharibi mwa Afrika, timu ya taifa ya Cameroon bao 1-0 uwanja wa taifa,
na baadaye kuwatungua simba wa milima ya Atlas, timu ya taifa ya
Morroco mabao 3-1 katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la
dunia.
Wakati
Tanzania ikipanda nafasi tatu juu, Simba watatu yaani timu ya taifa ya
England imeporomoka nafasi 3 na sasa ipo nafasi ya 7 huku wazee wa Samba
na waandaaji wa michuano ya kombe la dunia mwakani, timu ya taifa ya
Brazil ikiporomoka nafasi 1 na sasa ipo ya 19.
Timu
toka Barani Afrika ambayo iko juu sana ni Tembo wa pwani ya magharibi
ya Afrika, timu ya taifa ya Ivory Coast iliyopanda nafasi 1 na sasa ipo
nafasi ya 12.
Orodha nyingine ya timu bora za taifa duniani itatolewa na FIFA Mei 9 mwaka huu.
20 BORA:
1 Spain
2 Germany
3 Argentina
4 Croatia
5 Portugal
6 Colombia
7 England
8 Italy
9 Netherlands
10 Ecuador
11 Russia
12 Côte d’Ivoire
13 Greece
14 Mexico
15 Switzerland
16 Belgium
17 Uruguay
18 France
19 Brazil
20 Denmark
No comments:
Post a Comment