JAJI Mkuu David Maraga amejibu shutuma kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine wa Chama cha Jubilee, kufuatia uamuzi wa
Mahakama ya Juu kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais.
Viongozi wa Jubilee wamemkosoa Maraga wakidai anatumiwa na upinzani kutoa maamuzi yanayoupendelea muungano wa NASA, na wameapa
kuupitia uamuzi huo wa mahakama wakati uchaguzi utakapomalizika.
“Mimi si mwanasiasa na ninafanya kazi kwa kuzingatia misingi ya kiapo cha utii nilichoapa kuwatumikia Wakenya. Siungi mkono Jubilee wala NASA au
mtu yeyote,” alisema Jaji Maraga katika taarifa yake fupi jana.
Rais Kenyatta mwishoni mwa wiki iliyopita alimkosoa Maraga akimwita ‘mkora’, kwamba ‘alipindua’ matakwa ya mamilioni ya Wakenya waliomchagua.
Kufuatia vitisho hivyo, ambavyo vimelaaniwa vikali na wanaharakati na katika mitandao ya jamii, Maraga ambaye ni mzee wa Kanisa la Sabato (SDA),
alisisitiza kuwa anamwogopa Mungu pekee.
“Ninafuata katiba yetu. Nendeni mkaendeshe uchaguzi na iwapo mtu anapinga, lete shauri ukiwa na ushahidi mzuri na nitalifanyia kazi ipasavyo.
Kumbuka namhofia Mungu pekee,” alisema Maraga ambaye anaongoza mfumo wa mahakama