Monday, March 25, 2013

LOVENESS LOVE ''DIVA'' AJUTA KUGAWA PENZI KWA MO RACKA

Diva alhamisi iliyopita  alifunguka kuhusu kosa kubwa alilolifanya katika maisha yake tangu azaliwe. Na alichosema kajuta ni kua na uhusiano wa kimapenzi na  msanii Mo Racka. Hiki ndicho alichokiandika Twitter jana usiku




WEMA SEPETU AWAFANYIA SHOPPING YA ZAIDI YA TSH. MIL. 6.5 MBWA WAKE WAWILI






Staa wa bongo movie na mmilikiwa kampuni ya Endless love film anayejulikana kama Wema Isaac Sepetu hivi karibuni amefanya kufuru kwa mbwa wake wawili baada ya ‘shopping’ iliyogharimu dola 4,000 za Kimarekani (zaidi ya TSh. milioni 6.5)

Wema aliteketeza kiasi hicho cha fedha kwa kuwanunulia mbwa hao pafyumu, viatu na nguo, alivyoagiza kutoka nchini China, lengo likiwa ni kuhakikisha wanaishi katika mazingira mazuri.
Baada yay eye kuulizwa alikuwa na haya ya kusema
“Najua watu wanaweza kushangazwa na kitendo cha mimi kutumia kiasi hicho cha fedha lakini sioni kama ni tatizo kwani ni kitu ambacho kinanipa furaha katika maisha yangu.”
Mbwa hao wa Wema Sepetu aliowapa majina ya Van na Gucc wamekuwa ni gumzo kutokana na jinsi anavyowahudumia huku akiajiri watu maalumu wa kuhakikisha wanavaa, kula na kulala pazuri.

KAJALA AHUKUMIWA MIAKA 5, MUMEWE MIAKA 7

HUKUMU ya kesi iliyokuwa inamkabili staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja na mumewe imetolewa leo na Hakimu Sundi Fimbo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar. Katika hukumu hiyo Kajala amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 13 na mumewe kwenda jela miaka saba au kulipa faini ya shilingi milioni 200.
Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe, Faraji Agustino kukumbwa na msala wa kutakatisha fedha haramu.
Wasanii wa Bongo movie wanazichanga hapahapa kuzilipa ila zimepngua kidogo,Wema na Zamaradi wanakimbia ATM KUZICHUKUA ZINGINE.leo leo Kajala anafika nyumbani kwao

ISHA MASHAUZI NAYE BINGWA WA MADAWA YA KULEVYA AKILI MWENYEWE.......!!!


STAA wa muziki wa taarab na mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Aisha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’ ameibua gumzo na kushangaza mashabiki baada ya kukiri kuwa yeye ni mtumiaji wa pombe kali na madawa ya kulevya aina ya mirungi
Ishu hiyo ilijiri Alhamisi ya wiki iliyopita wakati akihojiwa na mtangazaji wa Redio Times FM, Hadija Shaibu ‘Dida’ kupitia kipindi chake cha Mitikisiko ya Pwani ambapo alisema mirungi na pombe kali ndiyo starehe yake kwani inampa stimu kabla hajapanda jukwaani na katika maisha yake ya kawaida nje ya usanii.
Mashauzi alifunguka hayo baada ya Dida kumtaka atoe ufafanuzi juu ya skendo ya kuvuta bangi inayomkabili ambapo alisema siyo kweli kwamba anavuta bangi ila akakiri kuwa anakula sana mirungi na kugida ulabu. Aliongeza kwamba kwa kuwa hana mume, mtoto wala hataki kuwa na familia, mirungi na pombe ndiyo vitu vinavyompa furaha maishani mwake.

UKWELI KUHUSU ELIMU YA NAIBU WAZIRI WA MH. MLUGO HUU HAPA



Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo anadaiwa kutumia ujanja katika wasifu na elimu yake ambapo katika maisha yake ya kielimu ametumia majina manne tofauti.
Philipo Augustine Mulugo ndiyo jina lake halisi ambalo alilisomea mpaka alipohitimu darasa la saba kwa mara ya kwanza 1988, lakini kutokana na kwamba hakufaulu kwenda sekondari alirudia darasa hilo.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi kwa takriban miezi mitatu sasa umebaini kuwa 1989, Mulugo alirudia darasa la saba katika Shule ya Msingi Rukwa ya mkoani Mbeya akitumia jina la Hamimu Hassan.

Imebainika kuwa kabla ya kuhitimu darasa la saba kwa mara ya pili, alibadili jina hilo (kutoka Hamimu Hassan) na kuwa Hamimu Augustino ambalo aliendelea nalo wakati akisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari kutwa ya Mbeya (Mbeya Day) mwaka 1990.

Hata hivyo, Mulugo mwenyewe akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam alipuuza tuhuma hizo kwa kusema kuwa ni njama za kisiasa zinazofanywa na maadui zake. Mulugo anasema madai hayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na amekuwa akiyajibu kwa kuwaonyesha vyeti vyake halali vya shule.

“Hayo madai ni ya muda mrefu, wewe sijui utakuwa mtu wa 20 kuuliza swali kama hilo. Mimi vyeti ninavyo na hata ukitaka ushahidi nitakuonyesha,” alisema Waziri Mulugo na kuongeza:

“Haya mambo kabla hata sijachaguliwa kuwa Mbunge, tulivyokuwa bado kwenye mchujo wa ndani, usiku wa manane watu walisambaza huu uvumi na nilivyoenda kwenye kikao nikatoa vyeti vyangu, wakaviona.”

Waliomfundisha

Baadhi ya walimu waliomfundisha Mulugo, watu waliofanya kazi naye pamoja na wakazi wa Kijiji cha Udinde alikozaliwa, maelezo yao yanathibitisha mabadiliko ya majina ya Mulugo kwa nyakati tofauti pia ngazi mbalimbali za kielimu.

Uchunguzi unabainisha kuwa baada ya kuhitimu kidato cha nne, alifaulu kwenda Shule ya Sekondari ya Wavulana, Songea ambako alisoma kati ya 1994 na 1996 akiendelea kutumia jina la Hamimu Mulugo.

Baada ya kuhitimu kidato cha sita, uchunguzi ulibaini kuwa Mulugo alirejea Mbeya na 1998 alilazimika kubadili tena jina pale alipotumia cheti cha mtu aitwaye Dickson Mulungu, kuombea kazi ya kufundisha katika Shule ya Sekondari ya Southern Highlands.

Habari zinasema Mulugo alichukua hatua hiyo ili kumshawishi mmiliki wa shule hiyo mfanyabiashara, Gulnoor Dossa (sasa ni marehemu), kumpa nafasi ya kufundisha shuleni hapo.

Chanzo: Mwananchi

CHID BENZ AANZA UGOMVI TENA AMPIGA NGWEA CLUB

                                                            Chid Benz

Rapper Chid Benz, amempiga Cow Bama a,k,a Ngwea nje ya Ambassador Lounge ikiyoko Mkapa tower, posta, usiku wa kuamkia leo.ugomvi huo ulitokea baada ya Chid
kumzingua Dully alipokua akiingia, ambapo mwisho wake aliamua kuondoka. Alipoondoka Dully Ngwea akamuuliza inakuaje unamzingua kubwa lao, ndipo Chid alipopaniki na kuanza kutoa lugha chafu huku akitaka kutokumsikiliza Ngwea, inasemekana Ngwea aliamua kukaa kimya lakini Chid aliendelea kungea kwa hasira na kusema "ndio nimemzingua kwani yeye nani" na kumbadilikia Ngwea
 

MADARAJA MAPYA YA KUFAULU KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE

Serikali kwa kupitia wizara ya elimu imefanya mabadiliko kwenye madaraja ya alama za mitihani ya kidato cha nne. Hapo awali, madaraja yalikuwa ni kama ifuatavyo:

A = 81%-100% 
B = 61%-80% 
C = 41%-60% 
D = 21%-40% 
F = 0%-20% 

Mabadiliko mapya yamefanywa na sasa madaraja MAPYA ni kama ifuatavyo:
A = 80%-100% 
B = 65%-79% 
C = 50%-64% 
D = 35%-49% 
F = 0%-34% 
Taarifa imetolewa mapema ili wanafunzi kwa kidato cha nne waanze kujiandaa vyema na mitihani ijayo

MJUE MWANAMUZIKI ALIYEMTOA KAFARA RAFIKI YAKE ILI APATE UMAARUFU


Baada ya kuvuta bangi, mwanamuziki mmoja nchini marekani (RAPER) anayefahamika kwa jila EL-ARMIN amtoa kafara rafiki yake ili kupata umaarufu, raper huyo aliamini akimuua rafiki yake atapata umaarufu nchini marekani na kupaa kama wasanii maarufu nchini humo. vyombo vya habari nchini marekani vimeripoti kwamba El-armin aliamini kwamba kutoa kafara ni ishara ya mafanikio,

Kabla ya kumuua rafiki yake huyo aliwekea risasi kichwani kwa rafiki yake na kusema  "wewe ni kafara yangu" rafiki yake huyo alizuia pisto  na alijua ni utani. baada ya dakika chache El-armin alimshoot rafiki yake tumboni na rafiki huyo kufa papohapo.

Ndoto zake hatimaye zimepote na amefungwa kifungo cha muda mrefu, masupastaa wakubwa kama 50cent, beyonce, lady gaga,kanye west je huwa wanafanya hivyo?

Mbatia aitaka serikali kuacha kutoa maamuzi ya kibabe na badala yake ikae meza moja na wamiliki wa vyombo vya habari.

Na.Mo Blog Team.
Serikali nchini imetakiwa kuacha kufanya mambo bila kutaka ushauri katika masuala ya kuhama kutoka mfumo wa analojia kwenda digitalii na badala yake ikae meza moja na wamiliki wa vyombo vya habari ili kupata muafaka wa kweli na ikibidi ivipe ruzuku ili kuhakikisha uendeshaji wa vituo hivyo katika mfumo huo mpya unafanikiwa.
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi Bw. James Mbatia (pichani), ameitaka  Serikali ikubali kwa nia njema kabisa angalau kwa muda wa miezi sita ijayo au hata mwaka mzima ujao kwa mikoa mitatu, kutumia mfumo wa analojia kwa kuwa ndio walikuwa wamejiandaa nao na ndio walikuwa wamesajili nao vyombo hivi ili kujiandaa kuingia kwenye digitali.
Hata hivyo serikali yenyewe imeshatoa tamko kwamba haitorudia nyuma kwenye mfumo wa analojia na badala yake itaendelea kusonga mbele katika mfumo wa digitali kwani tayari mfumo huo ni mfumo wa kiulimwengu.
Suala hilo limeleta changamoto kubwa na wadau mbalimbali wa masuala haya ya habari ambao wametaka kuwepo na mazungumzo ili kuweza kufikia muafaka mzuri katika uendeshaji wa vyombo hivi vya habari kwa kuwa wenyewe wanaona ni mzigo mkubwa kwa sasa kuingia katika mfumo huo wa digitali.

Rais Xi Jinping wa China awasili nchini kwa ziara ya siku mbili apokewa na Rais Jakaya Kikwete

Rais wa China, Mhe. Xi Jinping na mke wake wakiteremka kwenye ndege mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa Ziara ya Kitaifa ya siku mbili hapa nchini.
Mhe. Rais Xi Jinping na Mhe. Rais Kikwete wakiwa katika Jukwaa Maalum wakati nyimbo za mataifa yao zilipokuwa zikipigwa sambamba na mizinga 21 kwa heshima ya Mhe. Rais Xi Jinping.
Mhe. Rais Xi Jinping akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa kwa heshima yake.
Mhe. Rais Xi Jinping na mwenyeji wake Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwasalimia baadhi ya kina mama wa Dar es Salaam waliofika Uwanjani hapo kwa ajili ya mapokezi.
Mhe. Rais Xi Jinping na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete kwa pamoja na wake zao wakifurahia burudan iliyokuwa ikitolewa na moja ya viku ndi vya burudani vilivyokuwa uwanjani hapo mara baada ya Rais Xi Jinping kuwasili nchini.
Mhe. Rais Xi Jinping na Mhe. Rais Kikwete wakiondoka uwanjani hapo mara baada ya mapokezi.Picha Zote na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Sunday, March 24, 2013

MBEYA WABAINI CHANZO CHA WANAFUNZI KUFELI

Na, Modestus Nkulu

OFISA Elimu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Kaponda ametangaza kiama kwa watu wanaomiliki vituo vya kufundishia watoto masomo ya awali baada ya kubaini kuwa ndiyo chanzo cha kuwa na wanafunzi wanaongia darasa la kwanza bila kujua kusoma na kuandika.

Kaponda aliyasema hayo jana wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mkapa jijini hapa na kuwahusisha watendaji kutoka wilaya zote za Mkoa wa Mbeya kujadili changamoto za maendeleo zinazowakabili wananchi.

Akitoa ufafanuzi, ofisa huyo aliwaambia wajumbe wa kikao hicho kuwa baada ya kubaini hiyo ni moja ya sababu ya kushuka kwa kiwango cha elimu mkoani hapa, ofisi yake imejipanga kuvikagua vituo vyote vya masomo ya awali.

Alisema vituo vingi vya chekechea ndiyo chimbuko la maandalizi mabovu ya wanafunzi wanaoanza darasa la kwanza ambao licha kusoma miaka miwili, wengi wao wamekuwa hawajui kusoma na kuandika hivyo kukosa sifa ya kujiunga darasa la kwanza.
Kaponda alisema hali hiyo imechangia hata wanafunzi wanaojiunga na elimu ya kidato cha kwanza pia baadhi yao kuwa na uwezo mdogo kutokana na msingi mbovu, hivyo kushindwa kusoma na kuandika.
Aidha, ofisa elimu huyo amewatupia lawama wasimamizi wa mitihani kwa kujihusisha na rushwa na kwamba ofisi yake inaendelea kujipanga kukabiliana na changamoto hiyo.
Dk. Michaeli Kadeghe ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, alisema suala la kufeli kwa wanafunzi na baadhi yao kutojua kusoma na kuandika, ni aibu ingawa tayari taarifa zao zinaonesha kuwa wamefaulu mitihani.

Alisema mfumo wa mitaala ya elimu hapa nchini ndilo chimbuko la ubovu huu kwa kuwa haiwezekani wanafunzi wakaendelea kuwa na mfumo wa kuchagua majibu, hivyo ni mambo yanayopaswa kusitishwa haraka.

Mkuu huyo alisema kwa mfumo wa mitaala hiyo, ndiyo inawafanya hata wasiojua kusoma na kuandika kufaulu kwa staili ya kubahatisha katika mitihani yao, hivyo ni wakati mwafaka wa kufanya mabadiliko katika jambo hilo kwa wanafunzi kupimwa uelewa.

Kikao hicho kilichohudhuriwa na watendaji wa serikali kutoka katika wilaya zote za mkoani hapa pamoja na viongozi wa vyama vya siasa na makundi mengine ya kijamii, kilikuwa chini ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Normani Sigala kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Abasi Kandoro.
Chanzo;Tanzania daima

JACK CHUZI WA BONGO MOVIE AOLEWA BAADA YA KUKUBALI KUBADILI DINI....!!!

 Katika Hali ya Kushtusha na Kufuraisha....Staa wa Bongo Movie Jack Pentezel amewashtusha wengi baada ya Kuamua kubadili dini kuwa Muislamu kisha kuolewa na Mpenzi wake wa Muda Gadner Dibibi....

wadau wengi na wapenzi wa Bongo Movie wamekuwa wakihoji juu ya Ndoa Hiyo iliofungwa kisiri sana na kwa haraka,Je Ndoa Hiyo Itadumu? Je ni kweli wamehamua kukaa kwenye Maadili ya Ndoa..? au Ni kama Mchezo wa Mjini kubadilishana Dini na kuoana mwishowe ni kuachana....Tusubiri Tuone.....

Mpekuzi  inapenda kumtakia Jack Pentezel na Mumewe Gadner Dibibi Baraka Tele,Amani na Upendo utawale kwenye Maisha yao ya Ndoa..





MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMJULIA HALI MZEE KINGUNGE NYUMBANI KWAKE

1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, wakati alipofika kumjulia hali nyumbani kwake Victoria jijini Dar es Salaam jana Machi 23, 2013 baada ya mzee Kingunge kulazwa Hospitali ya Muhimbili kwa uangalizi hivi karibuni alipougua ghafla. Picha na OMR2Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, wakati alipofika kumjulia hali nyumbani kwake Victoria jijini Dar es Salaam jana Machi 23, 2013 baada ya mzee Kingunge kulazwa Hospitali ya Muhimbili kwa uangalizi hivi karibuni alipougua ghafla. Kulia ni Mke wa Mzee Kingunge. Picha na OMR3Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, wakati alipofika kumjulia hali nyumbani kwake Victoria jijini Dar es Salaam jana Machi 23, 2013 baada ya mzee Kingunge kulazwa Hospitali ya Muhimbili kwa uangalizi hivi karibuni alipougua ghafla. Picha na OMR

WASICHANA WADOGO NAO WAINGIA KATIKA BIASHARA YA NGONO KWA SH. 5000

Ni usiku wa saa 4 nipo katika eneo maarufu la Buguruni lililopo jijini Dar es Salaam nikiwa nimekaa napata kinywaji kwenye baa moja.

Katika eneo hilo ambalo lipo pembezoni mwa Barabara ya Mandela si tulivu sana kutokana na pilika pilika za magari na watu wanaopita karibu kwa shughuli mbalimbali.
Huku nikiendelea kupata kinywaji mara naona wasichana wadogo wenye umri wa miaka 14 hadi 16 wakizunguka zunguka katika eneo hili la baa.

Awali nilifikiri walikuwa wakitafuta msaada au wakipita kuelekea nyumbani kwao, kwani umri wao haukunipa picha kwamba walikuwa kazini wakati huo wa usiku wa kiza kinene.

Kilichonifanya niwaangalie kwa udadisi zaidi ni kuona jinsi walivyovaa nguo ambazo zilionyesha nusu ya sehemu zao za mapaja, huku kifuani wakiwa wamevaa blauzi zilizobana zikionyesha matiti yao madogo ambayo yanaanza kuchipua.

Kilichonitisha zaidi ni kuona wasichana hawa ambao wakati huo walipaswa kuwa nyumbani wakiwa mkononi wameshika vinywaji vikali aina ya ‘viroba’ na wengine wakivuta sigara.

Hawa ni sehemu ndogo tu ya wasichana wadogo ambao hukesha usiku kucha katika baadhi ya mitaa ya jiji la Dar es Salaam wakitafuta wateja ili wapate fedha za kujikimu.
Mwandishi analazimika kuwadadisi wasichana hawa ili kujua nini kilichosababisha waingie katika biashara hii.

Inavyokuwa
Mwandishi ana mwita mmoja wa wasichana hawa Neema Mashiri (16) (sio jina lake halisi) na kuongea naye katika sehemu tulivu katika baa hiyo huku wakitumia vinywaji kunogesha mazungumzo.
Neema akiwa mwenye kujiamini na kazi yake bila ya kutetereka anasema kazi hiyo aliianza zaidi ya miezi sita nyuma huku akiwa tayari amekutana na idadi ya wanaume ambayo haikumbuki kutokana na wingi wake.
“Kwa siku moja nakutana na wanaume katiya watano hadi saba na hii hutegemea siku na siku, kwani kuna siku huwa na biashara ya kutosha na tunapata fedha za kutosha,”anasema Neema.
Neema akieleza ujira ambao hulipwa anasema ni Sh3,000 hadi Sh5,000 kwa muda usiozidi dakika 30 kwa mwanamume mmoja huku wakati kwa yule anayetaka kulala naye hadi asubuhi hutakiwa kulipa Sh10,000 hadi Sh15,000.
“Baadhi ya wanaume wamekuwa wakitufanyia vitendo vya kikatili kwa kutuingilia kinyume cha maumbile, lakini kutokana na hali ngumu ya maisha hukubali kwani dau huwa kubwa Sh10,000 hadi Sh12,000, lakini wengine hutumia ubabe tu na kututumia bila kutulipa,” anasema Neema na kuongeza;

WANAFUNZI WA CHUO CHA UTUMISHI WAJIPIGA PICHA CHAFU WAKATI WAKIFANYA ZINAA....!!

Wanafunzi  watatu  wa chuo  maarufu  nchini wametia aibu ya mwaka   baada  ya  kunaswa wakivunja  amri ya  sita  huku  wakijipiga  picha  chafu  za  tukio  hilo.....

Kwa mujibu wa ripota wetu, tukio hilo la aibu  linahusisha  wanaume  wawili  na  msichana  mmoja  aliyetambuliwa  kwa  jina  moja  la  Fetty.....

Katika tukio  hilo la aina yake, Fetty  anaonekana  akigawa  penzi  kwa  jamaa    huku  jamaa  mwingine  akiwapiga   picha  hatua  kwa  hatua.....

Kuvuja  kwa  picha:
Picha  hizi  zinadaiwa  kusambaa na kumfikia  mpekuzi wetu  baada  ya  wanafunzi  hao  kutofautina  na  hivyo  kuamua  KUTUBU  DHAMBI  HII  kwa  staili  ya  KUUMBUANA
 

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...