Tuesday, November 05, 2013

MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 05, 2013

DSC 0015 383d6
DSC 0016 21d82

SULEIMAN ANAHITAJI MSAADA WETU AENDE INDIA KUTIBIWA

Wapendwa, Siku ya Leo haikuwa nyepesi kwangu na hata kwa mtoto Suleiman na familia yake, baada ya kupokea ujumbe rasmi kutoka kwa madakatri bingwa wa upasuaji wa Hospitali ya CCBRT kuwa Upasuaji huo HAUTAWEZEKANA kufanyika CCBRT kama tulivyojipa moyo mara ya kwanza.

LAKINI, wamekubali kutusaidia kupata hospitali nzuri nchini India kwa ajili ya kumsafirisha kijana Suleiman. Nguvu zenu zinahitajika sana kipindi hiki kigumu kwa familia hii. Tayari msamaria mwema ametoa tiketi moja ya kumsindikiza Suleiman India. Wapendwa, tushikamane, tunaweza. Hatua zinazofuata:
Kwanza kupata hospitali India.
Kufanya malipo
Kupata barua ya referral na kutafuta passport na visa ya Suleiman na msindikizaji Safari

CCBRT wataturudishia milioni 3 tulizolipa kama gharama za matibabu na tukijumlisha na pesa alizo nazo Imelda tuitakuwa tumebakiwa na shilingi milioni 6.2. Safari ni ndefu lakini msichoke.
Asanteni sana. Mola atuongoze. Amen

PAPII KOCHA, BABU SEYA KAZI IMEKWISHA.

Na Mwandishi Wetu

 MABERE Nyaucho Marando, wakili wa mwanamuziki maarufu nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ amesema amemaliza kazi ya kuwatetea wafungwa hao waliohukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kuwanajisi watoto 12 waliokuwa wakisoma Shule ya Msingi Mashujaa, Sinza jijini Dar es Salaam..........
Babu Seya (wa pili kulia) na Papii Kocha (wa pili kushoto) wakiwa mahakamani kusikiliza rufaa yao.

 Akizungumza na gazeti hili juzi, Marando alisema kazi aliyokusudia kuifanya ameimaliza, sasa anasubiri majaji waliosikiliza alichokisema ili watoe uamuzi wa mwisho lakini pia anamtegemea Mungu.

 “Mimi kazi nimemaliza sasa nawasubiri hao wakubwa (majaji) ili wapime nilichowaambia kwa mujibu wa sheria na kisha watoe uamuzi, lakini pia namtegemea Mungu,” alisema Marando.

SERIKALI YAIRUDISHA DARAJA SIFURI


Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imebatilisha uamuzi wake wa kubadili mfumo wa upangaji wa madaraja ya ufaulu kwa mitihani ya kidato cha nne kama ilivyotolewa awali kwa kurudisha daraja sifuri.

Kutokana na uamuzi huo, sasa daraja la tano lililotangazwa wiki iliyopita kuchukua nafasi ya daraja sifuri sasa limefutwa.

Uamuzi huo umetolewa siku nne baada ya wizara hiyo kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Profesa Sifuni Mchome, kutangaza kuwa serikali imeamua kubadilisha mfumo wa kupanga alama na madaraja ya ufaulu.

Uamuzi wa kushusha alama za ufaulu ulipokewa kwa hisia tofauti na wadau wa elimu nchini ambao walikosoa mfumo huo kwa kueleza kuwa unaipeleka kaburini sekta ya elimu ya Tanzania.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo akizungumza na NIPASHE jana kwa njia ya simu kutoka Dodoma, alisema baada ya kutafakari serikali imeamua kuondoa daraja la tano kama ilivyokuwa imetangaza awali na kurejesha daraja sifuri.

“Kwanza niwaombe radhi Watanzania kwa mkanganyiko huo uliojitokeza ambao ni jambo moja tu limewachanganya, lakini walio wengi wanapongeza mfumo huu wa madaraja, tulichokuja kuharibu ni ‘statement’ ya neno division five,” alisema.

Monday, November 04, 2013

GLOBAL EDUCATION LINK YAZINDUA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU NJE YA NCHI

Mkurugenzi wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia Temu ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyemwakilisha Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mpango wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ya nchi uliofanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Profesa Magishi Nkwabi Mgasa akiwapongeza kampuni ya Global Education Link kwa kushirikiana na Benki ya Afrika (BOA) kwa kuweza kubuni njia itakayowawezesha wanafunzi wengi waliokuwa wanapenda kwenye kusoma nje ya nchi ila wanakosa pesa. Vile vile aliwaomba wanafunzi kuacha kukurupukia vyuo vya nje bila kutambua kama vinatambulika Tanzania ama lah ili kuwaepushia usumbufu.  Uzinduzi huo ulifanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

RAIS KIKWETE NAYE ANAFUATILIWA NA MAREKANI?

kikwete_2e5c8.jpg
NA MWANDISHI WETU
HATUA ya Marekani kudaiwa kufuatilia mawasiliano ya viongozi wa nchi washirika wake wa karibu, sasa ni wazi imeiacha Tanzania katika wingu la shaka, kama viongozi wake nao wanafuatiliwa kwa namna ile ile inayoelezwa na viongozi wa Ulaya. Shaka hiyo inatokana na urafiki wa muda mrefu uliopo kati ya Tanzania na Marekani, ambapo kwa nyakati tofauti, marais watatu wa taifa hilo kubwa duniani wamepata kuzuru nchini.
Kauli tofauti zilizotolewa ndani ya wiki hii na majasusi wa mataifa makubwa duniani, ikiwemo Marekani na Uingereza, wakati wakizungumzia madai ya Marekani kufuatilia mawasiliano ya Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, kwamba nchi zote duniani zinachunguzana, ndiyo ambayo baadhi ya wafuatiliaji wa mambo wanadai kuwa Tanzania bila shaka haiwezi kukwepa kufuatiliwa.


Mbali na hiyo, kauli ambayo imepata kutolewa na mfanyakazi wa zamani wa shirika la NSA, Edward Snowden, kwamba ujasusi huo wa Marekani haufanywi dhidi ya watuhumiwa wa ujasusi na wakazi wa nchi zenye ugomvi na Marekani tu, bali hata marafiki na waitifaki wa karibu kabisa na nchi hiyo, ndiyo ambayo inajenga mazingira ya Tanzania nayo kuwemo kwenye orodha hiyo ya kufuatiliwa.
Marais watatu wa Marekani, kwa nyakati tofauti wamepata kuzuru nchini. Maraisi hao ni pamoja na Bill Clinton, George W. Bush na Barack Obama, ambaye alitembelea nchini mwezi Julai, mwaka huu.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU NOVEMBA 04, 2013

DSC 0002 de89d
DSC 0003 ae6e5
DSC 0004 db5d9

BOBBY WILLIAMSON KOCHA MPYA SIMBA SC

Bobby_3286b.jpg

Maofisa wa ngazi ya juu wa Simba wameanza mazungumzo na kocha Bobby Williamson wa Gor Mahia ya Kenya ili achukue mikoba ya Abdalla Kibadeni.
SIMBA itaanza mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, Januari 26 mwakani dhidi ya Rhino Rangers kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa na kocha mpya, Mwanaspoti linaweza kuthibitisha.
Maofisa wa ngazi ya juu wa Simba wameanza mazungumzo na kocha Bobby Williamson wa Gor Mahia ya Kenya ili achukue mikoba ya Abdalla Kibadeni.
Williamson (52), ni straika wa zamani wa West Bromwich Albion na katika mechi 53 aliyoichezea timu hiyo alifunga mabao 11.
Williamson, ambaye ni raia wa Scotland alijiunga na Gor Mahia msimu huu na tayari ameipa ubingwa wa Ligi Kuu Kenya ikiwa ni miaka 18 tangu timu hiyo itwae ubingwa wa Kenya mwaka 1995.

WAPINGA KUAHIRISHWA KESI YA KENYATTA

130409101249-kenyas-president-elect-uhuru-kenyatta-story-top_ec903.jpg
Waathirika wa kesi inayomkabili rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta wameutaka Umoja wa Mataifa kukataa wito wa kutaka kucheleweshwa kwa kesi dhidi ya Rais Kenyatta katika mahakama ya kimataifa ya ICC mjini The Hague, Uholanzi.
Baadhi ya viongozi wa Afrika wameandaa rasimu ya azimio la kuomba kesi inayomkabili Rais Kenyatta iahirishwe kwa mwaka mmoja kwa masilahi ya usalama wa taifa, kufuatia shambulio la kigaidi katika kituo cha kibiashara cha Westgate mjini Nairobi.
Lakini mwanasheria wa waathirika, Fergal Gaynor, amesema kucheleweshwa kwa kesi kutapunguza nafasi ya kupatikana haki kwa waathirika. 
Bwana Kenyatta anakanusha mashitaka yanayomkabili dhidi ya uhalifu wa kibinadamu, kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007

Sunday, November 03, 2013

DIAMOND PLATNUMZ ATIBUA MSAFARA WA RAIS...!! USALAMA WA TAIFA WATAKA KUMKAMATA...!!!

STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Alhamisi iliyopita alijikuta akiutibua msafara wa Rais wa Zanzibar, Dk. Mohamed Shein kufuatia kuondoka kwenye msiba wakati ilitangazwa kiongozi huyo ndiye aliyetakiwa kuanza kuondoka.
 Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond'.
Ishu hiyo iliyotafsiriwa kama jeuri ya staa huyo ilitokea Mbuzini Mjini Magharibi, Zanzibar baada ya kumalizika kwa mazishi ya baba wa Wema Sepetu, aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania Urusi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Waziri wa Elimu wa zamani katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, marehemu Isaac Abraham Sepetu.  
DIAMOND AINGIA
Awali, wakati waombolezaji wamekaa wakiusubiri mwili wa marehemu ufike, ghafla Diamond aliibuka akisindikizwa na kundi la wapambe mpaka alipokaa.

Diamond akiwa mstari wa mbele wakati wa mazishi ya Balozi Sepetu.
AWEKWA MSTARI WA MBELE
Diamond alipofika aliwekwa mstari wa mbele ambako walikaa ndugu wa karibu na watoto wote wa marehemu. 

  MC ATANGAZA ITIFAKI YA SERIKALI
Mwili ulipowasili, ratiba ya mazishi ikatangazwa na MC ambapo alitaja utaratibu wa mazishi mpaka watu watakaotakiwa kuweka mashada ya maua kaburini, akiwemo Rais Shein. 


Baada ya mazishi, Mwongoza Shughuli ambaye jina halikujulikana aliwaomba watu wote wazingatie itifaki ya usalama wa taifa kwamba ni lazima viongozi wote wa serikali waondoke ndipo waombolezaji wengine watawanyike. “Jamani naomba sana itifaki izingatiwe, asiondoke mtu yeyote kabla ya viongozi wetu wa serikali, akiwemo Rais Shein hawajaondoka,” alisema MC huyo. 
  DIAMOND APUUZA, ANYANYUKA
Baada ya MC huyo kutoa mwongozo, watu wote walitulia wakisubiri kiongozi wa kwanza kuondoka ambaye alikuwa ni Rais Shein kama itifaki ilivyotaka.

HOJA YA KUMNG"OA MAKINDA YAPIGWA KOMBORA

makinda_1af6c.jpg
Mchakato wa kumng'oa madarakani Spika wa Bunge, Anne Makinda(pichani) ambao umeanzishwa na Mbunge wa Nzega, Dk Khamis Kigwangalla (CCM), huenda usifanikiwe kutokana na vikwazo kadhaa vikiwamo kupingwa na baadhi ya wabunge wenye ushawishi mkubwa katika Bunge.  

Wabunge wameanza kumpinga hadharani kuhusu suala hilo ambalo jana mjadala wake uliyateka makundi ya wabunge waliokuwa wakihudhuria vikao vya kamati mbalimbali wakati wakiwa kwenye mapumziko. Katika viwanja vya Bunge jana, gazeti hili liliwashuhudia Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM) na swahiba wake kisiasa, Kangi Lugola ambaye ni Mbunge wa Mwibara (CCM) wakikataa kusaini karatasi waliyopelekewa kuunga mkono kung'olewa kwa Spika.

 Baadaye kwa nyakati tofauti walisema "hoja hiyo haina mashiko" na kwamba hawakutumwa na wapigakura wao kuwania posho bungeni.
Wabunge hao walikuwa wakirejea moja ya hoja za Dk Kigwangalla kwamba Makinda amekiuka kanuni kwa kuidhinisha malipo ya Sh430,000 kama posho kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, tofauti na wajumbe wa kamati nyingine ambao malipo yao ni Sh180,000 kwa siku.
Wengine wanaompinga Kigwangalla ni Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM) na yule wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR - Mageuzi), ambao pia walisema hawaoni sababu za msingi za kumwondoa Makinda madarakani.  

SHEHENA ZA PEMBE ZA NDOVU ZAKAMATWA DAR....!!!

Siku moja baada ya wabunge kuwataka Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki kujiuzulu kwa kushindwa kusimamia Operesheni Tokomeza Ujangili, pembe 706 za ndovu zimekamatwa jijini Dar es Salaam.
Pembe hizo 706 ni sawa na tembo 353 waliouawa katika hifadhi za wanyama pori mbalimbali hapa nchini. Tukio hilo lililotokea jana jioni katika Mtaa wa Kifaru, Mikocheni, wilayani Kinondoni, liliongozwa na Waziri Kagasheki ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Tarish Maimuna.

Waliokamatwa na shehena hiyo ya pembe za ndovu ni raia watatu wa China ambao ni Xu Fujie, Chen Jinzha na Huang Qin wote kutoka mji wa Guandung.

Raia hao wa China wamekuwa wakiishi katika nyumba hiyo kwa miaka mingi wakifanya biashara ya kuingiza nchini vitunguu swaumu kutoka China na kusafirisha nje ya nchi makombe yanayopatikana baharini.

Alipoingia ndani ya nyumba hiyo, Kagasheki ambaye aliambatana na askari polisi na baadhi ya maofisa usalama alishuhudia shehena kubwa ya pembe za ndovu ikiwa imehifadhiwa kwenye viroba vyenye uzito wa kilo 50.

MAMBO YAMWENDEA VIGUMU MASOGANGE.... SADC WAINGILIA HUKUMU YAKE NA KUIPINGA

MAKAMANDA wa vitengo vya kudhibiti madawa ya kulevya kwa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wamemaliza kikao chao jana kujadili mustakabali wa uhalifu ikiwemo hukumu iliyotolewa kwa Mtanzania Agness Gerald ‘Masogange’ aliyekamatwa na malighafi haramu aina ya Ephedrine, Julai 5, 2013 nchini Afrika Kusini kwamba ni ndogo.
Taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi Tanzania zimeeleza kuwa makamanda wa nchi hizo 15 walikutana jijini Arusha kuanzia Jumatatu iliyopita lengo kubwa likiwa kutokubaliana na adhabu zinazotolewa na baadhi ya nchi wanachama kwa wanaokutwa na hatia ya kukamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’.
WALICHOJADILI
Kwa mujibu wa chanzo kilicho ndani ambacho kiliomba hifadhi ya jina kwa kuwa si msemaji, makamanda wa nchi hizo walikuwa na kibarua kizito cha kujadili mbinu mbalimbali za kukabiliana na uhalifu pamoja na hukumu inayotolewa kwa watu wanaokutwa na hatia ya kukamatwa na unga.
“Walijadili matukio mengi ya uhalifu likiwemo suala la madawa ya kulevya, wakajadili mbinu za kukomesha biashara hiyo haramu ili waweze kupata suluhisho la kudumu,” kilisema chanzo hicho.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI NOVEMBA 3, 2013


DSC 0010 e5550
DSC 0011 7d3c1
DSC 0012 731e4

CHELSEA YAFUMULIWA 2-0 NA NEWCASTLE, MAN CITY YAPIGA MTU 7-0 ENGLAND

article-2483669-1924F49800000578-379_634x411_69528.jpg
article-2483669-192508D100000578-811_634x561_0ff39.jpg
Mourinho akimpongeza kocha wa Newcastle baada ya mechi
MABAO ya Yoan Gouffran na Loic Remy yameipa Newcastle ushindi wa 2-0 dhidi ya Chelsea katika Ligi Kuu ya England leo, huku Manchester City ikiifumua Norwich 7-0.
Gouffran alifunga bao lake dakika ya 68 na Remy akafunga dakika ya 89 katika mchezo huo ambao timu ya Jose Mourinho ilikamatwa kila idara.
article-2483669-1924F51B00000578-967_634x471_3689c.jpg
Kikosi cha Chelsea kilikuwa: Cech, Ivanovic, Terry, Luiz, Cole, Lampard/Schurrle dk70, Ramires, Oscar, Mata/Willian dk62, Hazard, Torres/Eto'o dk62Newcastle: (4-4-2): Krul 7; Debuchy 7, Williamson 6, Yanga-Mbiwa 6, Santon 6; Sissoko 8, Cabaye 7, Tiote 6 (Anita 53, 7), Gouffran 7 (Obertan 84); Shola Ameobi 5 (Cisse 62, 6), Remy 7.
Newcastle: Krul, Debuchy, Williamson, Yanga-Mbiwa, Santon, Sissoko, Cabaye, Tiote/Anita dk53, Gouffran/Obertan dk84, Shola Ameobi/Cisse dk62 na Remy.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...