Saturday, March 02, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 2/3/2013





UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
Academic Staff Assembly


Utangulizi

Wapendwa waandishi wa habari. Tunaomba kupitia ninyi tuweze kuongea na watanzania wenzetu kuhusu hali ya amani ilivyo nchini mwetu kufuatia kila aina ya dalili ya watanzania kukosa uvumilivu wa kidini. Tunatambua kuwa serikali yetu imefanya mambo mazuri mengi tu nchini, hilo hatuna mashaka nalo; hata hivyo kama watanzania tunadhani kuna baadhi ya mambo hayaendi sawa. Hivyo basi, tunaomba kuchukua nafasi hii kuelezea wasiwasi wetu kuhusu migogoro hii ya kidini inayozidi kukua nchini.

Migogoro hii ilianza kuvuka kama moshi lakini sasa inaanza kulipuka na kusambaa zaidi. Tumeshuhudia uchomaji moto wa kanisa kule Mbagala, kumwagiwa tindikali shekhe mmoja kule Zanzibar na Shekhe mwingine kuuawawa, kuchomwa makanisa Zanzibar, kupigwa risasi viongozi wa kikristo kule Zanzibar na pia mgogoro wa kuchinja huko Geita ambako tumeshuhudia mchungaji mmoja akiuawa.

Mbali na hayo, kuna matukio kadhaa kwenye shule zetu za sekondari yakihusisha migogoro ya kidini kati ya wakristo na waislamu. Haya tumeshahudia yakitokea sekondari za Bagamoyo, Ndanda, Kibiti, Ilboru na kwingineko. Pia yapo malalamiko yasiyo rasmi kuhusu udini kwenye sehemu za kazi na kwenye taasisi mbalimbali za serikali. Wapo wanaodai kuwa baadhi ya taasisi binafsi, za kidini na hata za serikali zinazohudumia watanzania wengi zimekuwa zikiajiri wafanyakazi kwa misingi ya kupendelea dini fulani fulani. Jambo hili hata kama ni la kuzungumzwa tu, ni vema likafanyiwa kazi maana hisia hizi zikipanuka hujenga chuki na kusababisha watanzania wasielewane.
Read more

Friday, March 01, 2013

SOGGY DOGGY "HUNTER" AACHA KAZI UHURU FM,ATIMKIA KWA WANYARU-IRINGA

 


Msanii/Mtangazaji Soggy Doggy ameacha mzigo pande za redio Uhuru na leo rasmi ameondoka Dar es salaam nakwenda Iringa ambapo atakuwa akifanya kazi katika kituo kingine cha Redio kinachoenda kwa jina la Ebony Fm.Soggy Doggy ashawahi kufanya kazi katika vituo vya redio mbalimbali hapa nchini kama Arusha na Mwanza.

Mtendaji mkuu TAZARA Bw. Akashambatwa Mbikusita-Lewanika aachia ngazi.



Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) Bw. Akashambatwa Mbikusita-Lewanika,(Pichani) hatimaye ameachia ngazi baada ya kuendesha kampeni kali ya miezi kadhaa kutaka aendelee kuongoza Mamlaka hiyo kwa miaka mingine mitatu.
Hatua hiyo ya kuachia ngazi imekuja baada ya Bodi ya Wakurugenzi na Baraza la Mawaziri la Mamlaka hiyo kuonyesha dhahiri kutotaka Mzambia huyo aendelee na uongozi wa TAZARA kutokana na utendaji wake mbovu na uongozi mbaya uliowabagua wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kwa misingi ya utaifa wao.
Habari za ndani za Mamlaka hiyo zimesema Bw. Akashambatwa ambaye kipindi chake cha uongozi kiliisha tarehe 22 Januari, 2013 kiliongezwa kwa maombi maalum ya Serikali ya Zambia kwamba Serikali hiyo ilihitaji muda mrefu kidogo kumpata mbadala wake, licha ya Serikali ya  Tanzania kutoridhishwa na utendaji wake.
Katika kikao chake cha tarehe 20 Februari, 2013 jijini Lusaka, Zambia, Baraza la Mawaziri lilijadili kwa siri na kwa kirefu suala la mtendaji Mkuu huyo ambaye inasemekana aliombewa tena na Serikali ya Zambia kipindi cha nyongeza, ombi ambalo inadaiwa lilipingwa vikali na ujumbe wa Serikali ya Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe.
Taarifa za uhakika ndani ya Wizara ya Uchukuzi zinasema Serikali ya Tanzania haikumtaka Mtendaji Mkuu huyo kwa sababu kadhaa zikiwemo :uwezo mdogo, ubadhirifu, kuchochea ubaguzi kati ya Watanzania na Wazambia, ukaidi na uchochezi. Inadaiwa kuwa Mtendaji Mkuu huyo alizuia kuanzishwa kwa mradi wa usafiri jijini Dar es Salaam bila sababu yoyote ya msngi na kuishia kusambaza taarifa za uongo na uchochezi Zambia na magazeti mbalimbali nchini.
Tarehe 25 Februari, 2013 Gazeti la kila siku la Zambia, Zambia Daily Mail, liliripoti tukio hilo la kuachia ngazi kwa kiongozi huyo ambaye anajulikana sana nchini Zambia kama mfanyabiashara na kiongozi wa kimila (chief),                                              
Gazeti hilo lilinukuu barua ya Bw. Akashambatwa ya tarehe  22 Februari, 2013 kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Ujenzi, Ugavi na Mawasiliano ya Zambia, akielezea kuwa hakuna faida ya kuomba kurefushwa kwa mkataba wake wakati vyombo vikuu vya uongozi vya TAZARA, Bodi ya Wakurugenzi na Baraza la Mawaziri, havionyeshi kumkubali.
Kuondoka kwa Bw. Akashambatwa kwenye uongozi wa TAZARA kunatarajiwa kupokewa na wafanyakazi wa TAZARA kwa nderemo na vifijo.

Google Waja na Miwani Inayopiga na Kurekodi Picha kwa Maelekezo.

Glass ya google
TEKNOLOJIA waliyotumia Google kutengeneza miwani ambayo ina uwezo wa kumpiga picha mtu au kurekodi bila muhusika kujua (google glass) sio mpya ila Kampuni ya Google ndio wakwanza kuja na teknoloji hiyo, ili kila mtu aweze kutumia na inakadiriwa huwenda bidhaa hii ikafanya vizuri sana katika mauzo.
Google glass ni rahisi sana kutumia, kama unataka kupiga picha unachotakiwa kusema ni “OK Glass, take a picture.” upo kwenye foleni unaona fujo unataka kuchukua video, mwambie Google Glass naye atakusaidia kuchukua video. Hii ndio kali, unataka kuwaonyesha ndugu na marafiki kitu unachokiona wakati huo huo? Google glass inafanya yote hayo, inakuja na kitu kama “Skype-style video chat”.
Umesafiri kwenda kuchukua mzigo China? Google glass itakusaidia kuchukua kutafsiri lugha. Umeenda Zanzibar kutembelea majengo ya kitalii na unabaki kushangaa shangaa, uliza Google glass na itakupa tour guide.
Google glass ni kifaa ambacho unaweza kutumia kurekodi video, kupiga picha, kutafuta habari katika Google, kutafsiri lugha, na unaweza fanya yote haya bila kutumia mikono yako (hands free). Tatizo ni kwamba, ukishavaa hiki kifaa kama miwani, watu hawajui kama unawarekodi kwenye video au vipi, na kwa wabongo walivyo wanavyojua kujihami kupigwa picha au kurekodiwa kwenye video, ukivaa Google glass unaweza tolewa baa.

 Kwa nchini Tanzania kifaa hiki ambacho kitakuwa na wastani wa bei ya sh. mil 2. 2 ($1500). Hata hivyo kifaa hicho kinachovaliwa kama miwani, sijui kama utaweza kutembea nacho hata hatua kumi kabla ya vibaka kukuvaa baada ya kujua thamani yake. Tusubiri Google wakiwezeshe kifaa hiki kiweze elewa kiswahili ndio na sisi tutakifaidi zaidi kwani hapa hamna kubonyeza bonyesha ni kuongea tu. Je ukipata Google glass utatumia kifaa hiki cha kisasa kufanyia nini? Acha maoni yako.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

MWANAMZIKI AMUITA SHABIKI JUKWAANI NA KUANDA "KUDENDEKA" NAYE



 Baada ya Mziki kukolea Msanii Akimuita shabiki stajini ili wacheze naye lakini mambo yalikolea zaidi pale walipojikuta wana kisiana stejini kitu kilichosababisha minongono kwa mashabiki



Udaku spesho.

Rais Kagame wa Rwanda akanusha kuwa na nia ya kugombea tena urais kwa awamu ya tatu.


 

Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema hana mpango wa kugombea tena muhula wa tatu madarakani baada ya muhula wake wa sasa kumalizika mwaka 2017.
Akizungumza mjini Kigali, rais Kagame amevishutumu vyombo vya habari kuanzisha mjadala juu ya iwapo ataibadili katiba ili aweze kuwania muhula mwingine.
Mjadala huo ulifuatia hatua ya rais huyo mapema mwezi huu kuunda kamati katika chama chake, kutafakari mwelekeo wa nchi baada ya muda wake madarakani kumalizika.
Chama cha upinzani cha FDU-Inkingi, kimetoa tangazo kikilaani njama zozote za kuifanyia marekebisho katiba ili kuruhusu muhula wa tatu kwa rais.-DW

Balozi mpya wa Uingereza nchini Tanzania Mhe.Dianna Melrose awasilisha hati zake za utambulisho ikulu



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati za utambulisho kutoka kwa balozi mpya wa Uingereza nchini Tanzania Mhe.Dianna Melrose ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi (Picha na Freddy Maro)

Hivi ndivyo Chadema walivyotikisa Mbeya jana


Mapokezi makubwa ya Mh. Freeman Mbowe katika viwanja vya Rwanda Nzovwe jijini Mbeya.



 Burudani mbalimbali pia zilikuwepo





 




Mh. Mbowe pia alimtaka waziri wa Elimu na mafunzo  ya ufundi kujiudhuru pamoja na naibu waziri wa wizara hiyo kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne  na kusema kuwa katika siku 14 alizozitoa zimebaki siku tatu za wao kuendelea kuwepo madarakani na kuongeza kuwa wasipofanya hivyo wataitisha maandamano ya nchi nzima kushinikiza waondolewe katika nafasi hizo. Mara baada ya kauli hiyo Mbowe aliwataka wananchi kuchangia fedha kwaajili ya wahanga siku ya maandamano ambapo zilichangishwa fedha kiasi cha sh. 3, 267, 550/=



 

Wakichangisha fedha kwaajili ya wahanga wa maandamano yatakayofanyika pindi mawaziri wataposhindwa kujiudhuru picha ya kwanza ni Mh. Sirinde, inayofuata ni Mh. Msingwa na ya mwisho ni Mh. Mbowe.

 

Picha na Keny Pino

JOKETI KUPAMBA UZINDUZI KAMPENI YA UNYANYASAJI




Na Mwandishi wetu

MWANAMITINDO nyota nchini, Joketi Mwegelo, anatarajiwa kunogesha uzinduzi wa kampeni ya kupinga unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto kike, unaotarajiwa kufanyika keshokutwa, ambapo shughuli mbalimbali na mada zitatolewa.


Joketi, ambaye anawika katika tasnia mbalimbali nchini  ikiwemo urembo, mitindo, muziki na filamu, atashiriki kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo ijulikanayo kama Okoa Mtoto wa Kike Tanzania utakaofanyika katika Kata ya Nyamongo wilayani Tarime, Mara.


Taarifa ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Nyumbani Kwanza Media Group iliyoandaa kampeni hiyo, Mossy Magere, imesema kuwa maandalizi yote muhimu yamekamilika na Joketi atawasili wilayani Tarime kesho tayari kwa kushiriki na atatoa mada ya masuala ya ujasiriamali kwa washiriki wa tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa.


Mossy alisema kuwa mbali na Joketi, wasanii mbalimbali watashiriki kutoa burudani wakiwemo wasanii nyota wa bongo fleva na wale wa asili wanaotamba mkoani Mara.


'Maandalizi yote ya msingi yamekamilika na kinachosubiriwa ni muda wa uzinduzi ufike, Joketi anatarajiwa kuwasili hapa kesho tayari kwa kushiriki nasi. Atapata fursa ya kutoa mafunzo na mbinu

za kimaisha kwa washiriki ambao wengi ni wanafunzi wa shule mbalimbali wilayani hapa,' alisema Mossy.


Kampeni hiyo ambayo itadumu kwa kipindi cha miezi sita, itazinduliwa rasmi keshokutwa na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, ambaye ameshirikishwa kwa karibu na Kampuni ya Nyumbani Kwanza.
Alisema mchakato wa uundwaji wa klabu za wapinga unyanyasaji  katika shule mbalimbali za sekondari wilayani Tarime ambapo kampeni hiyo inaanzia umekamilika na wanafunzi wamevutiwa na kujiunga kwa wingi kwenye klabu hizo ambazo zitakuwa kichocheo cha kuendeleza kampeni hiyo.


Mossy aliongeza kuwa, uundwaji wa klabu hizo unalenga kukiwezesha kizazi cha sasa na kijacho kuwa mstari wa mbele kukataa vitendo vya unyanyasaji.


“Kila jambo jema huanzia ngazi za chini, kwa sasa tunaendelea kuunda klabu za wapinga unyanyasaji ambazo zitakuwa zikipewa mafunzo na mbinu mbalimbali ili kuwajenga kufahamu madhara wakiwa wangali  wadogo shuleni.

Thursday, February 28, 2013

Rais Kikwete apokea ujumbe Maalum Kutoka Kwa Rais Omar El Bashir wa Sudan.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ujumbe maalumu kutoka kwa Rais Omar El Bashir wa Sudan ulioletwa na Mhe.Dkt.Nafie Ali Nafie ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.(picha na Freddy Maro).

SASA WATEJA WA NMB KUWEKA PESA ZAO KUPITIA M-PESA

vodacom
Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Mark Wiessing,( kulia) na  Afisa Mkuu wa Biashara- M-Pesa- Jacques Voogt wakitia sahihi katika mkataba kam ishara ya ushikiano na makubaliano ya kumwezesha mteja wa NMB kufanya muamala wowote kwenye akaunti yake kwa kutumia huduma ya M-Pesa wakati maofisa wa NMB na Vodacom wakishuhudia.
VODACOM 2Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Mark Wiessing,( kulia) na  Afisa Mkuu wa Biashara- M-Pesa- Jacques Voogt wakibadilishana mkataba kama ishara ya ushikiano na makubaliano ya kumwezesha mteja wa NMB kufanya muamala wowote kwenye akaunti yake kwa kutumia huduma ya M-Pesa wakati maofisa wa NMB wakishuhudia.
…………………………………………………………………
NMB leo hii  imeweka historia  kwa kuanzisha huduma mpya itakayowawezesha wateja  wake nchini kuweza kuweka amana zao kupitia mawakala zaidi ya 40,000 wa M-Pesa Nchi nzima. Pia wateja wa NMB wataweza kutuma fedha kutoka NMB kwenda MPESA.  NMB na Vodacom zimezindua huduma hiyo rasmi leo hii kwenye makao makuu ya NMB.
Sasa mtu yeyote au wateja wa NMB hawatahitaji kwenda ndani ya benki ili kuweka fedha kwenye akaunti kwani sasa wataweza kuweka fedha kwenye akaunti ya NMB bila kwenda tawini.  Pia sasa wateja zaidi ya 800,000 wa NMB mobile wataweza kutuma fedha kwenda MPESA.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo, Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bw.Mark Wiessing, “alisema “Ni huduma ya aina yake ambayo itawezesha mzunguko wa miamala baina ya wateja na benki kufanyika kwa urahisi na haraka, jambo litakalosaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki sanjari na kuboresha hali ya maisha na uchumi kwa watanzania wote mijini na vijijini”.

MBUNGE WA JIMBO LA UBUNGO-CHADEMA JOHN MNYIKA:'NCHI IMEINGIA TENA KWENYE MGAWO WA UMEME, SERIKALI IELEZE WANANCHI UKWELI NA HATUA KUHUSU UDHAIFU KWENYE UTEKELEZAJI WA MPANGO WA DHARURA.'

Mbunge wa jimbo la Ubungo-Chadema Mh John Mnyika-
---
Nchi imeingia tena katika mgawo wa umeme kinyume na ahadi iliyotolewa na Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo bungeni tarehe 28 Julai 2012. 

Hali hiyo ni matokeo ya Serikali kutozingatia tahadhari niliyoitoa bungeni tarehe 27 Julai 2012 kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani na kwa nyakati mbalimbali kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini juu ya hali tete iliyotarajiwa kuwepo na hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme. 

Ikiwa ni sehemu ya wajibu wa kibunge wa kuisimamia Serikali nawataka viongozi na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kuacha kuficha hali ya mambo na kuwaeleza ukweli wananchi kuhusu mgawo wa umeme uliojitokeza na hatua za haraka zinazochukuliwa kurekebisha hali hiyo. 

Iwapo Wizara na TANESCO hawatatoa matangazo ya ukweli kwa wananchi, kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini nitaeleza vyanzo vya mgawo wa umeme uliojitokeza ili hatua ziweze kuchukuliwa wakati huu ambapo wajumbe wa kamati ya nishati na madini wenye wajibu wa kuisimamia Serikali kwa niaba ya Bunge katika sekta hizo nyeti hawajateuliwa.


Aidha, pamoja na kutoa maelezo kuhusu mgawo wa umeme, Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO watumie nafasi hiyo pia kueleza hatua zilizochukuliwa kuhusu ukaguzi wa awamu ya pili kuhusu tuhuma za ufisadi katika ununuzi wa vifaa na uzalishaji wa umeme wa dharura ikiwemo kuhusu mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya kufua umeme. 

Ikumbukwe kwamba mwanzoni mwezi Agosti 2012 Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (NAOT) iliunda timu ya wakaguzi kufanya ukaguzi maalum wa hesabu za Shirika la Umeme (TANESCO) kufuatia tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma zilitajwa bungeni na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini katika maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani tarehe 27 Julai 2012 na Waziri wa Nishati na Madini wakati wa majumuisho ya hoja ya Serikali tarehe 28 Julai 2012. 

Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO waeleze pia hatua iliyofikiwa kuhusu uchunguzi mwingine uliofanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kuanzia mwezi Agosti 2012 wa mchakato wa ununuzi wa mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya kufua umeme wa dharura kutokana na tuhuma mbalimbali zilizotolewa bungeni kuhusu ununuzi huo suala ambalo Kambi Rasmi ya Upinzani ilitaka pia tarehe 27 Julai 2012 liundiwe kamati teule ya Bunge ili uchunguzi wa kina uweze kufanyika. 


Wenu katika uwakilishi wa wananchi, 

John Mnyika (Mb)
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini 

27 Februari 2013

Mtanzania apewa uwaziri Rwanda

RAIS Paul Kagame wa Rwanda amemteua Mtanzania, Profesa Silas Rwakabamba kuwa Waziri wa Miundombinu wa nchi hiyo katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanyika Jumatatu iliyopita.

Kabla ya uteuzi huo, Profesa Rwakabamba alikuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda. Ni mmoja wa mawaziri wanaoingiza sura mpya katika Baraza la Rais Kagame ambalo amelifanyia mabadiliko kwa kuunda wizara nyingine mpya.

Sura nyingine mpya katika Baraza hilo ambalo liliapishwa juzi Ikulu ya Rwanda ni pamoja na Seraphine Mukantabana (Wakimbizi na Menejimenti ya Maafa) na Oda Gasinzigwa (Ofisi ya Waziri Mkuu- Familia na Jinsia).

Akizungumza kwa simu na mwandishi wetu jana, mdogo wa Profesa Rwakabamba, Timothy Rwamushaija anayeishi Dar es Salaam, alisema ndugu yake alizaliwa katika Kijiji cha Bushagara, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera.

Alisema Profesa Rwakabamba alikuwa Mtanzania aliyeamua kuchukua uraia wa Rwanda na wote baba yao ni Mzee Titus Rwamushaija... “Huyu ni kaka yangu wa tumbo moja na kwa kweli tumefurahi sana kwa mafanikio yake sisi kama wanafamilia.”

Naibu Makamu Mkuu - Taaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Profesa Makenya Maboko alisema Profesa Rwakabamba alifanya kazi katika chuo hicho na aliondoka akiwa Mkuu wa Kitivo cha Uhandisi.

“Aliondoka wakati Kagame alipoingia madarakani na alikwenda kuongoza Taasisi ya Teknolojia ya Kigali (KIST) kabla ya kwenda katika Chuo Kikuu cha Kigali,” alisema Profesa Maboko.

Msomi huyo alikwenda Rwanda mwaka 1997, baada ya kuombwa na Rais Kagame ambaye alikwenda UDSM kuwaomba baadhi ya wahadhiri kwenda Kigali kufungua chuo kikuu katika taifa lake baada ya kumalizika vita ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1994.

Profesa Rwakabamba alikuwa Mkuu wa kwanza wa KIST na kukifanya kuwa miongoni mwa vyuo bora barani Afrika kwa masuala ya teknolojia jambo lililomfurahisha Rais Kagame.

Baada ya mafanikio hayo, Rais Kagame alimteua kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda, Butare ambako pia alijizolea sifa baada ya kusimamia vyema ujenzi wa mabweni kwa wingi na kiongozi huyo alimtunukia uraia wa nchi hiyo kama zawadi.

Hata hivyo, Profesa Rwakabamba atakuwa amelazimika kuukana uraia wa Tanzania kwa kuwa katiba ya nchi hairuhusu uraia wa nchi mbili.
Profesa Rwakabamba alipata elimu ya msingi huko Muleba na akajiunga na Shule ya Sekondari ya Ihungo.

Baada ya hapo, alijiunga na Chuo Kikuu cha Leeds, Uingereza na kupata Shahada ya Uhandisi mwaka 1971 na 1975 alipata Shahada ya Uzamivu katika fani hiyohiyo.
Chanzo: Mwananchi 

Tigo yaboresha huduma za mawasiliano na KABAANG


Meneja Chapa ya Tigo bw. William Mpinga akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya ya  kifurushi cha KABAANG kwa ajili ya wateja wao.kulia ni bi. Jacqueline Nnunduma Mtaalam wa ubunifu wa ofa za Tigo.
Mbunifu wa ofa za Tigo bi. Jacqueline Nnunduma akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya ya kifurushi cha KABAANG.kushoto bw. William Mpinga Meneja Chapa ya Tigo.
Mshindi wa Tigo smartcard promotion bw. Julius Raphael Kanza akiwa uwanja wa ndege J.K Nyerere akiongea na waandishi wa habari kabla ya safari yake ya kuelekea Madrid nchini Hispania kutazama mechi kati Real Madrid na Fc Barcelona jumamosi wiki hii itakayofanyika kwenye uwanja Santiago Bernabeu.

Tigo Tanzania imezindua bidhaa mpya ijulikanayo kama "KABAANG" ambayo itawapa wateja wake fursa ya kupata muda wa maongezi wa bure, kifurushi cha intanet na ujumbe mfupi bila kikomo kwa kujumuisha huduma hizi kuu tatu kwenye kifurushi kimoja.


“KABAANG” ni kifurushi cha wiki ambacho mteja akijiunga anapata dakika 300 za muda wa maongezi ambazo anaweza kuzitumia kupiga simu kwenda mtandao wowote ule, anapata kifurushi cha intaneti na kuweza kutuma ujumbe mfupi bila kikomo.


" Tuliona kuna haja kubwa sana ya kuzindua bidhaa itakayohusisha mahitaji mbalimbali ya wateja wetu kwenye kifurushi kimoja cha bei nafuu na kitakachowapatia wateja matumizi mbalimbali. 


Kifurushi hiki cha wiki kinamruhusu mteja kutumia huduma mchanganyiko ipasavyo na kwa bei nafuu kabisa na kitawafaa sana wajasiriamali na waajiriwa wa mashirika mbalimbali kwani kitawawezesha kuwasiliana kwa simu, sms na barua pepe muda wowote wakati wakiendelea na mambo mengine kwa shilingi 9000 tu wateja wa Tigo wanapata huduma nyingi na bora zaidi ” alisema Ndg. William Mpinga, Meneja wa chapa ya Tigo.


Ndg. Mpinga aliendelea kwa kusema " kwa kutumia KABAANG wateja wetu wataweza kuwasiliana vizuri zaidi kwani itapunguza mzigo wa uhitaji wao wa kutaka kuwasiliana kila wakati kwani inawapatia bidhaa iliyojumuisha mahitaji yao makuu ya mawasiliano kikazi na kwenye biashara. Mteja anahitaji laini moja tu ya simu kufurahia bidhaa hii bora kutoka Tigo".


Kutumia kifurushi hiki mteja anabidi atume neno "Kabaang" kwenda 15711, na baada ya hapo atapata ujumbe wa kuadhimisha kujiunga na kuweza kutumia kifurushi. Kabaang inapatikana kwa wateja wote wa Tigo wenye simu zinazotumia intaneti na kinagharimu shilingi 9,000 tu kwa wiki.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein Akutana na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa Nchi za Tanzania,Uganda na Burundi, Bw Philippe Dongie Ikulu Zanzibar

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa Nchi za Tanzania,Uganda na Burundi,Philippe Dongie,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili  ya mazungumzo na Rais,leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa Nchi za Tanzania,Uganda na Burundi,Philippe Dongie,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.Picha na Ramadhan Othman,ikulu-Zanzibar

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...