Tuesday, February 19, 2013

BALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI AMALIZA MUDA WAKE AAGA RASMI NA KUONDOKA KUREJEA NCHINI JANA


Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar na Mumewe Bw. Shariff Maajar, wakipata picha ya pamoja na Maofisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani waliofika nyumbani kwake mapema jana asubuhi ya Jumatatu Feb 18, 2013 kuwaaga na kuwasindikiza uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia.
Juu ni Mhe, Balozi na mumewe wakiwa kwenye gari tayari kwa safari ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles.
Mhe. Balozi katika picha ya pamoja na maofisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani waliofika uwanja wa ndege wa kimataifa kuwasindikiza yeye na mumewe (hayupo pichani) waliokua wanaondoka nchini Marekani jana Jumatatu Feb 18, 2013 kurejea Tanzania baada ya Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar, kumaliza muda wake.
Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar na mumewe,  Shariff Maajar, wakiwa wanaelekea kupanda ndege.
Maofisa na wafanyakazi wakiwa na masikitiko huku wakiwaaga kwa macho.
Baadhi ya Maofia wa Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, nchini Marekani, wakiwapungia kuwaaga Balozi na familia yake, wakati wakiondoka.
Container likiletwa kwa ajili ya kupakia mizigo ya Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico aliyemaliza muda wake na RODGERS EXPORTS LLC ya North Carolina ndio imepewa jukumu la kusafirisha mizigo ya Mhe. Balozi. Picha na Vijimambo Blog

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...