Tuesday, August 18, 2015

SAUTI SOL KUTAFUTA WACHUMBA TANZANIA


KUNDI linalofanya vizuri na wimbo wao wa ‘Nerea’ kutoka nchini Kenya, Sauti Sol, limetangaza kutafuta wachumba wa kuoa nchini Tanzania, huku wakiwaomba radhi wasichana wa Kenya. 

“Samahani kwa wasichana wa nchini Kenya kutokana na maamuzi yetu ya kutaka kuoa huku Tanzania. Dar es Salaam. Kwa sasa tunatafuta warembo wa kuwaoa,” waliandika wasanii hao kupitia akauti yao ya Twitter. 

Wasanii hao kwa sasa wanafanya vizuri nchini humo na wamefanikiwa kuchukua tuzo mbalimbali nje ya nchi ya Kenya.

Monday, August 17, 2015

ANDY MURRAY ATWAA KIKOMBE


Nyota wa mchezo wa Tenisi, Andy Murray 

Nyota namba tatu kwa ubora wa mchezo wa tenesi muingereza Andy Murray ametwaa ubingwa wa michuano ya Rogers Murray ametwaa ubingwa huu baada ya kumshinda mpinzani wake Novack Djokovic kwa seti 6-4 4-6 6-3 katika mchezo uliochukua muda wa saa tatu.

Kwa ushindi huu Murray anavunja mwiko wa kupoteza mapambano manane dhidi ya Novack ambae anashilikia nafasi ya kwanza kwa ubora.

Murray amemzawadia ushindi huo kocha wake Amelie Mauresmo, aliyepata mtoto wa kiume siku ya jumapili.

ARSENAL YASHINDA, CHELSEA YAPOKEA KICHAPO


Crystal Palace ikimenyana na Arsenal

Ligi kuu ya England imeendelea tena kwa michezo miwili kupigwa katika viwanja vya Etihad na Selhurst Park.

Katika mchezo wa kwanza Arsenal walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace Arsenal walianza kuandika bao lao la kwanza dakika ya 16 liliwekwa kimiani na mshambuliaji Olivier Giroud.

Crystal Palace wakasawazisha bao hilo kupitia kwa mlinzi wake Joel Ward. Bao la kujifunga la beki Damien Delaney likawapa ushindi Arsenal .

Katika mchezo wa pili Chelsea walikubali kichapo cha mabao 3-0 toka kwa Manchester City Magoli ya City yakifungwa na mshambuliaji Sergio Aguero, Vincent Kompany na Mbrazil Fernandinho akahitimisha kwa ushindi kwa bao la tatu kwa mkwaju mkali uliomshinda mlinda mlango wa Man City Joe Hart.

Tuesday, August 11, 2015

SHERIA YA MTANDAO KUANZA KUTUMIKA SEPTEMBA 01

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kiama kwa watumiaji vibaya na wahalifu wote wa mitandao nchini, kuwa siku zao zinahesabika kwani ifikapo Septemba mosi, mwaka huu, Sheria ya Uhalifu wa Mitandao itaanza kutumika na wengi huenda wakaishia gerezani.

Mamlaka hiyo imebainisha kuwa kwa sasa Tanzania inaongoza kwa kuwa na watumiaji vibaya wengi wa mitandao ya kijamii, jambo linalosababisha taarifa za mitandao mingi kutoaminika hadi nchi za nje kutokana na kujaa uzushi, uongo, uchochezi na lugha na picha za matusi.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy alikiri kuwa pamoja na kwamba mamlaka hiyo imefanya kazi kubwa ya kuelimisha jamii juu ya utumiaji sahihi wa mitandao hiyo, bado matumizi yake si mazuri hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi na kwa watu maarufu.

“Napenda kuwatahadharisha Watanzania na watumiaji wa mitandao hii kwa ujumla kuwa sheria hii si ya kupuuzwa, kwani kwa hali ilivyo wengi watatozwa faini na watashindwa kulipa na kuishia gerezani,” alisisitiza. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

MBOWE: NAENDELEA VIZURI



Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe 


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Freeman Mbowe amesema uchovu ndiyo sababu iliyomfanya kuugua ghafla jana na kulazwa katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili, jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika maandamano ya kumsindikiza mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa, kuchukua fomu jana, Mbowe aliugua ghafla eneo la Manyanya, Kinondoni na kulazimika kukimbizwa Muhimbili ambako amelazwa hadi leo.



Hata hivyo, mwanasiasa huyo ambaye anawania ubunge katika jimbo la Hai kupitia Chadema amewahakikisha wanachama na wafuasi wa Ukawa kuwa afya yake ni njema na huenda akaruhusiwa kutoka hospitalini ndani ya saa 48.

Akizungumza na Mwananchi jana, Ofisa Uhusiano wa Muhimbili Aminieli Aligaesha pamoja na kukiri kulazwa kwa mwanasiasa huyo, hakutaka kuweka hadharani kilichokuwa kinamsumbua Mbowe. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

DK. BILALI APUUZA UVUMI WA KUIHAMA CCM

MAKAMU wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal amekanusha taarifa za uzushi ziliposambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa anakihama Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza jana, Katibu wa Makamu wa Rais, Zahor Mohammed Haji kwa niaba ya Dk Bilal, alisema taarifa hizo ni za uongo na uzushi wa aina yake. Zahoro alisema, Dk Bilal yupo nchini Uingereza katika shughuli za ujenzi wa taifa na kwamba hana mpango wa kuondoka CCM na wanaoeneza uzushi huo wana lao jambo.

Katibu huyo amemnukuu Dk Bilal akisema; “Ndugu zangu wa CCM, na Watanzania kwa ujumla, napenda kuchukua fursa hii kuwa taarifu kwamba kuna taarifa inayoenezwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo facebook na whatsApp kuwa nitaitisha mkutano na vyombo vya habari ili kujitoa CCM.

MAGUFULI ATAKA KAMPENI ZA KISAYANSI KUPATA USHINDI WA TSUNAMI

Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli
Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Mtwara nje ya ofisi ya CCM jana. Picha na Ofisi ya CCM 

Waziri wa Ujenzi na mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amesema kuwa wana-CCM mwaka huu wanapaswa kufanya kampeni za kisayansi zaidi kuhakikisha wanapata ushindi wa tsunami utakaowezesha kuundwa kwa Serikali imara itakayowaletea maendeleo Watanzania wote.
Alisema kwa kufanya hivyo kutawasaidia kupata viti vingi na kusimamia shughuli zote za maendeleo na kwa manufaa ya wanaCCM na Watanzania wote kwani mahitaji yao na matarajio yao ni kupata maendeleo makubwa.
“Niwaombe wana CCM wenzangu, tushikamane tuwe wamoja. Kampeni za mwaka huu ni lazima tufanye kampeni za kisayansi zaidi, ni lazima kampeni zianze katika ngazi ya nyumba kumi, vitongoji kwa vitongoji, vijiji, mitaa, kata majimbo, wilaya, mikoa na baadaye urais kwa ujumla. Katika umoja huu nataka niwahakikishie ushindi wa mwaka huu wala si wa kimbunga, ni wa tsunami,” alisema Dk Magufuli. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

LOWASSA AIPAGAWISHA DAR, CHUKUA FOMU YA URAIS NEC


MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na vyama vingine vitatu vya upinzani vinavyounda umoja unaofahamika kwa jina la Ukawa, Edward Lowassa jana alichukua fomu za kuwania rasmi nafasi hiyo kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Lowassa, Waziri Mkuu wa zamani aliyejiunga Chadema hivi karibuni baada ya kushindwa katika mchakato wa kumpata mgombea urais kwa tiketi ya CCM, sasa ameungana na wagombea wengine kujitokeza NEC kuchukua fomu za kuwania urais.

Ametanguliwa na mgombea wa CCM, Dk John Magufuli ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi na Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Dovutwa. Wengine ni Mchungaji Christopher Mtikila wa DP, Mac-Millan Lyimo wa TLP, Hashim Rungwe wa CHAUMMA, Chifu Lutasola Yemba wa ADC na Dk Godfrey Malisa wa CCK. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMANNE AGOSTI 10, YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

Monday, August 10, 2015

WAALIOMUUA JENERALI NSHIMIRIMANA WAKAMATWA

Kiongozi wa mashtaka nchini Burundi amesema kuwa watu kadhaa wanaoshukiwa kutekeleza mauaji ya jenerali Adolphe Nshimirimana wamekamatwa. Hata hivyo Afisa huyo anasema kuwa viongozi waliopanga njama ya kumua jenerali huyo wangali wanasakwa.
Kufuatia mauaji ya kiongozi huyo wa kikosi cha ulinzi wa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, Mwanaharakati maarufu wa haki za kibinaadamu nchini humo alipigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na watu waliokuwa katika pikipiki .

Pierre Claver Mbonimpa alishambuliwa katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura mapema wiki hii. Mbonimpa amekuwa mkosoaji mkubwa wa tangazo la rais Nkurunziza ya kuwania muhula wa tatu.
Hadi kufikia sasa haijajulikana ni nani aliyekuwa amelenga kumtoa uhai.
Wakati huohuo taharuki imetanda katika mji mkuu wa Bujumbura baada ya milio ya risasi kusikika katika maeno kadha ya mji huo usiku wa kuamkia leo.

Hakuna taarifa zaidi ila habari zinasema huenda wanajeshi kadhaa wameuawa na wengine kujeruhiwa. Inaelezwa milio hiyo ya risasi ilisikika baada ya gari moja kutoka ofisi ya Rais wa nchi hiyo kuchomwa moto.
Burundi imekabiliwa na ghasia tangu hatua ya rais Nkurunziza mnamo mwezi Aprili kutaka kuwania muhula wa tatu. Wapinzani wamedai kwamba hatua hiyo ni kinyume na katiba huku jaribio la mapinduzi likifeli mnamo mwezi Mei.

Uchaguzi wa urais ulifanyika mwezi uliopita ambapo bwana Nkurunziza alishinda lakini ulisusiwa na upinzani.

Friday, August 07, 2015

SOMA MAGAZETI YA LEO AGOSTI 07, YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
. .
Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

CHENGE AKIRI KUPOKEA SH. 1.6 BILLION

Mh. Andrew Chenge 

Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge amekiri mbele ya Baraza la Maadili kupokea Sh1.6 bilioni kutoka Kampuni ya VIP Enginering and Marketing Limited, zikiwa ni malipo ya kutoa ushauri.

Pia, alihoji kama kuna tatizo kutumia taaluma yake ya sheria kuzishauri kampuni binafsi na kujipatia fedha.
Chenge ambaye alitoa utetezi wake jana saa 7:30 mchana, alisema hakulipwa fedha hizo kwa sababu ni kiongozi wa umma, bali kwa kutoa ushauri.
Alisema aliingia mkataba na kampuni hiyo wa kutoa ushauri wa kisheria dhidi ya Kampuni ya Mechmer ambazo ni kampuni binafsi zilizokuwa na mgogoro. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

MTIKISIKO: NI BAADA YA PROF. LIPUMBA KUJIENGUA UENYEKITI CUF

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akiaga waandishi wa habari baada ya kuwatangazia kujivua wadhifa huo katika mkutano alioufanya Dar es Salaam jana.

Hakuna neno jingine linalofaa kuelezea hali ilivyo ndani ya Ukawa zaidi ya “mtikisiko” baada ya Profesa Ibrahim Lipumba kuamua kujivua uenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) wakati mkakati wa vyama vya upinzani kushirikiana kutaka kushika dola ukiwa umeshika kasi.

Uamuzi wa Profesa Lipumba, mmoja wa waasisi wanne wa Ukawa-Umoja wa Katiba ya Wananchi unaoundwa na vyama vinne vya Chadema, CUF, NCCR Mageuzi na NLD-,unamaanisha anapoteza wadhifa wake wa mwenyekiti mwenza wa umoja huo ambao umeamua kushirikiana kwenye Uchaguzi Mkuu kwa kusimamisha mgombea mmoja kuanzia ngazi ya urais hadi udiwani atakayeungwa mkono na vyama hivyo.
Wengine walioongoza harakati za kuasisi Ukawa ni Freeman Mbowe, ambaye ni mwenyekiti wa Chadema, James Mbatia wa NCCR-Mageuzi na Emmanuel Makaidi wa NLD. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

Thursday, August 06, 2015

BAYERN MUNICH MABINGWA WA AUDI


Kikosi cha Bayern munich

Miamba ya soka la Ujerumani Bayern Munich wametwaa ubingwa wa michuano ya Audi mwaka 2015.

Bayern wakicheza katika uwanja wao Allianz Arena Jijini Munich, wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya klabu ya Real Madrid ya Hispania.

Bao la ushindi la Bayern lilifungwa Dakika ya 88 na mshambuliaji Robert Lewandowski,alieunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Douglas Costa.

Katika mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu Tottenham Hotspur waliwachapa AC Milan kwa mabao 2-0 kwa mabao ya Nacer Chadli, Dakika ya 8, na Thomas Carroll, Dakika ya 71.

FIORENTINA YAICHAPA CHELSEA KWAO


Kocha wa Chelsea Jose Mourinho

Klabu ya soka ya Fiorentiana ya Italia imewachapa mabingwa wa ligi ya England Chelsea kwa bao 1-0.

Bao pekee la ushindi la Fiorentina ama maarufu kama Viola liliwekwa kimiani na beki Gonzalo Rodríguez raia wa Argentina katika Dakika ya 34 baada ya Kipa wa Chelsea Begovic kutema Shuti la Alonso Mendoza.

Mchezo huu ni wa mwisho wa kirafiki kwa klabu ya Chelsea inayonolewa na Kocha Jose Mournho kabla ya kuanza kwa kipute cha ligi kuu ya Engalnd hapo Augusti 8. Ambapo wataanza utetezi wa ubingwa wao kwa kucheza Mechi yao ya kwanza dhidi ya timu ya Swansea City.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...