Monday, February 12, 2018

MAGAZETI YA LEO JUMATATU FEBRUARY 12, 2018 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

 
Subscribe YouTube Channel @jambotz

ZUMA KUNG'OLEWA LEO...?!!

Kiongozi wa Chama tawala nchini Afrika kusini cha ANC Cyril Ramaphosa amethibitisha kuwa chama kitafanya uamuzi wa mwisho juu ya hatma ya Rais Jacob Zuma.

Akizungumza kaika mkutano wa hadhara mjini Cape Town, Ramaphosa amedokeza kuwa Rais Zuma atatakiwa kujiuzulu.

Amesisitiza kuwa wala rushwa wote wanatakiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria, kitu ambacho anasema Nelson Mandela, baba wa taifa hilo angekitaka.

AGONGWA NA TRENI NA KUFARIKI AKIJIPIGA SELFIE...!!!

Picha haihusiani na tukio hili. 

Mwanamke mmoja amefariki akipiga picha aina ya Selfie na rafikiye katika barabara ya treni nchini Thailand.

Rafiki yake alisema kuwa walikuwa wamekunywa pombe na kuamua kujipiga picha hiyo na treni lakini hawakuona treni nyengine iliyokuwa ikija kutoka barabara nyengine ya treni, kwa mujibu wa polisi.

Miguu yake ilikatika na kufariki hospitalini ambako alikuwa amepelekwa kwa matibabu zaidi.

Rafiki huyo wa kiume alipata majeraha mabaya. Idadi ya watu wanaofariki wakipiga selfie katika maeneo hatari inaongezeka.

Wednesday, February 07, 2018

MKUTANO WA KUMJADILI RAIS ZUMA WAAHIRISHWA

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma

Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kimeahirisha mkutano wa viongozi wa juu wa chama hicho ulio tarajiwa kujadili hatima ya rais Zuma.

Hata hivyo badala yake taarifa iliyotolewa na chama hicho imeeleza kuwa wamekuwa na mazungumzo yenye ufanisi mkubwa na rais Zuma.

Rais Zuma yupo katika wakati mgumu kufuatia shinikizo la kumtaka aachie madaraka ambalo linatoka ndani ya chama chake,halikadhalika upinzani.

Siku ya jumanne bunge la taifa hilo liliahirisha hotuba ya kitaifa iliyotarajiwa kutolewa na rais Zuma.
Hata hivyo baadhi ya mitandao nchini humo imekaririwa ikisema kuwa rais Zuma anajiandaa kuachia madaraka iwapo makubaliano katiika mambo kadhaa yatafikiwa.

Mkutano wa kamati kuu ya chama hicho NEC unatarajiwa kufanyika siku ya februari 17 na 18 kwa mjibu wa taarifa iliyotolewa na kiongozi wa chama hicho cha ANC Cyril Ramaphosa.

Upande wa upinzani wenyewe unashinikiza Zuma kupigiwa kura ya kutokuwa na Imani, huku kikao cha kamati kuu kikidaiwa kuwa na nguvu ya kuweza kumuondoa Zuma madarakani hata bila hiari yake.

Friday, February 02, 2018

MZEE KINGUNGE AFARIKI DUNIA ALFAJIRI YA LEO

Mwanasiasa mkongwe, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia alfajiri ya leo..

Mzee Kingunge enzi za uhai wake amelitumikia Taifa la Tanzania mpaka ngazi za juu kabisa kama vile kuwa Mkuu wa Mkoa, Mbunge na hata Waziri.

Ni mmojawapo wa vijana wa TANU enzi zao hizo, walioshiriki harakati za kuutafuta uhuru mpaka ukapatikana. Yeye kingunge ndiye aliyekabidhiwa jukumu la kuzigawa kadi mia za kwanza kabisa za wana TANU baada ya TANU kuanzishwa ambapo, Bwana Sykes ndiye aliyezichapisha kwa pesa za kutoka mfukoni mwake.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Animal. 

Tuesday, January 02, 2018

TAZAMA PICHA 9 ZA BABU SEYA NA FAMILIA YAKE WAKIWA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM




Disemba 09, 2017 kwenye sherehe za Muungano wa Tanzania, Rais Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa 8,158 ikiwemo familia ya Nguza Viking.

RAIS MUSEVENI ASAINI SHERIA YA KUONDOA UKOMO WA UMRI WA RAIS

Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameidhinisha mswada unaoondoa kikomo cha umri kwa wagombea urais nchini humo, hatua inayompa nafasi ya kuwania tena urais mwaka 2021.

Mswada huo pia unarejesha takwa la rais kuongoza kwa mihula miwili pekee ya miaka mitano.

Kwa kuwa sheria hiyo itaanza kutekelezwa sasa, Bw Museveni anaweza akaongoza taifa hilo hadi 2031.

IKULU YAFUNGUKA KUHUSU KUAPISHWA KWA DR. SLAA

Zikiwa zimetimia siku 40 baada ya kuteuliwa kuwa balozi, Dk. Willibrod Slaa (pichani), hajaapishwa na kuzua minong’ono hatimaye Ikulu imefunguka na kuweka kila kitu wazi.

Itakumbukwa kuwa Rais Dk. John Magufuli alitangaza uteuzi wa Dk. Slaa kushika nafasi ya ubalozi Novemba 23, mwaka jana, lakini tangu wakati huo hajaapishwa.

Rais Magufuli amekuwa na utamaduni wa kuteua viongozi na baada ya siku chache wanaapishwa, lakini kwa Dk. Slaa imechukua muda mrefu na kuibua sintofahamu.

TAZAMA VIDEO YA BABU SEYA NA WANAE WALIPOENDA IKULU KUMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA MSAMAHA ALIOWAPA

Mwanamuziki Nguza Vicking “Babu Seya” na wanae Johnson Nguza “Papii Kocha”, Francis Nguza na Michael Nguza walipofika Ikulu jijini Dar Leo Januari 2, 2018 kumshukuru Rais Magufuli kwa msamaha wake aliotoa kwao dhadi ya kifungo cha maisha walichokuwa wakitumikia gerezani tangu walipohukumiwa miaka 13 iliyopita.

Wednesday, December 13, 2017

VIGOGO WENGINE WA ACT WAHAMIA CCM

 Mwenyekiti na katibu wa Chama cha ACT Wazalendo mkoani Singida, wamejivua uanachana na vyeo vyao na kuhamia CCM.

Viongozi hao ni aliyekuwa mwenyeketi Wilfred Noel Kitundu na katibu wa mkoa wa chama hicho, Loth Robert Thomas.
Viongozi hao wamechukua uamuzi huo mbele ya mkutano mkuu wa uchaguzi CCM mkoa wa Singida uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Uhazili mjini hapa juzi.

Kwa nyakati tofauti walisema changamoto ambazo upinzani walikuwa wakizipigia kelele, Rais John Magufuli ameendelea kuzitatua kwa ufanisi.

Tuesday, December 05, 2017

MBWA WA POLISI WAMUUMBUA ALIEDANGANYA KUWA KAPOLWA MIL. 20 ZA KAMPUNI

Mfanyakazi  wa kampuni ya saruji ya Simba Cement, Edward Ngassa amekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Dodoma kwa tuhuma za kutengeneza tukio la uongo la kuporwa Sh. milioni 20.4 na majambazi jana.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, mbwa wa polisi mwenye mafunzo ndiye aliyegundua udanganyifu huo wa Ngassa nyumbani kwake.

Kamanda Muroto alisema mtuhumiwa huyo alitengeneza tukio la uongo kwamba ameporwa fedha na majambazi katika eneo la Uhindini karibu na mgahawa wa Sunja.

Saturday, December 02, 2017

MKULIMA AFARIKI KWA KUPIGWA NA RADI AKIWA SHAMBANI USIKU

Mkazi mmoja wa kijiji cha Senga Kata ya Kamsamba wilaya ya Momba aliyetambuliwa kwa jina la Cleo Saini (23/25)amefariki baada ya kupigwa na radi alipokuwa analima kwa jembe la kukokotwa na ng'ombe mapema saa tisa usiku.

Pamoja na marehemu kufariki pia ng'ombe wawili waliokuwa wakikokota jembe wamekufa. Mtendaji wa kijiji cha Kamsamba Venance Athanas ametoa taarifa Polisi Kituo cha Kamsamba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Mathias Nyange amekiri kutokea kwa tukio ambapo Polisi wamekwenda eneo la tukio kwa uchunguzi zaidi wa tukio hilo.

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI DECEMBER 02, 2017 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

https://jambotz8.blogspot.com/

 
Subscribe katika YouTube channel ya Jambo Tz upate kuona habari na matukio mbalimbali toka duniani kote.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...