Thursday, June 27, 2013

MELI YA MAGUFULI YAZAMA BAHARINI.


 
PICHA ya maktaba ikionyesha meli ikizama baharini.

ILE meli maarufu kwa jina la ‘Meli ya Magufuli’ ambayo serikali iliinasa katika eneo lake la bahari ya Hindi ikivua samaki bila ya kibali, imezama baharini, Tanzania Daima Jumatano limebaini.

Habari ambazo gazeti hili limezipata, meli hiyo ambayo ina uwezo wa kuvua samaki kwenye kina kirefu baharini, imezama  baada ya wajanja wachache kukata vyuma vyake na kuuza kama chuma chakavu.

Kwa mujibu wa habari hizo, wajanja wamekuwa wakiingia na kukata vyuma vya meli hiyo baada ya serikali kuitelekeza kwa muda mrefu bila uangalizi tangu ilipoitaifisha.

Vyanzo vyetu vya habari vilipasha kuwa vyuma chakavu vya meli hiyo vimekuwa vikiuzwa kwa kampuni zinazonunua na kuvisafirisha nje ya nchi na kujiingizia mabilioni ya fedha.

Sehemu kubwa ya vyuma chakavu kutoka kwenye meli hiyo, vimeuzwa kwa kampuni moja inayomilikiwa na mmoja wa wabunge wa Jamhuri ya Muungano.

Inaelezwa kuwa sehemu kubwa ya meli hiyo imetengenezwa kwa malighafi aina ya Brass ambayo kilo moja kwa sasa inauzwa kwa sh 5,200.

Malighafi nyingine zilizotumika na bei yake kwa kilo kwenye mabano vikuzwa kama chuma chakavu ni Cast Aluminum (sh 1,700), Stainless (sh 1,500) na Soft (sh 2,000).


CCM WANG'ANG'ANIA SERIKALI MBILI KATIKA KATIBA MPYA.

 

Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kimemalizika mjini Dodoma huku kukiwa na taarifa kuwa chama hicho kimeweka msimamo wa kutaka kuwepo kwa mfumo wa Serikali mbili katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Mchakato wa Katiba Mpya ya Tanzania upo katika hatua ya rasimu na watu mbalimbali kupitia Mabaraza ya Katiba, wamekuwa wakitoa maoni yao.Tayari Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuwa chama hicho kitakuwa moja ya mabaraza ya katiba na kupata nafasi ya kuichambua, kuijadili na kutoa maoni kuhusu rasimu ilitolewa hivi karibuni na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya mwenyekiti wake Jaji mstaafu Joseph Warioba.
Habari za ndani zilisema kuwa kikao hicho kilichoongozwa na Rais Kikwete kilijadili mchakato wa Katiba Mpya, masuala ya maadili ndani ya chama na kuyatolea uamuzi.


Hata hivyo mmoja wa watendaji ndani ya chama hicho alisema kikao kilikuwa cha kawaida na kwamba kilikuwa kinapitia majukumu na kwamba hakuna kubwa lililojadiliwa. Habari zaidi zinadai kuwa mbali ya kuunga mkono mfumo wa Serikali mbili, CCM imetoa adhabu kwa wanachama wake wawili ambazo zitatangazwa katika siku iliyopangwa.

WATU 10, 799 WANASWA NA DAWA ZA KULEVYA TANZANIA

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Mizengo Pinda

WATU 10,799 wamenaswa wakijihusisha na dawa za kulevya katika kipindi cha miaka mitano pekee na kuonyesha namna gani biashara ya dawa hizo lilivyo tatizo nchini.
Kwa mujibu wa hutuba ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda, iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Urasimu na Bunge) William Lukuvi katika Siku ya Kupiga vita Dawa za Kulevya Duniani ni kwamba biashara ya dawa za kulevya ni tatizo nchini.
Pinda alisema kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.

WATU WA MIKOANI WASHAURIWA KUTOENDA DAR WAKATI WA ZIARA YA RAIS OBAMA HADI ATAKAPO MALIZA ZIARA YAKE.

 

Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe(PICHANI) amewashauri watu walioko mikoani kusitisha safari za kuja Dar es Salaam wakati wa ziara ya Rais wa Marekani, Barrack Obama kutokana na wingi wa wageni katika jiji hilo.

Ugeni huo pamoja na ule wa viongozi kumi na moja kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa Smart Partnership utakaofunguliwa kesho na Rais Jakaya Kikwete kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, umesababisha kuimarishwa kwa ulinzi katika maeneo mbalimbali hasa katika hoteli za kitalii ambazo zimeanza utaratibu wa upekuzi kwa wageni wake.

 

“Hoteli na nyumba za wageni zimefurika wageni na magari mengi yamekodiwa. Kwa ujumla, huduma za kijamii zitakuwa shida,” alisema.

Rais Obama na mkewe Michelle watawasili nchini Jumatatu na tayari wapambe na maofisa usalama kutokana Marekani wameanza kuwasili. Mbali ya ujio huo, wake wa marais kutoka nchi 14 za Afrika watakaokutana na Laura Bush, mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush. Pia Michelle atahudhuria mkutano huo utakaofanyika Jumanne na Jumatano ijayo.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JUNI 27, 2013





KUMEKUCHA BIG BROTHER, MWAKILISHI WA BB TANZANIA FEZA KESSY NDANI YA PENZI ZITO NA O"NEAL WA BOTSWANA

 
FEZA KESSY (TANZANIA)
  
O"NEAL (BOTSWANA) 
Feza akilana denda na O'neal kitandani.

HAKI ZA BINADAMU WAMTAKA WAZIRI MKUU PINDA AOMBE RADHI WATANZANIA, AKIKATA AWAJIBISHWE KWA MUJIBU WA SHERIA....!!!

Akizungumza na waandishi wa habari janaMkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo-Bisimba amesema kitendo cha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuruhusu matumizi ya nguvu kwa polisi dhidi ya raia ni cha kulaaniwa na wapenda haki wote na amemtaka waziri mkuu kuwaomba radhi watanzania.


KUPINGA KAULI YA WAZIRI MKUU "Wapigwe tu" ALIYOITOA BUNGENI TAREHE 20/06/2013

Taarifa hii ni matokeo ya ufuatiliaji wa utendaji wa shughuli za Serikali kama zinavyowasilishwa bungeni na kauli ya Waziri Mkuu (Mtendaji Mkuu wa shughuli za serikali Bungeni) aliyoitoa, Alhamisi ya tarehe 20 Juni 2013, wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo. Waziri Mkuu Pinda, alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama, hususan Jeshi la Polisi kuwapiga wananchi watakao kaidi na kupinga amri halali ya jeshi hilo. Katika tamko hilo, Pinda alisema Serikali imechoshwa na vurugu na kwamba hakuna namna nyingine ya kupambana na wananchi wanaodharau vyombo vya dola zaidi ya kipigo.

Waziri Mkuu Pinda alitoa msimamo huo Bungeni, wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM), aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa na Serikali kufuatia kuwa na matukio ya vurugu ya mara kwa mara nchini, hususan huko Mtwara na Arusha.
Katika majibu yake, Mh. Pinda, pamoja na mambo mengine alisema kuwa; “Mheshimiwa Mangungu hapa ameanza vizuri, lakini mwisho hapa naona anasema vyombo vya dola vinapiga watu, ukifanya fujo au umeambiwa usifanye hiki ukaamua kukaidi utapigwa tu. Akaendelea kusema kuwa, “Lazima wote tukubaliane kuwa nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya sheria na kama wewe umekaidi, unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ndio jeuri zaidi, watakupiga tu.

CHADEMA WAKATAZWA KUVAA KOMBAT BUNGENI...!!

Kombati za CHADEMA mzozo
Siku moja baada ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na wabunge wenzake watatu kuzuiwa kuingia bungeni juzi, uongozi wa Bunge umesisitiza kuwa kombati zao zinakiuka kanuni.

Mbowe na wabunge wenzake wa CHADEMA, Tundu Lissu (Singida Mashariki), Godbless Lema (Arusha Mjini) na Ezekiel Wenje (Nyamagana) walizuiwa na askari kwa madai kuwa wamevalia sare za chama ambazo kikanuni haziruhusiwi.

 

Uamuzi huo uliibua hali ya sintofahamu kwa wabunge wa CHADEMA kutokana na Mbowe kuvalia vazi hilo mara nyingi tangu aingie bungeni mwaka 2010.

Licha ya kanuni za Bunge kuruhusu vazi la ‘safari suti’ kwa wanaume lenye mshono kama kombati zinazovaliwa na baadhi ya wabunge wa CHADEMA, Tanzania Daima Jumatano limebaini kuwa uamuzi huo unaacha maswali mengi yanayohitaji majibu.

Akizungumzia uamuzi huo jana, Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel alisema suti hizo za wabunge wa CHADEMA zilikiuka kanuni ya 149 (3) (b) (i).

Kipengele hicho cha kanuni kinasomeka kuwa inaruhusiwa suti ya Kiafrika au safari ya mikono mirefu au mifupi yenye ukosi au shingo ya mviringo na yenye fulana au bila fulana ndani, ya rangi moja, isiyokuwa na nakshi, pamoja au bila baragashia.

Joel alifafanua kuwa yawezekana huko nyuma wamekuwa wakifanya makosa kwa kuwaruhusu wabunge hao kuingia na suti hizo, lakini sasa kuanzia juzi wameamua kuanza
 kuchukua hatua ya kuwazuia.

“Zile wanasema sio sare ya chama, lakini wote tunawaona kwenye mikutano na shughuli za chama ndizo zinavaliwa na isitoshe tuliwahi kuwatahadharisha kuwa ziko kinyume na kanuni wasizivalie bungeni ila wamekuwa wakiendelea kuzivaa,” alisema.

SAFARI YA RONALDO KUREJEA MAN U YAIVA

ronaldo2 b06e8
CRISTIANO Ronaldo anaweza kurejea Manchester United baada ya kugundulika atakuwa na mkutano na viongozi wa klabu hiyo ya Old Trafford ndani ya siku tatu zijazo. 
Nyota huyo wa Real Madrid amekuwa akihusishwa na kurejea England baada ya kupitia msimu wa bila furaha Bernabeu, lakini ilitarajiwa kuwasili kwa kocha mpya, Carlo Ancelotti kungemfanya abaki Hispania. 
Na gazeti la Hispania, El Pais limeripoti kwamba nahodha huyo wa Ureno atakutana na viongozi wa Man u kabla hajaenda kuanza msimu mpya Madrid.

Kwa kuwa FIFA inazuia klabu kufanya mazungumzo na wachezaji walio ndani ya Mikataba na klabu zao, pande zote zimejipanga kukana kufanya mazungumzo, ambayo itamsaidia sana kocha mpya, David Moyes kuelekea msimu ujao.

Lakini Ancelotti amesema wakati akitambulishwa kuwa kocha mpya wa Madrid leo kwamba: "Cristiano ni mchezaji mkubwa na ninajivunia kufanya naye kazi. 

"Nimewakochi Zidane, Ronaldo na Ronaldinho, na ninajivunia kumuongeza na yeye.' 


Alipoulizwa kuhusu Radamel Falcao, mchezaji aliyekuwa anawaniwa na Madrid ambaye amesaini Monaco, Ancelotti alisema: "Ni mchezaji mzuri, lakini kuna Ronaldo, Higuain na Benzema,"alisema. Chanzo: binzubeiry

Wednesday, June 26, 2013

TANGAZO: NAFASI ZA MASOMO



|             ST. THOMAS INSTITUTE OF TECHNOLOGY & MANAGEMENT
                 
                              P.O. BOX 6089, Morogoro. CEL: 0713 530261, 0717-707025, 0767 530261, 0655 758980
                                                  Email: magkit2005@yahoo.com
Chuo kipo Morogoro mjini, Kilakala. Chuo Kipo katika mazingira mazuri ya kujifunzia. Studio za kisasa kwa wanafunzi wa Uandishi wa habari na Utangazaji.
LIST OF COURSES
S/N
COURSE
DURATION
1
CERTIFICATE IN BUSINESS ADMINISTRATION
1YEAR
2
 CERTIFICATE IN HOTEL MANAGEMENT
6MONTHS
3
CERTIFICATE IN HUMAN RESOURCE MANAGEMENT.
1YEAR
4
CERTIFICATE IN INFORMATION TECHNOLOGY (IT).
1YEAR
5
CERTIFICATE IN COMPUTER SCIENCE.
1YEAR
6
CERTIFICATE IN RECORD MANAGEMENT
1YEAR
7
  CERTIFICATE IN PROCUREMENT AND SUPPLY
1YEAR
8
CERTIFICATE IN NURSERY TEACHING AND KIDERGATEN
6MONTHS
9
CERTIFICATE IN ACCOUNTANCY.
1YEAR
10
CERTIFICATE IN COMMUNITY DEVELOPMENT.
1YEAR
11
CERTIFICATE IN JOURNALISM&MASS COMMUNICATION

1 YEAR
12
BASIC CERTIFICATE IN BUSINESS ADMINISTRATION
6MONTHS
13
BASIC CERTIFICATE IN HUMAN RESOURCE MANAGEMENT.
6MONTHS
14
BASIC CERTIFICATE IN INFORMATION TECHNOLOGY (IT).
6MONTHS
15
BASIC CERTIFICATE IN COMPUTER SCIENCE.
6MONTHS
16
BASIC CERTIFICATE IN RECORD MANAGEMENT
6MONTHS
17
  BASIC CERTIFICATE IN PROCUREMENT AND SUPPLY
6MONTHS
18
BASIC CERTIFICATE IN ACCOUNTANCY.
6MONTHS
19
BASIC CERTIFICATE IN COMMUNITY DEVELOPMENT.
6MONTHS

Kwa wanachuo wa Uandishi wa Habari na Utangazaji Muhula mpya utaanza Rasmi tarehe July 8 mwaka huu..

MZEE MANDELA AFANYIWA MAOMBI MAALUM


 ASKOFU mkuu wa kanisa la kianglikana mjini Cape Town, Afrika Kusini, Thabo Makgoba, amejitolea kufanya maombi kwa niaba ya rais mstaafu Nelson Mandela ambaye anaugua sana hospitalini.
Kasisi huyo anamuombea Mandela aweze kupata nafuu na amewataka wananchi kumshukuru kwa yote aliyowafanyia.
Jamaa za Nelson Mandela wamekutana nyumbani kwake huko Kunu, huku hali yake ya afya ikizidi kudorora hospitalini, Pretoria.
Afya ya Bwana Mandela ilikuwa mbaya zaidi Jumapili.
Maombi hayo yalitolewa baada ya Askofuu huyo kumtembelea Mandela hospitalini ambako kiongozi huiyo wa zamani amekuwa akilazwa kwa wiki mbili na nusu zilizopita baada ya kuugua mapafu.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa wajukuu wa rais huyo wa zamani wa Afrika kusini wanakutana nyumbani kwake kijijini katika mkoa wa Eastern Cape province, ambako viongozi wa kitamaduni wamealikwa.
Halikopta ya jeshi kadhalika zilionekana zikipaa karibu nyumbani kwa mandela. Afisi ya Rais jacob Zuma ilitangaza jumapili kuwa hali ya mzee Mandela ya afya ilikuwa mbaya sana. Chanzo: bbcswahili

Ujio wa Obama: Mashirika ya ndege yatakiwa kubadili ratiba za safari Julai Mosi

Maandalizi ya ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama nchini yanazidi kupamba moto huku maofisa wa usalama wa Marekani wakipiga kambi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.

Aidha, kutokana na ujio huo, Serikali imeagiza mashirika yote ya ndege kubadili ratiba zao za safari Julai Mosi, siku ambayo Rais huo atatua nchini. Jana, waandishi wetu walishuhudia pilikapilika za kuimarisha ulinzi katika uwanja huo jambo ambalo uongozi wa uwanja huo jambo wamelieleza kwamba halijawahi kutokea.
Ulinzi haujawahi kutokea Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Moses Malaki alisema jana kwamba ratiba za uwanjani hapo zitabadilika kutokana na uzito wa ugeni huo.Alisema kwa kawaida anapokuja kiongozi mkubwa wa kitaifa katika uwanja huo hakuna ndege inayoruhusiwa kutua kwa kipindi cha nusu saa. “Ni kweli hali hiyo pia itakuwapo atakapokuja Rais Obama na safari za ndege zitabadilika kulingana na ratiba ya kutua na kuondoka kwa Rais huyo,” alisema Malaki.Pia alisema ulinzi katika uwanja huo umeimarishwa kwa mwezi mmoja sasa na tangu wakati huo, maofisa wa usalama wa Marekani wamekuwa wakifika kwa nyakati mbalimbali. “Sijawahi kuona ulinzi mkali kama huu, wamekuja marais wengi hapa nchini lakini ulinzi huu ni wa kutisha, sijui kwa sababu gani?” alisema Malaki.Alisema awali, wakati maofisa hao walipoanza kuwasili nchini hawakutambua ni mgeni gani anayetarajia kufika lakini baadaye walipelekewa taarifa kuwa ni Rais Obama na baadaye walitaarifiwa kuwa angetua saa 8.40 mchana, Julai Mosi.Mkurugenzi huyo alisema Rais Obama atakuja na ndege nne, moja itakayombeba, ya pili kwa ajili ya mizigo, ya tatu itakuwa ya waandishi wa habari na maofisa wa usalama na ya mwisho ni kwa ajili ya dharura ambayo itaegeshwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

MTOTO WA MNADHIMU MKUU WA JWTZ AFUMWA KWA MGANGA WA KIENYEJI AKIROGA

 
Mama mmoja ajulilikanae kwa jina la Magreth simon Nkwera ambae ni mtoto wa kwanza wa mnadhimu mkuu wa kwanza wa JWTZ Brig Gen Simon Nkwera amekamatwa kwa Mganga wa kienyeji akijaribu kutekeleza jaribio la kuwauwa baadhi ya watoto wa mumewe na baadhi ya ndugu zake huko kibaha maili moja mkoani Pwani na hivi sasa yupo katika kituo cha polisi Maili moja akisubiri kupandishwa kizimbani.
Mtuhumiwa akiwa ndani ya chumba cha mganga na mganga wake aitwae Yahaya tayari kwa mauwaji
Mtuhumiwa huyo akiwa ndani ya gari la polisi baada ya kukamatwa
Mtuhumiwa akiwa anahojiwa na mzee wa ukoo wa shirima Afisa polisi jeshi daraja la Kwanza (woii mstaafu) Joseph Shirima mara baada ya kumkamata live kwa sangoma.
CHANZO VIJIMAMBO

NATASHA AFUNDWA: MASTAA WAKATA MAUNO MBAYA:

Baadhi ya waalikwa wakijiachia pamoja na Natasha (kushoto) wakati wa sherehe hiyo.
Na Imelda Mtema
HUKU siku za kufunga ndoa zikihesabika, mkongwe kwenye filamu za Kibongo, Suzan Lewis ‘Natasha’ amefanyiwa sherehe ya kufundwa kabla ya kwenda kwa mumewe ambayo huko mitaani inajulikana zaidi kwa jina la singo.Shughuli hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, Tandika Maghorofani, Dar ambapo iliandaliwa na shostito wa Natasha aliyejulikana kwa jina moja la Nuru.

APEWA SOMO
Natasha aliwekwa ndani kwa muda wa saa moja akipewa somo la ndoa na watu maalumu walioandaliwa kwa ajili ya shughuli hiyo kabla ya kutoka nje kuungana na wageni waalikwa.

Alipotoka nje, alikutana na waalikwa ambapo kati yao ni mastaa mbalimbali Bongo kisha wakaungana kwenye zoezi zima la kucheza ngoma.
KIASILI ZAIDI
Waalikwa walipata nafasi ya kupakwa urembo mbalimbali wa kiasili usoni na kuifanya hafla hiyo iwe ya kipekee kutokana na vivutio hivyo.
Baada ya yote hayo kukamilika, msafara wa kuelekea nyumbani kwa Natasha, Yombo ulianza huku ngoma zikiendelea kupigwa na mastaa mbalimbali wakikata mauno ndani ya gari.

Akizungumzia shughuli hiyo, Natasha alisema: “Nashukuru sana jamani kwa kupita hatua hii ya kwanza kuelekea kwenye ndoa yangu. Siwezi kuacha kumshukuru zaidi rafiki yangu Nuru kwa kunifanikishia.”

SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU KAULI YA WAZIRI MKUU...YADAI POLISI WANARUHUSIWA KUPIGA NA KUUA KISHERIA

Serikali imetoa tamko bungeni kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi ikieleza kuwa sheria ya kanuni ya adhabu inaruhusu kutumia nguvu za kadiri hata kiasi cha kusababisha madhara au kifo. 
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kunukuliwa bungeni akiwataka polisi kuwashughulikia kwa kuwapiga watu wote wanaokaidi kutii sheria.
“…Nasema wapigwe tu, maana tumechoka sasa,” alisema Pinda alipojibu maswali ya papo hapo Alhamisi iliyopita.
Akisoma tamko hilo bungeni jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima alisema kuwa kifungu cha 18(B) na 18(C) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu kinatoa uwezo kisheria wa kutumia nguvu za kadiri hata ikibidi kiasi cha kusababisha madhara au kifo katika mazingira ya kisheria.
Aliyataja mazingira hayo kuwa ni pamoja na kuokoa uhai wa mtu mwingine, kuzuia madhara makubwa ya mwili yasitokee kwake au kwa mtu mwingine na kumzuia mtu anayetenda tendo ovu la kubaka au kunajisi mtoto au kufanya vitendo kinyume na maumbile.
Pia kumzuia mtu anayevunja nyumba usiku au unyang’anyi wa kutumia silaha au kuchoma nyumba moto au kufanya kitendo chochote kinachohatarisha uhai wa mtu au mali.
Alieleza kuwa Kifungu cha 18 na 18(A) cha Sheria ya Adhabu Sura namba16 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002, kinampa haki mtu yeyote akiwemo askari kujilinda, kumlinda mtu mwingine, kulinda mali yake au mali ya mtu mwingine ikiwemo ya Serikali na taasisi zake, ambayo iko chini ya uangalizi wake kisheria.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...