Sunday, September 28, 2014

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI SEPTEMBA 28, 2014 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ARSENAL YAPONEA CHUPUCHUPU EMIRATES….OXLADE-CHAMBERLAIN AOKOA JAHAZI

1411841753978_wps_25_Arsenals_English_striker_
Mshambuliaji wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain (kushoto) alifunga goli la kusawazisha dhidi ya Tottenham
MASHABIKI wa Emirates walishangilia kwa matarajio ya kushinda mechi ya watani wa jadi wa kaskazini mwa London baina ya Arsenal na Tottenham, lakini wametoka sare ya 1-1.
Arsenal walitawala mchezo na kushambuli zaidi, lakini hawakuweza kupata magoli.
Tottenham walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 56 kupitia kwa Nacer Chadli, lakini Alex Oxlade-Chamberlain aliisawazishia Arsenal mnamo dakika ya 74.
Arsenal's Alex Oxlade-Chamberlain celebrates scoring the equaliser against Tottenham at the Emirates
Alex Oxlade-Chamberlain akishangilia goli lake. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAANDAMANO YA KUMPINGA KABILA YAFANYIKA

Rais Joseph Kabila
Maelfu ya watu wameandamana nchini Jamhuri ya kidemorasi ya Congo wakimpinga rais wa taifa hilo Joseph Kabila.
Wafuasi wa upinzani wanataka rais Kabila kuondoka madarakani wakati muhula wake wa pili wa uongozi utakapomilika mnamo mwaka 2016.
Kuna shaka kuwa huenda katiba ikabatilishwa ili kumruhusu kuwania muhula wa tatu.
Maandamano kwenye mji mkuu Kinshasa yaliripotiwa kuwa ya amani lakini polisi walitumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji kwenye mji wa Goma ulio mashariki mwa nchi hiyo.
Rais Joseph Kabila alichukua mamlaka mwaka 2001 kufuatia kuuawa kwa babake Laurent Kabila. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

SALVA KIIR ATAKA KUSITISHWA KWA VITA

Rais Salva Kiir na Riek Machar wakibadilishana makubaliano ya kusitisha vita
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amesema kuwa serikali yake imejitolea kumaliza vita nchini nchini humo.
Akiongea kwenye mkutano mkuu wa baraza la umoja wa mataifa mjini New York Kiir ameitaka jamii ya kimataifa kuwashinikiza waasi kuheshimu makubaliano ya kusitisha vita.
Vita vya kisiasa nchini Sudan Kusini kati ya rais Kiir na makamu wake wa zamani Riek Machar vimesababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwalazimu mamalioni ya wengine kuhama makwao.
Mzozo ulianza mwezi Disemba mwaka uliopita na makubaliano ya kumaliza vita yameshindwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

BAHATI MBAYA SIMBA, YANGA HAWAGUSI CHAMAZI…NGOMA INGEKUWA TAMU SANA

azam web_3
UWANJA wa Azam Complex unaomilikiwa na mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc umezidi kuwa mgumu kwa timu za ligi kuu.
Timu pinzani zinapofika maeneo ya Chamazi zinaanza kupata harufu ya kipigo kutoka kwa wenyeji wao.
Chamazi si sehemu salama kwa timu za ligi kuu isipokuwa kwa Simba na Yanga ambao hawajawahi kucheza katika uwanja huo.
Azam fc wakiendelea kuutumia vyema uwanja wao wa nyumbani, jana walishinda mabao 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting ya Mkoani Pwani.
Kabla ya mechi hii, niliandika kupitia mtandao huu nikisema Azam fc wataifunga Ruvu Shooting kwasababu mazingira ya Chamazi ni rafiki kwao na wana kikosi kilichojaa. Nilisema sio rahisi kuifunga Azam katika uwanja wake, hata rekodi zinaonesha hivyo.
Azam walikwenda kupumzika wakiwa mbele kwa bao 1-0 liliofungwa na Mrundi, Didier Kavumnagu katika dakika ya 40. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...