KOCHA mkuu wa timu ya Taifa ya soka ‘Taifa Stars’, Boniface Mkwasa, amesema uwezo mkubwa aliokuwa nao kiungo wa Simba,
ndio umemfanya amuite kwenye kikosi chake kitakachocheza na Chad, Machi
23 kwenye mchezo wa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon),
utakaochezwa mji wa Djamena, nchini Chad.
Mkwasa alimjumuisha mchezaji huyo kwenye kikosi chake hicho chenye jumla ya wachezaji 25, licha ya kuwa tayari ameshatangaza kuacha kuichezea timu ya Taifa ili kutoa nafasi kwa wachezaji wengine.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii jana, Mkwasa alisema, Mwinyi ameonyesha mchango mkubwa kwenye timu yake ya Simba na ndio sababu iliyompelekea kumjumuisha kwenye kikosi chake ambacho kulingana na ratiba ilivyobana anahitaji kuwa na wachezaji wenye uzoefu mkubwa ili kuweza kupambana na Chad kwani hawana muda mrefu wa kujiandaa.
“Hizo taarifa za kuwa amestaafu kuichezea timu ya Taifa sijazipata hivyo haikuwa kikwazo kwangu kumuita, lakini pia bado ana kiwango kizuri ni kijana mkongwe na amekuwa na mchango mkubwa kwenye timu yake, bado ana nafasi kubwa ya kulisaidia Taifa lake,” alisema. Like page yetu ya facebook Jambo Tz