Wednesday, May 29, 2013

(News) Staki kusikia nyimbo zote za marehemu ALBERT MANGWEAR alizorekodi BONGO REC zikipigwa CLOUDS FM kuanzia sasa.

 Muda mfupi uliopita nilipokea simu kutoka kwa Producer mkongwe hapa bongo anajulikana kwa jina la P Funk Majani na kuniomba nipokee msg hii hapa chini na kuwaomba watanzania walijue hili na baadae atatoa barua rasmi.

TAARIFA YA KIFAMILIA KUHUSU MAZISHI YA NGWEA NA JINSI MWILI HUO UTAKAVYOLETWA TANZANIA

 
Baba Mdogo wa Marehemu Mzee Mangweha ambaye yuko Mbinga Songea kikazi, amesema kuwa wamekubaliana na kaka yake mkubwa yaani baba mkubwa wa Ngwair, David Mangweha ambaye naye yuko Songea kuwa watu watakutanika Mbezi kwa msiba na pia mapokezi yatafanyika hapa Dar es salaam Mbezi Beach. 
Ingawa bado kikao cha familia nzima hakijafanyika lakini baba huyo mdogo amesema wanaweza kulazimika kuzika Morogoro sehemu ambayo baba yake alizikwa.
Baba huyo mdogo alisema kuwa kesho ndo watarudi Dar es Salaam pamoja na kaka yake yaani baba mkubwa wa marehemu. 

Kuhusu mwili kuletwa hapa Tanzania kutoka Afrika Kusini baba mdogo amesema kuwa mpaka sasa hawajajua jinsi gani mwili huo utafika hapa lakini kuna ndugu zao ambao tayari washaanza kufanya taratibu za kuwasiliana na ubalozi wa Afrika Kusini ili kujua ni jinsi gani mwili huo utafika hapa.

Kama kutakuwa na mabadiliko yeyote watakapowasili kesho baba mdogo na baba mkubwa baada ya kikao cha familia watatoa taarifa.

MAAJABU AGNESS JERALD ‘MASOGANGE’ ANASUMBULIWA NA TATIZO LA KUOTA NDOTO MBAYA USIKU NA KUAMKA KISHA KUTOKA NJE NA KUTIMUA MBIO.


VIDEO Queen wa Bongo Fleva, Agness Jerald ‘Masogange’ anasumbuliwa na tatizo la kuota ndoto mbaya usiku na kuamka kisha kutoka nje na kutimua mbio, jambo ambalo kwa wengi linaweza kuonekana kuwa ni maajabu.
 
                                                        Agness Jerald ‘Masogange’.
Habari kutoka kwa sosi wetu, zinasema kuwa katikati ya wiki iliyopita, Masogange akiwa ndotoni, aliamka na kufungua milango na geti la nje kisha kutimua mbio umbali mrefu akiwa na nguo za kulalia na miguuni hana  viatu.

“Bahati nzuri ni kwamba, wakati anahangaika kufungua geti, rafiki yake aliyekuwa amelala naye alishtuka na kushangaa kukuta milango iko wazi. Alipotoka nje, akakuta Masogange ndiyo anamalizia kufungua geti kubwa na kuanza kukimbia hivyo akamkimbiza,” kilieleza chanzo chetu.
Akaongeza: “Lakini pia aliwapigia simu marafiki zake wengine na kuwajulisha juu ya tukio hilo, maana mwenyewe ilikuwa mara ya kwanza kumuona katika hali hiyo.”

MASOGANGE ANASEMAJE?
Risasi Mchanganyiko kama ilivyo kawaida yake ya kutokukurupuka, lilimsaka Masogange kwa simu na kufanikiwa ambapo alithibitisha tukio hilo na kufafanua kwamba liliwahi kumtesa kwa muda mrefu huko nyuma, likaisha.

“Ilikuwa hatari sana lakini namshukuru rafiki yangu kwa kunisaidia. Unajua hili tatizo liliwahi kunitesa sana wakati nikiwa mdogo lakini nilikwenda Mbeya nikapewa dawa tatizo likapotea kabisa hadi juzi liliporudi tena,” alisema.
Habari na Global Publishers.

NGWAIR ALIKUA MUUMINI MZURI, NA MASAA MACHACHE KABLA YA KIFO ALIANDIKA MSTARI HUU KUTOKA KATIKA BIBLIA


MAGAZETI YA LEO JUMATANO MEI 29, 2013

7 02703  1 45fee

SIKILIZA NA DOWNLOAD NYIMBO YA MAOMBOLEZO KWAAJILI YA KIPENZI CHETU ALBERT MANGWEA...R.I.P BROTHER

SONG - R.I.P BROTHER NGWEA
ARTIST - MOZEH THOMAS & MIRROR RHYMES
OVERCLASSIC MUSIC/ EIZER
 SIKILIZA HAPO CHINI...

Click hapa >>>>>         R.I.P NGWEA

 

KAULI YA MAMA MZAZI WA NGWEA..... "MWANANGU ALINIAHIDI KUWA ATARUDI IJUMAA ILIYOPITA"

Marehemu Albert Mangwair enzi za uhai wake.

Akiongea kupitia kipindi cha Amplifire cha Clouds FM, kutoka mkoani Morogoro, mama mzazi wa msanii Albert Mangwair aliyefariki dunia leo akiwa nchini Afrika Kusini, amesema kuwa mara ya mwisho kuwasiliana na marehemu ilikuwa wiki mbili zilizopita ambapo Mangwair alimwambia kuwa mzima na anaendelea vizuri na kwamba angerejea nchini Ijumaa iliyopita. Aliongeza kuwa taarifa za kifo cha mwanaye amezipata jioni hii kwa masikitiko. Wakati Mangwair anaelekea Afrika Kusini hakumuaga mama yake japo akiwa huko alikuwa anawasiliana naye. Kuhusu taarifa za mazishi mama Mangwair amesema bado anasubiri shemeji zake wafike ili wapange. Mungu ampumzishe Mangwair mahali pema peponi. Amen!

MWANA FA NA KALAPINA WAAHIRISHA SHOW ZAO ZA MWISHO WA WIKI KUTOKANA NA KIFO CHA MSANII MANGWEA...

Kutokana na habari za kufariki kwa mwanamuziki Albert Mangwair, msanii ambaye ni mmoja kati ya wana Hip Hop maarufu nchini, Mwanamuziki mwingine pia wa Hip Hop Hamis Mwin'jumah, a.k.a MwanaFA(Pichani)nametangaza kuahirisha show yake ya The Finest iliyokuwa ifanyike Ijumaa hii May 31, 2013.

 
MwanaFA ameiambia Mdimuz Blog kwamba kuguswa kwake na taarifa hizi kumesababisha ajisikie kuomboleza kwanza, kabla maisha mengine hayajaendelea, kwa hiyo amewaomba radhi mashabiki, hasa wale waliokuwa wameshanunua tiketi, na kuwaomba wawe na subira, tarehe y

SIRI YA MAFANIKIO YA MUONEKANO MPYA WA VICENT KIGOSI

Kwa Kipindi kirefu amekuwa akionekana kuwa mwenye mwili nadhifu na
mengine yakizushwa
kwa kila aina ya usemi....Lakini Blog yako ya This is Diamond imeweza
Kujua Lililo nyuma ya pazia...
The Prezdah wa Bongo Movie Vicent Kigosi almaarfu kama
Ray the Greatest, ameamua kueka kando mambo yote ya starehe
na hivi sasa yuko gym kutengeneza
 mwili wake na Afya kwa ujumla ili kulitumikia vyema Taifa lake la
 Tanzania kupitia tasnia ya Film..

Zifuatazo ni Picha kadhaa tu Star Huyo wa BongoMovie akiwa
Gym akitengeneza mwili kiujumla...


Hakika Ray the Greatest  Huu ni mfano wa kuigwa kwa wewe
 mwananchi kwa kufanya mazoezi
kutengeneza afya yako kwa ujumla......

This is Diamond inakutakia Baraka tele na Amani katika kazi
 yako ya sanaa na mipango
Lukuki kwenye jamii....

Tuesday, May 28, 2013

SOMA ALICHOKISEMA BUSHOKE AKIWA SOUTH AFRIKA KUHUSU KIFO CHA NGWAIR

Kuna taarifa kuwa chanzo cha kifo cha ghafla cha rapper Mangweir ni kuzidisha madawa ya kulevya aliyotumia usiku wa kuamkia leo. Inadaiwa kuwa Mangwea alikuwa pamoja na mtu aitwaye M TO THE P ambaye naye yupo mahututi kwa sasa.


Hata hivyo mwenyeji wa rapper Albert Mangwea aliyefariki leo jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini, amesema hit maker huyo wa Mikasi amefariki akiwa usingizini.



Akiongea na Clouds FM muda mfupi uliopita, mwenyeji huyo aitwaye Jonathan amesema usiku wa kuamkia leo Mangwair alirudi nyumbani alikofikia akiwa mzima wa afya lakini mpaka kunakucha hakuonesha dalili za kuamka.

“Sijui hata huko alitumia nini,” amesema.

Ameongeza kuwa asubuhi kulipokucha aliondoka kuendela na mishemishe yake na alipokuwa huko wenzake walimpigia simu kumtaarifu kuwa wamempeleka hospitali ya St. Helen ya jijini humo kwakuwa alikuwa bado hajaamka na ndipo walipogundua kuwa ameshafariki.

Hata hivyo amesema hakuweza kujua sababu za kifo cha Ngwair kwakuwa maelezo ya daktari yalikuwa kitaalam kiasi cha kushindwa kuelewa. Ngwair alikuwa amepanga kurudi leo nchini.

HII NDIO SABABU INAYODAIWA KUSABABISHA KIFO CHA NGWAIR. SOMA HAPA


ripoti kamili
Taarifa Nilizo Pata Kutoka South
Africa Kutoka Kwa Hussein
Original Ambaye Yupo Pretoria
Amesema Ngwear Amefariki Leo

Asubuhi. Alikuwa Ghetto Moja Na
Msanii M To The P.
Walivyokwenda Kuwagongea
Asubuhi Walikuta Ngwear
Amefariki Na M To The P
Amepoteza Fahamu Kabisa. Pia
Daktari Ameshatoa Taarifa Kwa
Watu Wa Karibu Wa Ngwear
Huko South Africa. Ngwea akiwa na msanii M to the P jana south africa.mtu wa karibu anasema walitakiwa kurudi dar leo lakini waliwakuta wamezima kwenye room wote wawili baada ya kuji overdose madawa ya kulevya na M to the P yupo hoi hospitali.

BREAKING NEWZZZZZZZZZZ....!!! MSANII ALBERT MANGWAIR AFARIKI DUNIA LEO HUKO AFRIKA KUSINI


Mwanamuziki wa Hip-Hop ALBERT MANGWAIR amefariki dunia LEO huko Afrika Kusini katika hospitali ya Hellena Joseph.

DR CHENI ALISHWA CHAKULA CHENYE SUMU NA KUKIMBIZWA HOSPITALI, LULU AHAHA HOSPITALINI.



Katika hali ya kushangaza na isiyo eleweka mwigizaji Mahsein Awadhi maarufu kama Dr. Cheni amekumbwa na balaa la kulishwa chakula chenye sumu weekend iliyopita alipokuwa kwenye sherehe moja ya harusi jijini Dar es Salaam alipohudhuria kama MC au mshereheshaji wa harusi hiyo.

Akiongea na bongo movies leo asubuhi, Dr. cheni alisema kuwa baada ya kumaliza kula chakula ambacho alipakuliwa na mmoja wa wahudumu wa sherehe hiyo alianza kujisikia vibaya na kuishiwa nguvu na aliamua kutoka nje kujaribu kupata hewa akidhani ladba ni joto la ukumbini ila hali ilizidi kuwa mbaya na aliamua kutafuta maziwa akihisi labda inaweza kuwa vidonda vya tumbo ndipo alipoanza kutapika na baadae kukumbizwa hospitalini na ndipo alipogungulika kuwa amelishwa chakula chenye sumu.

Tulipomuuliza labda sababu gani anahisi zinaweza kuwa zimepelekea watu hao kutaka kumdhuru alisema kuwa, mpaka sasa hajaweza kupata jibu kamili ila anaamini watu waliofanya hivyo wanamfahamu na wana nia mbaya sana kwake na sio watu wema. Dr. Cheni alisema kuwa kwa sasa hali yake inaendelea vizuri na moja ya watu walikuwa wa kwanza kufika hospitalini baada ya yeye kupatwa na majanga hayo ni mwigizaji Elizabeth Michael (LULU) ambaye kwa sasa yupo karibu sana na Dr. Cheni aliyekuwa mstari wa mbele katika kushughulikia mpaka kufanikisha suala la dhamana ya kesi iliyokuwa inamkabili mwanadada huyo. Pole sana Dr. Cheni.

KIJANA AKUTWA NA SEHEMU ZA SIRI ZA MWANAUME AKIZIUZA

Foster Mangani
Jeshi la polisi nchini malawi wanamshikilia kijana mmoja baada ya kumkuta akiuza sehemu ya siri ya mwanaume.kijana huyo mwenye miaka 24 alikamatwa baada ya wananchi kutoa ripoti kituo cha polisi kuwa kunamzee kalala relini huku akiwa anatokwa damu nyingi ndipo polisi walipofika eneo la tukio na kumkuta mzee huyo akiwa hio na kuamua kumkimbiza hosipitali.
Mtuhumiwa Samuel Banda
 
Baada ya kufikishwa hosipitali ndipo madaktari walipo gundua kuwa mzee huyo alikuwa amejeruhiwa kwa kukatwa sehemu zake za siri,mara moja madaktari walilipoti wa maofisa hao wa polisi na ndipo msako mkali ulipo pita katika wilaya ya Lakeshore huko mjini Salima na polisi hao kufanikiwa kumtia mbaroni kijana huyo baada ya kumkuta kijana huyo akiwa ktk gesti bubu akijaribu kuuza uume huo kwa dola za kimarekani 360.

Polisi walisema mtuhumiwa Samuel Banda alikamatwa na kiungo hicho ambacho alikuwa amekifunga ktk karatasi nyeupe na mtuhumiwa alikiri kuwa huwa anauza viungo mbalimbali vya binadamu kwa wafanya biashara maarufu nchini humo ambao wanaamini wakivipata viungo hivyo huwasaidia katika biashara zao na huwaongezea utajiri.
Mtuhumiwa Samuel Banda

MAGAZETI YA LEO JUMANNE MEI 28, 2013

7 5c323

1 bfd68

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...