Tuesday, February 26, 2013

Khadija Kopa, Isha Mashauzi Watoana Kijasho DAR LIVE.

Malkia wa mipasho, Khadija Kopa, akionesha umahiri wake wa kutikisa nyonga.
Mashabiki wanaomfagilia Isha Mashauzi wakiwa wamevamia steji baada ya kuwadatisha.
Aziza Abul ‘Bonge’ wa TOT Taarab akikamua.
Malkia wa mipasho akiserebuka na mmoja wa mashabiki wake aliyepanda jukwaani kumtunza.
Wakali Dancers wakiwajibika jukwaani.
Shabiki akimtunza Malkia wa mipasho baada ya kukunwa na mipasho.
Isha Mashauzi akikamua.
Mashabiki wakijimwaya kwa raha zao.
WAKALI wa miondoko ya muziki wa mwambao nchini, Malkia wa miondoko hiyo, Khadija Kopa akiwa na Kundi la TOT Taarab na Isha Ramadhani ‘Mashauzi’ jana waliugeuza Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live kuwa uwanja wa mapambano baada ya kushindana kutoa burudani kwa kuonesha makali yao na kuwafanya mashabiki kila mmoja kumtaja mshindi wake.
Kabla ya wakali hao kuanza kuhenyeshana jukwaani burudani hizo zilianza kwa kunogeshwa na shoo kali ya washiriki wa shindano la Mic King linaloendeshwa ukumbini hapo kila Jumapili. Baada ya washiriki hao wanaowania gari, kundi la Wakali Dancers lilivamia jukwaa na kufanya vitu vyake pia.
(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL )

SIMBA SC WAITISHA MKUTANO MKUU WA DHARURA


Msemaji wa klabu ya simba Ezekiel Kamwaga akizungumza na Waandishi wa Habari  leo mchana 


KIKAO cha Kamati ya Utendaji ya Simba SC jana, kimefikia uamuzi wa kuitisha Mkutano Mkuu wa dharula wa klabu hiyo, ambao ajenda yake itakuwa moja tu, kujadili mwenendo wa timu katika mashindano mbalimbali inayoshiriki.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo, makao makuu ya klabu, Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga amesema kwamba siku na mahali ambako Mkutano huo utafanyika vitatajwa wakati wowote kuanzia sasa.
Aidha, Kamwaga alisema kwamba hadi sasa hakuna kiongozi yeyote wa Simba SC aliyejiuzulu na kwamba uongozi upo pamoja. “Hadi sasa hakuna kiongozi yeyote wa klabu ya Simba aliyejiuzulu. Uongozi upo pamoja na mambo yote yatajadiliwa kwenye mkutano huo wa dharula,”alisema.
Akiuzungumzia mchezo wa marudiano, Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kamwaga alisema kwamba timu itaondoka Alfajiri ya Ijumaa kwenda Angola kuwavaa wenyeji wao, Recreativo de Libolo.
Alisema mechi hiyo itafanyika Jumapili mjini Calulo, umbali wa kilomita 200 kutoka mji mkuu wa Angola, Luanda.
“Kwa mujibu wa kanuni za CAF (Shirikisho la Soka Afrika) kama umbali wa mji ambao inachezwa mechi unakuwa ni zaidi ya kilomita 200, timu mwenyeji inatakiwa kumsafirisha mgeni kwa ndege, kwa hivyo ni matumaini yetu, wenyeji wetu watakuwa tayari wametutayarishia ndege, kwa kuwa hatuwezi kusafiri kwa basi kwa zaidi ya saa nne,”alisema Kamwaga.
Kamwaga alisema kwamba, Mkuu wa msafara wa timu atakuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu, Zacharia Hans Poppe, wakati upande wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) utawakilishwa na Mjumbe wake wa Kamati ya Utendaji pia, Muhsin Balhabou.
Kamwaga alisema kikosi kamili cha Simba kitakachokwenda Angola kitatajwa Alhamisi kwa kuwa leo ni mapema sana, kwani wanahofia anaweza kuumia mchezaji yeyote wakati amekwishatajwa kuwemo kwenye safari.
Simba SC ilifungwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza na Libolo wiki iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na ili isonge mbele, inatakiwa kushinda 2-0.
Mwaka 1978, Simba iliwahi kufanya maajabu ikitoka kufungwa 4-0 na Mufulira Wanderers ya Zambia mjini Dar es Salaam katika michuano hiyo hiyo na kwenda kushinda 5-0 ugenini, hivyo kusonga mbele. 

Baada ya habari kuenea kuwa kakamatwa na MADAWA ,MSANII TIMBULO HUU NDO UJUMBE ALIO UANDIKA BBM


VODACOM MAHELA YAWAKUTA WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO


 Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Rukia Mtingw(kulia) akiongea na Mshindi kwenye simu ya mezani wakati wa Droo  ya  kuwapata washindi wa shilingi Milioni 5 na Milioni moja  katika  Promosheni ya"MAHELA"inayoendeshwa na kampuni hiyo,ambapo wafanyabiashara ndogondogo wa Kagera na Dar es Salaam Bw.Rashid Kagombora na Adam Ramadhan wamejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5.wanaoshuhudia kushoto kulia ni Matina Nkurlu Meneja Uhusiano,Benjamin Michael Maneja wa Huduma za Ziada na Afisa Mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania Bi.Chiku Salehe,Mteja anatakiwa kutuma neno"MAHELA"kwenda namba 15544 na kuweza kujishindia.Zaidi ya shilingi Milioni 400 zinaendelea kushindaniwa.

Monday, February 25, 2013

RAGE: TUTAFANYA MAAMUZI MAGUMU KWA MATOKEO HAYA


Na Dina Ismail
KAMATI ya utendaji ya klabu ya Simba inatarajiwa kutoa uamuzi mgumu kuhusiana na mwenendo mbaya ulionayo timu hiyo katika ligi kuu ya Vodacom.
Aidha, Rage amekanusha taarifa za kujiuzulu kwake kufuatia mwenendo mbaya wa timu hiyo kwenye ligi hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage alisema kwamba kamati ya utendaji ya Simba ilitarajiwa kukutana jana kwa ajili ya kujadili mustakabali wa timu yao.
Alisema kikao hicho kitajadili kwa kina hali iliyopo sasa ambayo imesabababisha timu yao kupoteza hata matumaini ya kutetea ubingwa wao.
“Tutakuna baadaye leo na kujadili hali hii maana tukiiacha hivi hivi inaweza kutuletea madhara makubwa sana…pia tutatoa maamuzi mazito baada ya kikao chetu,”alisema.
Kuhusu na taarifa za kujiuzulu kwake, Rage alisema anashangazwa na taarifa hizo zinapotoka kwani kama atafikia uamuzi huo ataitisha mkutano na waandishi wa habari na kuzungumzia hatua hiyo.
“Mimi sijasema nitajiuzulu jamani hata hiyo taarifa yenyewe ukiisoma haileweki, hivyo nawaomba wanasimba kutulia kuona kipi kitakachofuata,”aliongeza Rage
Simba imeonekana kusuasua sua katika ligi hiyo baada ya kutokuwa na matokeo ya kuridhisha sambamba na kuamulia vipigo katika mechi zake.
Hali hiyo ilianza kujitokeza tangu mwishoni mwa mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo ambao ulipelekea kutoka kileleni hadi kushika nafasi ya tatu.
Aidha, tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi hiyo, Simba imeshinda mechi mbili dhidi ya African Lyon 3-1 na Tanzania Prisons 1-0, huku ikitoka sare mbili dhidi ya JKT Ruvu na JKT Oljoro kwa bao 1-1 kabla ya kufungwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar juzi.

MWANAMUZIKI WA BONGO FLAVA AL MAARUFU KWA JINA LA ''TIMBULO''''' AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA HUKO BURUNDI.



Msanii wakizazi kipya, anae ondoka na mitindo ya bongo flava Ally TIMBULO kuna tetesi zinasema kuwa amekamatwa na dawa zakulevya Mjini Bujumbura .......

Habari zinadai kwamba Msanii huyo alikuwa na mpango waku endesha tamasha Mjini Bujumbura mwezi wa 4 baada ya maombi lukuki ya washabiki wake Mjini Bujumbura/nchini Burundi . ......
 

WAZIRI WA MICHEZO AIFUTA KATIBA YA TFF ILIYOTUMIWA NA KINA MTIGINJOLA KUWAFYEKA KINA MALINZI, WAMBURA... AAMURU ITUMIKE KATIBA YA 200

\


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt Fenella Mukangara Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt Fenella Mukangara


SERIKALI imeingilia kati sakata la uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kuamuru kufutwa kwa katiba ya sasa ya shirikisho hilo na badala yake kuamuru itumike katiba ya zamani (mwaka 2006) baada ya kubaini kuwa iliyopo ina kasoro nyingi.
Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari leo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo imeeleza kuwa katiba ya sasa ya TFF si halali. Imeelezwa vilevile kuwa msajili wa vyama vya michezo aliyedaiwa kuipitisha katiba hiyo ameondolewa. 
Mchakato wa uchaguzi mkuu wa TFF umesimamishwa kutokana na mgogoro mzito uliotokana na kuenguliwa kiutata kwa wagombea kadhaa, wakiwamo Jamal Malinzi anayewania urais na Michael Wambura anayetaka kugombea nafasi ya makamu wa rais.
Kamati ya rufani ya TFF inayoongozwa na Iddi Mtiginjola ndiyo iliyozua balaa lote la sasa baada ya kuwaengua kina Malinzi na mwishowe kumuacha makamu wa sasa wa rais, Athumani Nyamlani abaki kuwa mgombea pekee.
Hata hivyo, tayari mchakato wa uchaguzi huo uliozua mabishano makali umeshasimamishwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na maafisa wa chombo hicho cha juu cha mchezo wa soka duniani wameshaanza kuwasili kufuatilia kinachotokea nchini.
Uamuzi wa serikali wa kufuta katiba ya sasa na kutaka itumike ya 2006 unampa ahueni kubwa Wambura ambaye alishasema hadharani kuwa  ataiburuza TFF mahakamani kama isipoachana na katiba mpya na kufuata ya zamani; huku akitoa sababu kadhaa za kupinga matumizi ya katiba mpya, mojawapo ikiwa ni kupitishwa kwake kwa njia ya waraka wa barua pepe (e-mail) kwenda kwa wajumbe badala ya kufuata maelekezo ya katiba yanayotaka mabadiliko kufanywa na wajumbe kupitia mkutano mkuu.
Hata hivyo, kwa mujibu wa taratibu za FIFA, ni marufuku kwa shughuli za soka kuingiliwa na serikali au mahakama na nchi yoyote inayokwenda kinyume na taratibu hizo hujikuta ikifungiwa kama ilivyowahi kutokea nchini Kenya.
(CHANZO: straikamkali.blogspot.com)

MIMBA YA SISTER P "YAPOROMOKA



MSANII wa  hiphop hapa Bongo,Happy Peter maarufu kama Sister P , ambaye aliyetamba enzi hizo na ngoma kama "Anakuja" , Amejikuta mimba yake ikiporochoka  kufuatia mazoezi makali ya kujiandaa na wimbo wake mpya.

Uongozi wa Lifeline Music waizuia Ngoma ya MwanaFA isitoke leo

                                                             TAARIFA KWA WADAU

Leo tarehe 25 Februari mwaka 2013 ndio ilikuwa iwe siku nyingine ya kihistoria katika medani ya muziki wa kizazi kipya.

Kwa siku kadhaa sasa tumekuwa tukitangaza kwamba wimbo mpya wa MwanaFA ulio katika mahadhi ya Hip Hop uitwao “Kama Zamani” aliowashirikisha Man'dojo, Domokaya na The Kilimanjaro Band (Wana Njenje) ungeanza kuuzwa kupitia njia mbalimbali kama ‘iTunes’, ‘Amazon’ na kupitia katika simu za mkononi.
Pia ndio tarehe ambayo Kama Zamani ingeanza kusikika katika vituo vya redio Tanzania na nchi za jirani.
Lifeline Music Inc. ndiyo inayosimamia muziki wa MwanaFA kwa sasa, ikiwa ni kampuni ambayo inafanya kazi za muziki, kuangalia na kuhakikisha kwamba wasanii inaowasimamia wananufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na kazi zao; na kwamba muziki unaofanyika kwa sasa unafuata kanuni zote zinazosimamia makubaliano ya biashara.

Kama mjuavyo, biashara yoyote ina pande mbili na mafanikio yake yanategemea zaidi maridhiano baina ya pande hizo na utimizaji wa vipengele tofauti ndani ya mikataba ya biashara.

Katika kuboresha maslahi ya wanamuziki husika na wimbo huu,pia kuboresha zaidi njia zitakazotumika kuhakikisha ya kwamba burudani hii itawafikia washabiki wengi zaidi wa muziki unaofanywa na MwanaFA, Kilimanjaro Band(Wana Njenje) na Man’Dojo na Domokaya, tumefikia uamuzi wa kusubiri na kusogeza mbele siku ya kuachia wimbo wa Kama  Zamani kama ilivyopangwa hapo awali.
Tunachukua nafasi hii kuwaomba radhi mashabiki ambao mmekuwa mnasubiri kwa hamu kusikia ni nini muungano huu wa muziki wa kizazi kipya na moja ya bendi kongwe kabisa za muziki yenye miaka zaidi ya 40 katika tasnia ya muziki Tanzania umewaandalia.

Kwa niaba ya MwanaFA, uongozi wa Lifeline Music Inc. unaomba uvumilivu na subira toka kwenu mashabiki na wapenzi wa muziki. Tunaamini kwamba subira huvuta heri na mambo mazuri hayahitaji haraka.
Tunawashukuru kwa dhati kwa ushirikiano wenu.

Henry Mdimu
PR Strategist
Lifeline Music Inc

PICHA HIZI MTU SAMEHE BURE,HII KANGA MOKO HAIFAI(SHUHUDIA PICHA) SERIKALI LAZIMA IINGILIE KATI


Jamaa alizwa mbela ya mashabiki.

Mzuka ukaanza kumpanda:

ATAKAYE SEMA ALIYEMUA PADRI MUSHI ATAZAWADIWA MILLION 10



WAKATI kukiwa na taarifa kwamba maofisa wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) wametua nchini kwa ajili ya kufanya upelelezi wa mauaji ya Padri Evarist Mushi, Jeshi la Polisi limetangaza dau la Sh10 milioni kwa atakayefichua aliyemuua padri huyo.Padri Mushi aliuawa kwa
kupigwa risasi Jumapili iliyopita wakati akienda kuongoza ibada katika Kanisa la Mtakatifu Teresia lililopo Beit el Ras nje kidogo ya mji wa Zanzibar, ambapo inadaiwa kuwa waliomuua walikuwa wamepanda pikipiki aina ya Vespa na walimfyatulia padri huyo risasi tatu akiwa ndani la gari yake.

Wakati polisi wakitangaza dau hilo, Sheikh Ali Khamis Ali (65) mkazi wa Kitope Kaskazini Unguja, aliuawa jana kwa kukatwa mapanga mjini Zanzibar, baada ya wezi kuvamia shambani kwake.

RAISI KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA BABA MZAZI WA RAISI WA UGANDA YOWERI KAGUTA MUSEVENI

Rais Dkt. Jakaya Kikwete juu akiweka shada la maua kwenye jeneza na kutoa heshima zake za mwisho. Chini kabisa akiwa na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakiweka udongo kwenye kaburi la Mzee Amos Kaguta  wakati wa mazishi yake yaliyofanyika katika kijiji cha Rwakitura. Kulia ni Mama Janet Museveni
.....................................................

Picha na habari na Freddy Maro
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana aliungana na mamia ya wananchi wa Uganda katika kushiriki Mazishi ya Mzee Amos Kaguta(97) Baba ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda,yaliyofanyika katika kijiji cha Rwakitura,magharibi ya Uganda.

 Rais Kikwete aliwasili katika mazishi hayo akitokea Addis Ababa mji Mkuu wa Ethiopia alipokuwa huko kuhudhuria Mkutano wa viongozi wa cnhi za Maziwa Makuu uliokuwa na lengo la kutafuta amani ya kudumu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 

Akitoa salamu zake za RambiRambi katika msiba huo Rais Kikwete alisema kuwa Watanzania wapo pamoja na ndugu zao wa Uganda wakati huu wa majonzi na kusema kuwa yeye binafsi anampa pole Rais Museveni na familia yake na kumtaka awe na moyo wa subira katika kipindi hichi na kumuombea marehemu. 

Rais Museveni alimshukuru Rais Kikwete kwa kufika katika msiba huo ambapo alisema kuwa Marehemu Mzee Amos atakumbukwa kwa kuthamini elimu ambapo aliwapeleka watoto wake shule na kwa kufanya mabadiliko ambapo alikubali kufuata njia bora za ufugaji wenye tija jambo ambalo ni gumu kwa wazee wengi wenye umri wake.

Rais Museveni alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuwatunza vyema wazazi wao ili waishi muda mrefu na kulaani tabia ya baadhi ya vijana kuishi kwa kutegemea mali za wazazi wao badala ya kuzalisha mali yao wenyewe akiongeza kuwa wazee wana hazina kubwa ya maarifa kutokana na kukumbana na changamoto nyingi katika maisha yao. 

 Marehemu Mzee Amos Kaguta alizaliwa mwaka 1916 katika kijiji cha Kabahambi,Kikoni Mtungamo nchini Uganda. Rais Kikwete na ujumbe wake akiwemo Waziri wa Ulinzi Mh.Shamsi Vuai Nahodha waliondoka kurejea jijini Dar es Salaam baada ya mazishi hayo

TUME YA PINDA KUCHUNGUZA MATOKEO KIDATO CHA NNE 2012 YAPINGWA.

Dk. SLAA ADAI HOJA YA MBATIA ILIKUWA NA MAJIBU YOTE. 
 WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA. 
DK SLAA.
James Mbatia, Mbunge mteule katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

SIKU moja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuunda tume maalumu ya kuchunguza matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa hivi karibuni, wanasiasa na wasomi wamempinga wakidai ni kupoteza muda na fedha kwa kuwa hoja binafsi ya Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia ilikuwa na majibu.

USHAHIDI WA PICHA WABONGO WALIVYOJITOKEZA KWENYE SHOW YA ALLI KIBA NA DIMPOZ JIJINI LONDON


Picha:Umati wa Washabiki ulifika Kushuhudia Show ya Ommy Dimpoz na Alli Kiba Huko London,Show hii Ilifanyika katika club moja iitwayo OUTLET....

Pinda akutana na Balozi wa Canada.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na Balozi wa Canada nchini, Mhe.Alexandre Leveque kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam leo Februari 25, 2013. (Picha na Ofisi a Waziri Mkuu).
 
 

Rais Kikwete aondoka Addis Ababa kuelekea Uganda kuhudhuria mazishi ya Baba yake Rais Museveni.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  maafisa mbalimbali wa ubalozi wa Tanzania Nchini Ethiopia katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa jana jioni ya Februari 24, 2013 baada ya kuhudhuria hafla ya Utiaji saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Rais Kikwete, kabla ya kurejea Dar es salaam jana, alikwenda Uganda kuhudhuria mazishi ya baba mzazi wa Rais Yoweri Kaguta Museveni, Mzee Amos Kaguta, aliyefariki siku ya Ijumaa na kuzikwa kijijini kwake Rwakitura.
 Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Profesa Joram M. Biswaro akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Balozi Naimi Aziz (kati) na Afisa ubalozi Samwel Shelukindo wakipungia kumuaga Rais Kikwete wakati ndege yake ikiondoka uwanjani hapo jana jioni ya  Februari 24, 2013.(PICHA NA IKULU).
By Freddy Maro, Rwakitura, Western Uganda   
Rais  Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana ameungana na mamia ya wananchi wa Uganda katika kushiriki Mazishi ya Mzee Amos Kaguta(97)  Baba ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda,yaliyofanyika katika kijiji cha Rwakitura,magharibi ya Uganda.
Rais Kikwete aliwasili katika mazishi hayo akitokea Addis Ababa mji Mkuu wa Ethiopia alipokuwa huko kuhudhuria Mkutano wa viongozi wa nchi za Maziwa Makuu uliokuwa na lengo la kutafuta amani ya kudumu nchini  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Akitoa salamu zake za RambiRambi katika msiba huo Rais Kikwete alisema kuwa Watanzania wapo pamoja na ndugu zao wa Uganda wakati huu wa majonzi na kusema kuwa yeye binafsi anampa pole Rais Museveni na familia yake na kumtaka awe na moyo wa subira katika kipindi hichi na kumuombea marehemu.
Rais Museveni alimshukuru Rais Kikwete kwa kufika katika msiba huo ambapo alisema kuwa Marehemu Mzee Amos atakumbukwa kwa kuithamini elimu ambapo aliwapeleka watoto wake shule na kwa kufanya mabadiliko ambapo alikubali kufuata njia bora za ufugaji wenye tija jambo ambalo ni gumu kwa wazee wengi wenye umri wake(97).
Rais Museveni alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuwatunza vyema wazazi wao ili waishi muda mrefu na kulaani tabia ya baadhi ya vijana kuishi kwa kutegemea mali za wazazi wao badala ya kuzalisha mali yao wenyewe akiongeza kuwa wazee wana hazina kubwa ya maarifa kutokana na kukumbana na changamoto nyingi katika maisha yao.
Marehemu Mzee Amos Kaguta alizaliwa mwaka 1916 katika kijiji cha Kabahambi,Kikoni Mtungamo nchini Uganda.
Rais Kikwete na ujumbe wake akiwemo Waziri wa Ulinzi Mh.Shamsi Vuai Nahodha waliondoka kurejea jijini Dar es Salaam baada ya mazishi hayo.

Juliet Naivasha ajishindia Tsh 5,000,000 Kupitia DStv Rewards.


Mshindi wa pili wa DStv Rewards, Juliet Naivasha, akifurahia zawadi yake ya kitita cha Tshs Milioni 5 kama inavyoonekana katika mfano wa hundi aliyoishikilia.
Kwa wiki ya pili mfululizo, wateja wa DStv wanaolipia akaunti zao kila mwezi kabla hazijakatwa na hivyo kuingia katika droo maalumu inayochezeshwa kila wiki na kutoa nafasi kwa wateja kujishindia mamilioni ya fedha imeendelea tena kwa kumpata mshindi wake wa pili.
Kupitia kampeni hiyo ambayo imepewa jina la DStv Rewards, Juliet Naivasha, mfanyakazi wa National Bank Of Commerce (NBC), amekuwa mshindi wa pili na kujishindia kitita cha Tshs 5,000,000 (Milioni 5).

Mshindi wa pili wa DStv Rewards, Juliet Naivasha ( wa pili kutoka kushoto), akiwa na wafanyakazi wa MultiChoice Tanzania (Ronald Shelukindo na Furaha Samalu) pamoja na Mama yake mzazi, Hilder Lawrence Nyambo (anayemfuatia katika picha) pamoja na mdogo wake Lisa (kulia)
DStv Rewards ni sehemu ya kampeni maalum ya kampuni ya MultiChoice Tanzania kuwashukuru wateja wao kutokana na ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka kwao.
Akiongelea DStv Rewards, Meneja Masoko wa kampuni ya MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu, amesema DStv Rewards ipo wazi kwa kila mteja na hivyo amewashauri waendeleee tu kulipia akaunti zao kabla hazijakatwa ili wapate nafasi ya kuibuka washindi.
Wakati huo huo: Mteja wa DStv, Bwana John Komakoma,ameibuka mshindi katika droo nyingine ambayo imepewa jina la Spot The Rewards Box ambapo pindi mteja akiwa anatizama televisheni na kufanikiwa kuona kibox fulani chenye nembo ya DStv, anatakiwa kutuma SMS yenye majina yake yote mawili na namba yake ya simu kwenda katika namba +27 711 745 622 ndani ya dakika tano tangu alipokiona “kibox”.

Kwa ushindi huo Bwana John Komakoma ameshinda Subscription ya mwaka mzima (miezi 12) ya DStv.Kwa maana hiyo, Bw.John ataendelea kufaidi DStv bila malipo yoyote kwa kipindi cha mwaka mzima!

Mshindi wa droo ya Spot The Rewards Box, Bw. John Komakoma (katikati) akipongwezwa na Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania, Baraka R.Shelukindo huku Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu akishuhudia. Bw. John Komakoma amesema yeye ni shabiki wa Liverpool wa kutupwa!
Kampuni ya MultiChoice Tanzania kupitia DStv inawapongeza washindi wote.

Sunday, February 24, 2013

ADEN RAGE MWENYEKITI WA SIMBA KESHO KUACHAIA NGAZI?


Mwenyekiti wa Simba ismail Aden Rage
HABARI zilizotufikia hivi punde kutoka ndani ya klabu ya soka ya Simba zinasema kuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage anatarajiwa kujiuzulu nafasi yake kutokana na kipigo ilichopewa timu yake jioni ya leo na Mtibwa Sugar. 
Taarifa hizo zimedokeza kuwa, Rage atatangaza msimamo huo wa kuachia ngazi Msimbazi kesho atakapokutana na waandishi wa habari.
MICHARAZO imekuwa ikimsaka Rage mwenyewe kusikia kauli yake, lakini simu yake imekuwa haipatikani, hivyo juhudi zinaendelea ili kuthibitisha taarifa hizo na tutawajuvya mara tukibahatika kumpata.

MUIGIZAJI STEVE NYERERE ATUPWA LUPANGO



 
 Eneo la tukio la ajali hiyo.
 Mashuhuda wakishuhudia ajali hiyo, gari likiwa mtaroni.
 Kushoto ni gari ya Stive yenye namba za usajiri T 779 BZL na (kulia) ni gari lililohusika na ajali hiyo lenye namba za usajiri T 584 BQV.
 Huu ndiyo waya wa umeme uliosababisha ajali hiyo.
 Askari wa usalama barabarani, akipima ajali hiyo.
 Askari akimkunja Stive na kumpakia katika gari lao ili kuondoka naye kumpeleka kituoni Mabatini.
 Gari la Stive likiwa limebondeka kwa mbele lilikogongana na gari jingine.
 Gari husika na ajali likiwa limetumbukia mtaroni.
Baadhi ya warembo walikuwa na Stive katika gari lake ambao ni miongoni mwa washiriki wa Movie hiyo, wakiwa eneo la tukio.
**********
Movie mpya ya Msanii wa kuigiza sauti za Viongozi Stive Nyerere, iliyokuwa ianze kurekodiwa leo imeingia dosari baada ya msanii huyo kupata ajali na kuswekwa lupango katika kituo cha Polisi cha Mabatini, asubuhi hii.
Msanii huyo amepata ajali hiyo maeneo ya karibu kabisa na kituo cha Mabatini, wakati akiwa na msafara wa wasanii wenzake wanaoshiriki katika Movie hoyo, wakati wakielekea kuanza kurekodi.

Wasanii hao pamoja na Stive, walikuwa wakitokea katika Kambi yao iliyokuwa maalum kwa maandalizi ya kuanza kurekodi ikiwa ni pamoja na kufanyia mazoezi katika kambi hiyo iliyodumu kwa wiki kadhaa.

Ajali hiyo ilikuwa kama hivi:- Wakati Stive akiwa na baadhi ya washiriki wa movie yake katika gari lake na wakiwa katika mwendo kuelekea eneo la kushuti sini zao, ghafla aliona gari aina ya funcargo ikiwa imesimama mbele yake huku katikati ya barabara akiwapo jamaa aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo hilo.

Baada ya kushindwa kusimama kwa ghafla ndipo alipoigonga gari hiyo kwa nyuma na gari hiyo kutumbukia mtaroni. 

Mashuhuda wa ajali hiyo walieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni Fundi umeme aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo hilo ili kuweza kuondoa waya wa Umeme uliokatika na kulala katikati ya barabara huku ukiwa na moto, ili kuepusha madhara zaidi.

Baada ya ajali hiyo, walifika askari Polisi wakiambatana na askari wa usalama barabarani, ambapo alianza kupima ajali hiyo huku madereva wakijibizana na fundi aliyesimamisha magari, ambapo majibizano hayo yaliingiliwa kati na mmoja kati ya askari waliofika eneo hilo.

Katika majibizano hayo baina ya fundi, Askari na madereva wote wawili, ndipo kulitokea kupishana kauli baina ya Stive na Askari huyo, aliyediriki kumuita Stive mjinga, ambapo Stive alishindwa kuvumilia na kuamua kumjibu na ndipo alipokunjwa 'Tanganyika Jeki' na kukokotwa hadi katika gari walilokuja nalo askari hao na kumpakia na kisha kuondoka naye kuelekea katika Kituo cha Mabatini. 
 
credits: Sufiani Mafoto

WAANDISHI WA HABARI WANUSURIKA KUTEKWA WAKITOKA KUHOJI MASWALA YA GESI MTWARA

Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, walioshiriki Kongamano la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mjini Mtwara, wakilindwa na Askari wa Kikosi cha Polisi cha Kutuliza Ghasia (FFU), eneo la Chuo cha VETA, mjini Lindi jana asubuhi walipopelekwa na  mabasi madogo maarufu kwa jina 'Coaster' kutoka Mtwara Mjini, walikokimbia vitisho vya baadhi ya wakazi wa mji huo, waliopanga kuwavamia wakiwa kwenye mabasi makubwa mawili yaliyopangwa kuwasafirisha kwenda Dar es Salaam jana, wakiwahisi kuwa wanahabari hao walikuwepo mkoani humo kupeleleza suala la Gesi.  (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA  Na Richard Mwaikenda, Mtwara

WAANDISHI wa Habari 150  kutoka vyombo mbalimbali wamenusurika kuvamiwa na wananchi wakiwahisi kwamba walikwenda mjini Mtwara kupepepeleza suala la Gesi.

Wanahabari hao waliokuwepo Mtwara katika Kongamano la siku mbili la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), lilibidi wabadili muda wa kuondoka jana badala ya saa mbili asubuhi waliondoka alfajiri saa 11.

Uamuzi huo ulitolewa baada ya kuwepo fununu kwamba wananchi hao walipanga kuwavamia na kuwadhuru waandishi wa habari wakiwa kwenye mabasi mawili ya Kampuni ya amanju yaliyotakiwa kuondoka Mtwara saa mbili asubuhi kwenda nao Dar es Salaam.

Fununu hizo ziliwapata wanahabari wakiwa kwenye hafla ya chakula cha usiku waliyoandaliwa na NHIF, kwenye Hoteli ya Makonde Beach juzi usiku, ambapo hata Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia alihudhuria, lakini hakufika mwisho baada ya kusikia taarifa hizo.

Hongera rais Kagame : Rais Paul Kagame wa Rwanda na Mke wake Bi Jeannette Kagame wakishirikiana na wananchi wa Kanyinya wilaya ya Nyarugenge kuchimba mitaro ya maji jana( Feb 23,2013).



Rais Paul Kagame wa Rwanda na Mke wake Bi Jeannette Kagame wakishirikiana na wananchi wa Kanyinya wilaya ya Nyarugenge kuchimba mitaro ya maji  jana( Feb 23,2013): Hongera rais Kagame.

MDEE AONGELEA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE


 Mheshimiwa Halima Mdee akinukuu ilani ya uchaguzi ya CCM wakati akijibu swali
Mbunge wa Kawe Mheshimiwa Halima Mdee amesema watoto wa viongozi kusoma shule za binafsi maarufu kama “Academia”  inachangia matokeo mabovu ya kidato cha nne kwa shule za kawaida. Mdee aliyasema hayo wakati akijibu swali la chanzo cha kushuka kwa kiwango cha ufaulu mwaka hadi mwaka wakati akiongea na Fina Mango katika Kipindi cha Makutano. “Kwa Mtazamo wangu mimi, zamani watoto wa viongozi tulikuwa tunasoma shule hizi za umma, kwa siku hizi tunawasomesha hizi shule za academia, kwa ubinafsi wetu hawa huku kwa kuwa watoto wetu hawapo hata ule moyo wa kutoa maelekezo unakuwa haupo”

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...