Thursday, January 08, 2015

MATOKEO YA KOMBE LA MFALME JANA HISPANIA... REAL MADRID YA RONALDO YAPIGWA 2-0

article-2901036-247E14AF00000578-297_964x390
 
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
SpainCopa del Rey January 7
FT Villarreal 1 – 0 Real Sociedad
FT Atletico Madrid 2 – 0 Real Madrid

SIMBA YATINGA NUSU FAINALI YA MAPINDUZI

Vijana wa timu ya Simba yenye makao yake makuu Msimbazi jijini Dar es Salaam  
 
katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar, timu ya Simba imetinga hatua ya nusu fainali baada ya kuichakaza Taifa Jang'ombe mabao 4-0 katika mchezo wa robo fainali uliochezwa jana usiku mjini Zanzibar. Michezo mingine ya robo fainali inaendelea leo kwa timu za KCC ya Uganda kumenyana na Polisi Zanzibar, Azam ya Tanzania itakwaruzana na Mtibwa Sugar pia ya Tanzania, huku Yanga ikikamilisha michezo ya hatua hiyo kwa kupambana na JKU ya Zanzibar saa mbili usiku mjini Zanzibar. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

FERNANDO TORRES AREJEA KWA KISHINDO

Fernando Torres  
 
Fernando Torres arejesha ushindi katika klabu yake ya Atletico Madrid kwa kuwabamiza Real Madrid 2-0 katika michuano ya Kombe la Mfalme, Copa del Rey.
Mbele ya umati wa mashabiki 46,800 waliokuwa wakiishuhudia mechi hiyo ya aliyekuwa mchezaji mahiri wa timu za Liverpool na Chelsea, amerejea katika timu yake iliyomkuza na kumtambulisha kipaji chake, Atletico Madrid.
Raul Garcia,aliipatia timu yake bao la kuongoza katika dakika ya 58 akifunga kwa njia ya penalti, huku Jose Maria Gimenez akikamilisha ushindi wa Atletico kwa kufunga bao kwa njia ya kichwa katika dakika ya 76 ya mchezo.
Torres mwenye miaka 30 alibadilishwa katika dakika ya 59. Mchezaji aliyechukuliwa kwa mkopo kutoka katika timu ya Italia ya AC Milan wiki iliyopita, ndiye aliyeongoza kwa ufungaji katika timu ya Atletico kwa misimu mitano kabla hajatia mguu Liverpool mwaka 2007.
Mashabiki wapatao 45,000 waliishuhudia mechi iliyopigwa katika uwanja wa Vicente Calderon mnamo siku ya Jumapili wakati ambapo utambulisho wa Torres ulipofanyika na papo hapo jezi zenye jina lake zikaanza kuuzwa ambapo ndani ya saa 24, ziliuzwa jezi 2,000. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

STEVEN GERRARD AKARIBISHWA LA

Kobe Brayan  
 
Mchezaji maarufu wa mpira wa kikapu nchini Marekani, Kobe Brayant katika kuonyesha umoja michezoni amemtumia ujumbe nahodha wa timu ya Liverpool Steven Gerrard, baada ya uthibitisho kutoka timu ya LA Galaxy kwamba kiungo huyo mkabaji ataungana na timu hiyo mwaka huu.
Katika ujumbe wake wa video kwa Steven, Brayant anamwambia mchezaji huyo wa zamani wa timu ya England kuwa yeye ni shabiki wake wa muda mrefu na kwa hilo Brayant anaamini ushindi mwingine unakuja kwa timu ya Galaxy, na anathibitisha ushindi upo, maana ana imani na Steven Gerrard.
Gerrard atakipiga katika ligi kubwa za vilabu baada ya mkataba wake wa awali na Anfield kumalizika. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Wednesday, January 07, 2015

CCM, CUF WALIANZISHA


 
Utata mpya umeibuka kuhusu matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa baada ya wagombea watatu waliotangazwa washindi kuwekwa kando ikidaiwa kuwa badala yake walioshindwa waliapishwa kuchukua nafasi zao, hali iliyozua vurugu kubwa zilizotulizwa na polisi kwa mabomu ya machozi Ubungo jana.
Kutokana na hali hiyo, wafuasi wa CUF wanaodai wagombea wa chama chao ndiyo walioshinda, waliibuka na kutanda nje ya Hoteli ya Landmark kupinga kuapishwa kwa baadhi ya wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa CCM katika Wilaya ya Kinondoni, hatua iliyosababisha baadhi ya wagombea na mashabiki kushushiwa kipigo hadi polisi walipoingilia kati kwa kurusha mabomu ya machozi na risasi za moto kuwatawanya.
Vurugu hizo zilizodumu kuanzia saa tatu hadi saa tano asubuhi, zililenga kuzuia wateule watatu wa mitaa ya Ukwamani, Pakacha na King’ong’o kuapishwa kwa madai kuwa siyo walioshinda.
Kwa upande mwingine, aliyekuwa mgombea wa Mtaa wa Msisiri, Juma Mbena alivamia eneo hilo akidai kuwa Gasper Chambembe (CUF), ambaye alishinda katika mtaa huo hakustahili kuapishwa, kitendo kilichosababisha ashushiwe kipigo na wafuasi wa CUF. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MAFUTA YAZIDI KUSHUKA BEI NCHINI




Bei ya mafuta ya petroli, dizeli na ya taa nchini inazidi kushuka kutokana na kuporomoka kwa bei ya mafuta ghafi katika soko la dunia tangu Juni mwaka jana.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Felix Ngamlagosi alisema jana kuwa bei ya rejareja ya petroli kuanzia leo imeshuka kwa Sh74, dizeli kwa Sh62 na mafuta ya taa kwa Sh54.

Bei hizo zinashuka wakati kukiwa na mjadala mkali kuwa bei zilizopo sasa hazisadifu hali halisi ya kuporomoka kwa mafuta ghafi yanayouzwa kwa Dola 50 za Marekani kwa pipa. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...