Tuesday, July 18, 2017

WANA CCM 202 WAJITOKEZA KUWANIA UONGOZI KIBITI

Wanachama 202 wa CCM wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wilayani hapa, mkoani Pwani.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, jana Jumatatu Julai 17, Katibu wa CCM wilayani hapa, Zena Mgaya amesema idadi hiyo ni nje ya idadi ya Wana CCM waliochukua fomu za kugombea nafasi za uongozi wa Kata,Shina na Tawi.

Zena amesema pamoja na kuwepo kwa changamoto kubwa za mauaji ya viongozi mbalimbali wa chama hicho, bado mwitikio wa wanachama kuchukua fomu umekuwa wa kuridhisha hasa kuanzia ngazi ya kata na wilaya.

"Pamoja na kuwepo kwa changamoto za mauaji ya mara kwa mara kwa viongozi wetu bado wanachama wetu wamekuwa na mwitikio wa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi," amesema.

Amesema kati ya wanachama waliochukua fomu za kuwani nafasi mbalimbali, 10 wanagombea uongozi kwenye nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho ngazi  ya wilaya.

Amesema, wanachama wanane wanagombea nafasi ya katibu uenezi na 48 wanagombea nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya.

Chanzo: Mwananchi

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...