Wednesday, December 31, 2014

CCM KUTUMIA PANGA LA 2005

 
Vigezo 13 vilivyowekwa na CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2005 kumpima mwanachama anayefaa kugombea urais, ndivyo vitakavyotumika kuwaengua makada wanaoendelea kujitokeza kuwania nafasi hiyo mwakani, imefahamika.
Vigezo hivyo vinaonekana kuwa kizingiti kwa baadhi ya makada wa chama hicho ambao tayari wametangaza na wengine wanaotajwa kutaka nafasi hiyo ya juu nchini, ukiachilia mbali mnyukano unaotarajiwa kutoka vyama vya upinzani vinavyoonekana kupata nguvu.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula amelithibitishia gazeti hili kwamba, “Sifa hizo 13 zilizotumika mwaka 2005 na 2010 ndizo zitakazotumika pia mwaka 2015 na wala hakutakuwa na maboresho wala nyongeza ya aina yoyote.”
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

ASKOFU MKUDE AASA VIONGOZI KUWA WAADILIFU

ASKOFU Telesphor Mkude wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro
 Askofu Telesphor Mkude wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro

WATUMISHI wa umma wa ngazi mbalimbali waliopewa dhamana ya kuwatumikia wananchi wameombwa kuzisoma na kusikiliza kwa umakini hotuba mbalimbali za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili ziwaweke kwenye msingi wa kuwa na maadili mema, uadilifu na uwazi.
Changamoto hiyo imetolewa na Askofu Telesphor Mkude wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, hivi karibuni wakati akizungumza na gazeti hili kwenye ofisi ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Patrice, mjini Morogoro.
Akijikita katika suala la maadili ya viongozi wa umma, Askofu Mkude, alisema suala la kufuata maadili, kuonesha uadilifu na uwazi katika uwajibikaji wa kuwatumikia wananchi ni sifa kuu ya kiongozi yoyote yule.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO DESEMBA 31, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

RAIS JAMMEH "BADO NIPO MADALAKANI"

Rais wa Gambia Yahya Jammeh 
 
Rais wa Gambia amesema kuwa bado analiongoza taifa hilo la Afrika magharibi baada ya vikosi vyake vya usalama kutibua jaribio la mapinduzi.
Yahya Jammeh amesema kuwa kamanda mmoja wa jeshi wa zamani alijaribu kuchukua udhibiti wa taifa hilo alipokuwa ziarani Ufaransa.
Hatahivyo hajulikani aliko.Milio mikali ya riasi ilizuka karibu na makao ya rais katika mji mkuu.
Bwana Jammeh alichukua mamlaka kupitia mapinduzi mwaka 1994 na wapinzani wake wamekuwa wakimkosoa kwa uongozi wake wa kiimla.
Duru za kidiplomasia na zile za kijeshi zinasema kuwa wanajeshi kutoka kwa jeshi la ulinzi wa rais wanadaiwa kufanya shambulizi hilo katika makao ya rais mjini Banjul mapema siku ya jummane.
Serikali imekana kwamba kulikuwa na jaribio la mapinduzi katika taarifa iliotangazwa katika radio ya taifa.
Hatahivyo,bwana Jammeh baadaye alikiri kuhusu shambulizi hilo na kusema kuwa wanajeshi waaminifu wa Lamin Sanneh aliyemtaja kama mwenye aibu walivamia mji mkuu wa Gambia kutoka Senegal katika jaribio la kutaka kuipindua serikali yake.
Amesema kuwa wavamizi hao hatahivyo walikabiliwa na vikosi vya usalama na kuwaua wanne kati yao huku wengine wanne zaidi wakikamatwa. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

RAIS MPYA WA TUNISIA KUAPISHWA

Rais mteule Beji Caid Essebsi kuapishwa kama rais mpya wa Tunisia baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa urais nchini Tunisia 
 
Rais mteule wa Tunisia Beji Caid Essebsi anatarajiwa kuapishwa baada ya kushinda uchaguzi wa kwanza uliokuwa huru nchini humo. Alimshinda rais aliyekuwa mamlakani Moncef Marzouk. Ushindi wake unaaminisha kwamba Tunisia ndilo taifa ambalo limejinasua kutoka utawala wa kiimla hadi ule wa kidemokrasia.
Siku ya jumatatu,tume ya uchaguzi ilithibitisha kuwa bwana Essebsi alishinda kura ya raundi ya pili dhidi ya Marzouk. Rais huye mteule ataapishwa katika bunge la wawakilishi wapwa ambapo chama chake Nidaa Tounes kimepata wabunge wengi.
Raia wa Tunisia wakisherehekea ushindi wa Caid Essebsi
Tayari maandalizi ya kumuapisha yamekamilika mjini Tunis.
Hatua hiyo hiyo itafikisha tamati mvutano wa demokrasia wa miaka minne ya ghasia zilizoghubika taifa hilo zilizopeleekea kung'olewa kwa utawala wa Rais Zine el-Abedine Ben Ali.
Bwana Essebsi alihudumu katika utawala wa Ben Ali, pamoja na uongozi wa rais wa zamani Habib Bourguiba. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

BOKO HARAM WAVAMIA KIJIJI NA KUUA WATU 15

Wapiganaji wanaodhaniwa kuwa ni Boko Haram wamevamia kijiji Kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuua watu takriban 15.
Shambulizi hilo lilitokea katika kijiji cha Kautikari katika jimbo la Borno, pale washukiwa wa Boko Haram walipowasili kijijini humo kwa magari yenye silaha, wakilenga askari wa ulinzi wa jadi wa mji huo.
Kijiji hicho kipo karibu na Chibok mahali ambapo kundi la Boko Haram, liliwateka nyara wasichana wa shule zaidi ya mia mbili mwezi Aprili mwaka huu.
Zaidi ya watu elfu kumi wameuwawa Nchini Nigeria na Boko Haram mwaka huu pekee. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...