Thursday, March 10, 2016

MKWASA ATAJA SABABU ZA KUMUITA KAZIMOTO

kazimotozKOCHA mkuu wa timu ya Taifa ya soka ‘Taifa Stars’, Boniface Mkwasa, amesema uwezo mkubwa aliokuwa nao kiungo wa Simba, ndio umemfanya amuite kwenye kikosi chake kitakachocheza na Chad, Machi 23 kwenye mchezo wa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon), utakaochezwa mji wa Djamena, nchini Chad.

Mkwasa alimjumuisha mchezaji huyo kwenye kikosi chake hicho chenye jumla ya wachezaji 25, licha ya kuwa tayari ameshatangaza kuacha kuichezea timu ya Taifa ili kutoa nafasi kwa wachezaji wengine.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii jana, Mkwasa alisema, Mwinyi ameonyesha mchango mkubwa kwenye timu yake ya Simba na ndio sababu iliyompelekea kumjumuisha kwenye kikosi chake ambacho kulingana na ratiba ilivyobana anahitaji kuwa na wachezaji wenye uzoefu mkubwa ili kuweza kupambana na Chad kwani hawana muda mrefu wa kujiandaa.

“Hizo taarifa za kuwa amestaafu kuichezea timu ya Taifa sijazipata hivyo haikuwa kikwazo kwangu kumuita, lakini pia bado ana kiwango kizuri ni kijana mkongwe na amekuwa na mchango mkubwa kwenye timu yake, bado ana nafasi kubwa ya kulisaidia Taifa lake,” alisema. Like page yetu ya facebook Jambo Tz


Akizungumzia utovu wa nidhamu aliouonyesha Mwinyi wiki chache zilizopita kwa kumpiga mwandishi wa habari Shinyanga, Mkwasa alisema kama anatuhumiwa kwa vitendo vingine vya utovu wa nidhamu hajawahi kuvionyesha akiwa uwanjani, hivyo hana kikwazo chochote cha kumfanya asimuite kwenye kikosi chake.

“Kama alionyesha utovu wa nidhamu ni nje ya uwanja, nina imani watakaa watazungumza na yataisha kwa amani,” alisema. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

Katika hatua nyingine, imebainika chanzo cha kutemwa kwa winga wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Ngassa, katika kikosi cha Stars ambacho kitavaana na Chad mwezi huu.

Habari ambazo zimelifikia gazeti hili zinadai kuwa Ngassa ambaye anaichezea klabu ya Free State ya Afrika Kusini, amefanyiwa upasuaji wa mguu wake wa kushoto juzi, baada ya kuumia vibaya na atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi miwili au zaidi.

Mkwasa alitangaza kikosi cha wachezaji 25 juzi huku akimtema Ngassa kutokana na matatizo aliyopata pamoja na nyota wengine ambao hawapo fiti kwa ajili ya kuivaa Chad Machi 23, mwaka huu ugenini.

Imeelezwa kuwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lilikuwa tayari limetuma barua kwa klabu ya Free State kwa ajili ya kumuombea ruhusa ya kujiunga na Stars, lakini ikashindikana kutokana na winga huyo kuwa majeruhi.
Kwa sasa Free State inashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi kwa kufikisha pointi 28. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

Na Mtanzania

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...