Monday, September 23, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA 23, 2013

DSC 0027 512b4
DSC 0028 c7bcf

MILIO YA RISASI YASIKIKA NDANI YA WESTGATE


kenya 645db
Huku hali ya mshikemshike ikiendelea kushuhudiwa katika jengo la Westgate lenye maduka, ufyatulianaji risasi umesikika ndani ya jengo hilo lenye maduka na mikahawa zaidi ya themanini.


Wapiganaji wa Al shabaab wamewateka nyara raia ambao idadi yao haijulikani. Walikuwemo ndani ya jengo wakiendelea na shughuli zao kuanzia Jumamosi mchana wakati wapiganaji wa Al shabaab walipowavamia na kuanza kufyatua risasi kiholela.

Inaarifiwa kuna maiti kumi katika ghorofa ya kwanza ya jengo hilo.
Inaarifiwa wapiganaji hao wanaoaminika kuwa wanachama wa Al Shabaab ni kati ya kumi na kumi na watano na bado wangali ndani ya jengo hilo.

BARARBARA YA MLIMA KITONGA MKOANI IRINGA KUPANULIWA

Picha-21 d563b
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli (katikati) akipewa maelezo na Meneja wa Tanroads mkoa wa Iringa Eng. Poul Lyakurwa wakati alipokuwa akipita kukagua eneo la Kitonga katika barabara ya TANZAM mkoani Iringa. Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga (kulia) na Eng. Chrispianus Ako kutoka Tanroads Makao Makuu (wa kwanza Kushoto) pamoja na watendaji wengine kutoka Wizara ya Ujenzi.

Kujifunga kwa barabara katika eneo la Kitonga katika barabara kuu ya TANZAM kumekuwa kukisababisha adha kubwa kwa wasafiri. Eneo hilo liko mkoani Iringa katika barabara kuu inayoanzia jijini Dar es Salaam ikiunganisha na mikoa ya kusini magharibi mwa nchi yetu pamoja na nchi jirani za Zambia, Congo DR na Malawi.
Barabara katika sehemu ya Kitonga inapita katika muinuko mkali ambapo inapotokea ajali au gari kuharibika, huwa ni vigumu kwa magari mengine kupita hadi gari lilizoba njia liondolewe.
Hivi karibuni Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alikutana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Dkt. Christine Ishengoma ambapo pamoja ya mambo mengine yaliyozungumziwa katika kikao hicho, lilijitokeza suala la kujifunga mara kwa mara kwa barabara ya TANZAM katika eneo la Kitonga.

"NITAHUDHURIA MKUTANO WA UN, MAREKANI" BASHIR

bashiri cf7dd
Rais wa Sudan Omar El bashir amethibitisha kwamba atahudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa jijini New york juma hili, licha ya kusakwa na mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC.
Bashir anatuhumiwa kwa mauaji ya kimbari katika jimbo la Darfur.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Bashir amesema kuwa tayari amekodisha chumba cha kulala katika hoteli moja mjini humo na kwamba hatishiki kukamatwa na Marekani kwa kuwa sio mwanachama wa ICC.
Hata hivyo haijulikani iwapo atapewa viza kwa kuwa imekuwa utamaduni wa taifa hilo ambalo limetoa vibali hivyo kwa viongozi kama Robert Mugabe wa Zimbabwe na Mahmoud Ahmedinejad wa Iran kuhudhuria mkutano huo. Chanzo: bbcswahili

Sunday, September 22, 2013

"SERIKALI KURUDISHA O’LEVEL KATIKA SHULE KONGWE" PINDA


Pinda1 WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali imeanza kushughulikia utaratibu wa kurejesha utoaji wa elimu ya kidato cha kwanza hadi kidato cha nne katika baadhi ya shule kongwe ili kurudisha ufaulu uliokuwepo na kuimarisha malezi ya watoto kuanzia elimu ya chini.

Amesema uamuzi huo unafuatia kaulimbiu ya kutaka kuwajengea wanafunzi maadili mema katika mazingira ya shule za sekondari tangu wanapoingia kidato cha kwanza badala ya mfumo wa sasa ambapo wanakuja kupata mafunzo hayo kidato cha tano na cha sita lakini wanakuwa hawajapata msingi imara tangu wakiwa wadogo.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumamosi, Septemba 21, 2013) wakati akizungumza na mamia ya wanajumuiya waliohitimu katika shule hiyo (Alumnae), wanafunzi waliopo pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe za Jubilei ya miaka 50 ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo, alikuwa akijibu maombi yaliyotolewa na Dk. Maria Kamm ambaye aliongoza shule hiyo kwa miaka 22 kuanzia mwaka 1970 hadi 1992, pamoja na wazungumzaji wengine katika sherehe hizo.

Alisema Serikali ilikwishatoa maelekezo kwa Makatibu Tawala wa Mikoa kwa ajili ya shule tano ambazo ziliondolewa madarasa ya kidato cha kwanza hadi cha nne na mojawapo ya shule hizo ni Sekondari ya Wasichana ya Weruweru.


PICHA MBALIMBALI ZA SHAMBULIO LA KIGAIDI JIJINI NAIROBI JANA AMBALO LIMEUWA ZAIDI YA WATU 60 NA WATU 100 WAMEJERUHIWA VIBAYA SANA








MATUKIO YALIYOJILI KATIKA MKUTANO WA KATIBA ULIOFANYIKA VIWANJA VYA JANGWANI JANA







 Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Azaveli Lwaitama.




 Askofu Zakaria Kakobe akihutubia katika Mkutano wa Katiba Viwanja vya Jangwani.




 Mbunge wa Ubungo Mh John Mnyika akihutubia katika Mkutano wa Katiba Ulioitishwa na Umoja wa Vyama vya siasa, Wanaharakati na Viongozi wa Dini.

SIMBA, MBEYA CITY ZAINGIZA MIL 123/-

Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Mbeya City iliyochezwa jana (Septemba 21 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 123,971,000.
Watazamaji 21,936 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 32 ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2.
Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 30,064,741.95 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 18,910,830.51. 
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 15,287,156.92, tiketi sh. 3,145,790, gharama za mechi sh. 9,172,294.15, Kamati ya Ligi sh. 9,172,294.15, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 4,586,147.08 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 3,567,003.28.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI SEPTEMBA 22, 2013

DSC 0001 7a34a
DSC 0002 72785

Saturday, September 21, 2013

PENNY......."DIAMOND AKISAFIRI HUWA NAPATA HOMA KABISA"

Penny au sukari ya Diamond
Yule mwanadada anayewapandisha presha wadada wa mujini Penny mungilwa ama ukipenda muite sukari ya Diamond amechonga na thesuperstarstz nakueleza mengi kuhusu sukari wake huyo ambaye kwa sasa yupo nchini malaysia katika bonge la show.

Penny ambaye pia ni mtangazaji wa Tv hapa nchini tanzania amesema kwake hakuna wakati mgumu anaoupata kama Diamond akisafiri penny aliielezea thesupestarstz kuwa anaumia sana kumkosa sukari wake huyo na mara nyingi hujikuta akiugua kabisa kama diamond akimtajia safari.

Penny ameyasema hayo wakati diamond akiwa nchini malaysia kikazi alikokwenda kupiga bonge la show nchini humo na kumuacha penny ndani ya bongo....Kiukweli hakuna wakati mgumu na huwa naumwa kama diamond akisafiri yaani huwez  amini nimemzoea sana bby wangu jamani alisema penny

BAADA YA KUIBA SIMU, IKIPINGWA SIMU YAITA TUMBONI NA BAADA YA DAKIKA 10


Kijana mmoja mkazi wa kitongoji cha DDC Mji mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya, Mkoani Mbeya Bwana GOODSON MWASYOGE amejikuta yupo katika wakati mgumu baada ya kuiba simu ya mfanyabiashara eneo hilo baada ya wiki moja simu hiyo imekuwa ikilia tumboni baada ya kupigwa huchukua kama dakika kumi na tumbo lake kuvimba.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa Bwana ASIFIWE MWAKALONGE amethibitisha kwa tukio hilo akiwa sambamba na mjumbe Bwana MOHAMMED SAID.


Wakati huo huo Kaka wa muhanga wa tukio hili Bwana DANIEL MWASYOGE akiwa na Mama mzazi Bi CHRISTINA MWAKALONGE amemtaka aliyeibiwa simu kumsamehe kijana wao kwa kosa alilolifanya naye amekiri kutenda tukio hilo na anaomba msamaha kuwa abilisi alimpitia tuu hakuwa na tabia ya wizi na baadhi ra wananchi wa mtaa huo wanashangaa.
 

MBEYA CITY FC YAITULIZA SIMBA KWA SARE YA MAGOLI 2 - 2

 KIPINDI CHA PILI KIKIWA KINAENDELEA
 MASHABIKI WAKIWA WANAFUATILIA MECHI KWA UKARIBU 

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPTEMBA 21, 2013

DSC 0014 e5b03
DSC 0015 f1b92

Friday, September 20, 2013

MWALIMU MKUU ANASWA NA MAGUNIA 6 YA BANGI HUKO MKOANI KAGERA.

MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Mukubu, Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Silidion Kaiza (43), anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa na bangi gunia sita.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi alisema kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 17, mwaka huu, shuleni hapo katika kata na kijiji cha Muganza majira ya saa tano asubuhi.
 
Alisema kuwa raia wema walitoa taarifa kituo cha polisi Rulenge kwamba kuna mwalimu anajihusisha na biashara ya kuuza dawa za kulevya, jambo walilohofia kuwa huenda akawaathiri wanafunzi wa shule hiyo kwani anazihifadhi shuleni.

JWTZ LATOA UFAFANUZI KUHUSU AJIRA

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
Simu ya Upepo  : “N G O M E”                Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo  :                              DSM  22150463  
                                                                     Sanduku la Posta 9203,
Telex                     : 41051                            DAR ES SALAAM,19                                                                Septemba, 2013.
Tele Fax                                         : 2153426
Barua pepe          : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                       : www.tpdf.mil.tz
Taarifa kwa vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kuwataarifu Wananchi wote kuwa taarifa zilizoenea kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu za mkononi (sms) na mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba JWTZ limeanza kuajiri wataalamu Jeshini (Professionals) siyo kweli na halina utaratibu wa kutangaza ajira kupitia mitandao ya kijamii au kupitia simu za mikononi.
          Kwa kawaida, utaratibu wa kujiunga na Jeshi hutangazwa kwenye Vyombo vya Habari pale ambapo Jeshi linahitaji kuandikisha askari wapya.  JWTZ huelekeza utaratibu wa kuzingatia katika kuwasilisha maombi husika kwa taarifa hii, wananchi wote wanatahadharishwa kuhusu ujumbe huo unaoelekea kusababisha usumbufu kwa wananchi na JWTZ.  Taarifa hiyo haijatolewa na JWTZ hivyo wananchi wajihadhari na yeyote atakayejitokeza kuwarubuni na hatimaye kutapeliwa kwa namna yoyote.
                       
Imetolewa na:
Kurugenzi ya habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...