Tuesday, January 05, 2016

BENITEZ ATUPWA NJE REAL MADRID, ZIDANE ACHUKUA NAFASI

Uongozi wa klabu ya Real Madrid umemtimua kocha wake Rafael Benitez ambaye ana Miezi 7 tu katika Mkataba wake wa Miaka Mitatu.

Sasa nafasi yake imechukuliwa na mchezaji mkongwe mfaransa Zinedine Zidane ambaye awali alikuwa Kocha wa Kikosi B cha Real Madrid .

Hii inatokana na matokeo mabaya kwa timu hiyo, ambapo ilitoka Sare 2-2 na Valencia, katika Mechi ya La Liga, Sare ambayo imewaacha Vigogo hao nafasi ya 3 wakiwa nyuma ya Atletico Madrid kwa pointi 4.

Tangu atue Madrid, Benitez amekuwa si kipenzi cha Mashabiki wa Klabu hiyo, baada ya kufungwa bao 4-0 kwenye mechi ya El Clasico Mwezi Novemba na Mahasimu wao Barcelona, pia kutupwa nje ya michuano ya Copa del Rey.

Tuesday, December 29, 2015

ARSENAL YAPAA KILELENI


Wachezaji wa timu ya Arsenal

Washika bunduki wa London, Arsenal wamekaa kileleni mwa ligi ya England kwa pointi 39 baada ya kuichapa Bournemouth kwa mabao 2-0.

Arsenal walipata mabao yao kupita kwa beki Gabriel Paulista aliyefunga bao la kwanza Dakika ya 27 ya mchezo kisha kiungo wa Kijeruman Mesut Ozil, akahitimisha kazi kwa bao la pili alilolifunga katika dakika ya 63.

Nao Mashetani Wekundu wa Man United wakaenda sare ya 0-0 na mabingwa watetezi Chelsea, Everton wakicheza katika dimba lao la Goodson Park wakalala kwa kipigo cha mabao 4-3 dhidi ya Stoke city.

Matokeo mengine ni: Crystal Palace 0 – 0 Swansea Norwich 2 – 0 Aston Villa Watford 1 – 2 Tottenham West Brom 1 – 0 Newcastle West Ham 2 – 1 Southampton

Monday, December 28, 2015

MLINZI WA OSAMA BIN LADEN AFARIKI DUNIA


Al Bahri


Taarifa kutoka Yemen zinasema aliyekuwa mlinzi wa Osama Bin Laden, amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Vyanzo vya habari vya kitabibu vimesema kwamba Nasser al Bahri ambaye pia alikuwa akijulikana kama Abu Jandal alifariki siku ya Jumamosi, katika Hospitali iliyoko kwenye mji wa Mukalla kusini mwa Yemen.

Alirudi nchini humo mwishoni mwa mwaka 2008, baada ya kuachiliwa kutoka katika kizuizi alichowekewa na Marekani huko Guantanamo.

Al Bahri alijulikana kuhusika na mashambulizi yaliyofanywa na mtandao wa kigaidi katika miaka ya 90, katika nchi za Afghanistan, Somalia na Bosnia.

Thursday, December 17, 2015

MAGUFULI "ELIMU BURE ITAPATIKANA"

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amewahakikishia Watanzania kwamba elimu ya bure itapatikana kama alivyoahidi.

Akijibu swali la fedha zitapatikana wapi za kutimiza ahadi yake ya elimu ya bure, Magufuli amesema, mwezi huu wa Desemba pekee, Tanzania inatarajiwa kukusanya kiasi cha dola bilioni 1, ambazo hazijawahi kukusanywa.

Amesema kuanzia mwezi huu fedha za kusomesha wanafunzi bure zitaanza kutengwa kuanzia mwezi huu. Kwa mujibu wa Dkt Magufuli, Serikali imefikia uamuzi wa kutenga dola milioni 65.5, ambazo zitapelekwa moja kwa moja katika shule zenye uhitaji na kwamba fedha zitakapotumwa, nakala ya barua itapelekwa kwa mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya pamoja na mkurugenzi wake.

Rais Magufuli ameonya yeyote atakayetumia fedha hizo vinginevyo kwamba atachukuliwa hatua kali. Amesema fedha hizo zitasaidia katika ununuzi wa vitu kama vile chaki, maandalizi ya mitihani na vitu vingine vya muhimu shuleni.

Thursday, December 10, 2015

MH. MAGUFULI ATANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.

BARAZA LA MAWAZIRI

Wizara ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.
Mawaziri - George Simbachawene  na Angella Kairuki
Naibu Waziri - Sumeilam Jafo. Naibu.

Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira
Waziri - January Makamba
Naibu Waziri – Luhaga Jerrson Mpina

Thursday, November 26, 2015

DJIBOUTI, ZANZIBAR HEROES HALI TETE

Kikosi cha Zanzibar Heroes

Michuano ya CECAFA CHALENJI CUP 2015 imeendelea jana Jumatano kwa michezo minne ya hatua ya makundi. Harambe stars ya kenya ilitoka sare ya bao 1-1 na Burundi, wenyeji Ethiopia wameifunga somalia bao 2-0, Malawi imeifunga Djibout bao bao 3-0.

Sudani kusini ikitoshana nguvu na ndugu zao Sudan baada ya kutoka bila ya kufungana.
Michuano hiyo itaendelea tena kesho ijumaa kwa michezo kadhaa, Rwanda wataikabili somalia, Vibonde Zanzibar Heroes watakuwa viwanjani dhidi ya Kenya.

Sudan kusini watawakabili Malawi na Djibout itachuana na SudanMichuano hiyo itaendelea tena kesho ijumaa kwa michezo kadhaa, Rwanda wataikabili somalia, Vibonde Zanzibar Heroes watakuwa viwanjani dhidi ya Kenya.

Sudan kusini watawakabili Malawi na Djibout itachuana na Sudan. Michuano hiyo itaendelea tena kesho ijumaa kwa michezo kadhaa, Rwanda wataikabili somalia, Vibonde Zanzibar Heroes watakuwa viwanjani dhidi ya Kenya.

Sudan kusini watawakabili Malawi na Djibout itachuana na Sudan.

Wednesday, November 25, 2015

BARAZA LA MAWAZIRI LABADILISHWA...!!!


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta

Rais wa Kenya amefanya mabadiliko katika Baraza lake la Mawaziri, na kuwaacha wote wizara zao zilizotajwa katika ufisadi. 

Rais Uhuru Kenyatta amechukua hatua hiyo siku moja tu baada ya kutangaza ufisadi kuwa tishio kwa usalama wa kitaifa.

Rais ameahidi kufanya mabadiliko zaidi katika afisi yake hivi karibuni. Katika hotuba ilioonyeshwa kwa njia ya Televisheni, Rais Uhuru Kenyatta ameongeza idadi ya wizara kutoka kumi na tisa hadi ishirini na kuongeza idara mpya chini ya wizara mbalimbali katika kile alichosema ni kusaidia mawaziri kutekeleza majukumu yao bora zaidi .

KILIMANJARO STARS YACHINJA MTU CECAFA...!!!


Wachezaji wa Kilimanjaro Stars

Michuanao ya Cecafa Chalenji Cup Imeendelea tena jana kwa michezo miwili katika hatua ya makundi. Zanzibar ilifungwa bao 4-0 na Uganda ikiwa ni Mechi ya Kundi B.

Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) imeichapa Rwanda bao 2-1 katika mchezo uliopigwa mjini Awassa na kupaa kileleni mwa Kundi A wakiwa na Pointi 6 kwa Mechi 2 na kujihakikishia kucheza hatua ya Robo Fainali.

Mabao ya Kilimanjaro stars yalifungwa na Said Ndemla pamoja na Simon Msuva huku bao la Rwanda likifungwa na mchezaji Tisiyege.

Michuano hiyo itaendelea tena leo jumatano kwa mechi kadhaa ambapo Kenya itachuana na Burundi.

Somalia itaivaa Ethiopia, Malawi itaikabili Djibouti na Sudan kusini watachuana na ndugu zao Sudan.

BARCELONA YAIZIMA AS ROMA


Mchezaji wa As Roma

Barcelona wakiwa nyumbani walichomoza na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya As Roma.

Buyen Munich wakiichapa Olympiakos bao 4-0, Maccabi Tel Aviv wakila hio kwa Chelsea kwa kichapo cha mabao 4-0. 

BATE Borislov wakifungana bao 1-1 na Buyer Liverkusen , FC Porto wakilala bao 2-0 dhidi ya Dynamo Kiev, Zenit St P wakiichapa Valencia bao 2 – 0 na Lyon wakilala mbele ya KAA Gent bao 2-1.

ANDY MURRY TAYARI KWA DAVIS CUP


Kikosi cha Timu ya Tennis ya Uingereza

Timu ya Taifa ya Uingereza ya Tenis, imewasili nchini Ubegiji kwa mchezo wa fainali ya Davis Cup utakaopigwa ijumaa nchini humo. 

Timu hiyo inaongozwa na Andy Murray imewasili chini ya uangalizi wa ulinzi mkubwa kufuatia tishio la matukio ya kigaidi ambayo yameonekana kutishia amani nchini ubelgiji.

Timu hiyo inayojulikana pia kama Great britain ilipaswa kufika nchini humo tangu Jumapili lakini ikaahirisha kutokana na masuala ya kiusalama zaidi.

 Kikosi cha Uingereza kinawakilishwa na Andy Murray, Jamie, Kyle Edmund, Dominic Inglot na James Ward ambao tayari wapo nchini Ubelgiji.

Tuesday, November 10, 2015

MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA MUHIMBILI, ABADILISHA USIMAMIZI WA HOSPITALI

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. John Pombe Magufuli akiongea na mgonjwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipofanya ziara ya kushitukiza hospitalini hapo.

Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo amefanya ziara nyingine ya kushtukiza, wakati huu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kufanyia mabadiliko usimamizi wa hospitali hiyo.

Kiongozi huyo mpya amesikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa wagonjwa hususan wanaolala chini, kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu. 

“Pia amekasirishwa na hali ya kutokujali wala kushughulikia vifaa vya kufanyia kazi ambapo amekuta mashine muhimu za uchunguzi wa magonjwa kama vile MRI na CT-SCAN zikiwa hazifanyi kazi kwa muda wa miezi miwili sasa, ilihali mashine kama hizo katika Hospitali za binafsi zinafanya kazi na wagonjwa wanaelekezwa kwenda kutafuta huduma huko,” katibu wake mkuu Ombeni Sefue amesema.

Sunday, November 01, 2015

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2015 YATANGAZWA, UFAULU JUU


Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dkt Charles Msonde


Wahitimu 518, 034 kati ya 763, 602 waliofanya mitihani ya kuhitimu darasa la saba iliyofanyika nchini kote kuanzia Septemba 2 hadi Septemba 10, mwaka huu wamefaulu mitihani yao, Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limesema leo.


 Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt Charles Msonde amesema idadi ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 67.84, asilimia 10.85 zaidi ya ufaulu wa mwaka 2014 ambapo waliofaulu walikuwa asilimia 56.99. 

Dkt Msonde amesema, ufaulu katika masomo yote umeongezeka kwa asilimia kati ya 4.61 hadi 17.22 ikilinganishwa na mwaka 2014 huku watahiniwa wakifaulu zaidi somo la Kiswahili (asilimia 77.20) na kufaulu kwa kiwango cha chini katika somo la Kiingereza (asilimia 48.56.

Amesema kati ya watahiniwa wote waliofaulu 264, 130 ni wasichana ambao ni sawa na asilimia 64.60 ya wasichana wote 408, 900 waliotahiniwa huku wavulana wakiwa 253, 904 sawa na asilimia 71.58 ya wavulana 354, 706 waliotahiniwa.

Wednesday, October 28, 2015

TOYOTA NDIO GARI MAARUFU ZAIDI DUNIANI


Sasa ni rasmi Toyota ndiyo gari maarufu zaidi duniani. Kampuni hiyo ya kutengeneza magari ya Japan imeipiku Volkswagen kutoka kwenye nafasi ya kwanza ya orodha ya makampuni yaliyouza idadi kubwa zaidi ya magari duniani mwaka huu.

Yamkini Toyota imeuza takriban magari milioni 7.5 katika kipindi cha miezi tisa ya mwaka huu. Wapinzani wao wa karibu Volkswagen kwa upande wao wameuza magari milioni 7.43. Nafasi ya tatu inashikiliwa na kampuni ya kutengeneza magari ya Marekani, General Motors.
GM iliuza magari milioni 7.2 katika kipindi hicho cha miezi 9 ya mwanzo wa mwaka huu. Wadadisi wanasema kuwa sakata ya udanganyifu iliyoikumba kampuni hiyo ya ujerumani itaathiri zaidi mauzo yake katika siku za hivi punde.

Sunday, October 25, 2015

UCHAGUZI WAHAIRISHWA KWA KUKOSA KARATASI ZA UDIWANI


Wakati zoezi la upigaji kura likiendelea nchi nzima wakazi wa kata ya Matongo, jimbo la Bariadi, mkoani Simiyu wameshindwa kupiga kura kwa nafasi ya udiwani kwa kile kinachodaiwa uhaba wa karatasi za kupigia kura.

Akiongea na waandishi wa habari Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo Abdallah Malela amesema kukosekana kwa karatasi ndicho chanzo cha uchaguzi kwa ngazi ya udiwani kusitishwa katika eneo hilo.

Alisema kuwa kata hiyo ina jumla ya wapiga kura 7500, na vituo 17 lakini karatasi ambazo zimetoka Tume ya ucHaguzi zilikuwa 3400 tu, huku zaidi ya wapigakura 4100 wakikosa karatasi hizo za kupigia kura.

RPC ARUSHA AONYA WANAOTAKA KUFANYA VURUGU


Kamanda wa Polisi mkoa Arusha, Liberatus Sabas .

Kamanda wa Polisi mkoa Arusha, Liberatus Sabas amesema jeshi hilo limebaini vikundi vilivyojipanga kufanya vurugu na akavitaka kuacha kutekeleza mpango huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda Sabas alisema wamebaini kuwa zaidi ya vijana 100 wamesambazwa mjini Arusha na Arumeru kwa ajili ya kufanya vurugu wakati wa uchaguzi. 

Alisema polisi wamejipanga kukabiliana na uhalifu au vurugu zozote zitakazotokea katika kipindi cha uchaguzi kwa kuwa tayari wamepokea tetesi za kuwapo kwa makundi hayo. “Natoa onyo kwa hayo makundi kuwa kama wanataka usalama waache mara moja kwa kuwa hawatakuwa salama,” alisema Liberatus.

Wednesday, October 14, 2015

RONALDO ATWAA KIATU CHA DHAHABU

Cristiano Ronaldo akiwa na buti za dhahabu 
 
Cristiano Ronaldo ametunukiwa kiatu cha Dhahabu kwa Ufungaji Bora huko Ulaya na kuweka rekodi kwa kutwaa kwa mara ya nne.

Katika msimu wa 2014/15, Ronaldo alifunga mabao 48 kwenye La Liga na kutwaa Buti ya Dhahabu kwa mara 3 akiwa na Real Madrid. Msimu wa 2007/08 akiwa na Manchester United alitwaa tena kiatu hicho baada ya kuwa mfungaji bora.

Hii ni mara ya kwanza katika Historia ya Miaka 47 ya Tuzo hii ya Buti ya Dhahabu kwa Mfungaji Bora wa Ligi za Ulaya kuichukua mara 4.

Ronaldo, ameifungia Real Jumla ya Mabao 323, na kufika Rekodi ya mabao mengi iliyokua imewekwa na mchezaji wa zamani wa timu hiyo Raúl González Blanco aliyekua kaifungia timu hiyo mabao 323. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

TAIFA STARS KUIVAA ALGERIA NOVEMBA 14

Kikosi cha Taifa Stars ya Tanzania 
 
Timu ya Taifa ya Tanzania itajitupa uwanja Novemba 14 kukipiga na timu ya taifa ya Algeria ikiwa ni hatua ya pili kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwaka 2018 nchini Urusi.

Katika mchezo huo Stars wataanzia nyumbani katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam.
Mchezo wa marudiano utakuwa huko nchini Algeria siku tatu baadae ambapo Mbweha hao wa Jangwani watakua ndio wenyeji wa mtanange huo.

Kikosi cha Stars chini ya Kocha Mkuu Charles Mkwasa kimefanikiwa kusonga hatua ya pili ya michuano hiyo baada ya kuiondosha Malawi (The Flames) kwa jumla ya mabao 2-1, nyumbani ikishinda 2-0, na kufungwa 1 – 0 jijini Blantyre. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

Monday, October 05, 2015

RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA 13





Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete
Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete 

Rais Jakaya Kikwete amewateua wakuu wapya 13 wa wilaya na kuwahamisha vituo vya kazi wengine saba.
Walioteuliwa ni Shaaban Ntanambe ambaye anakwenda Chato; Thabisa Mwalapwa (Hanang), Richard Kasesera (Iringa), Ruth Msafiri (Kibondo) na Abdallah Njwayo (Kilwa).

Wengine ni Asumpta Mshama (Wanging’ombe), Mohammed Utaly (Mpwapwa), Dauda Yasin (Makete), Honorata Chitanda (Ngara), Vita Kawawa (Kahama), Christopher Ng’ubyagai (Mkalama), Hawa Ng’humbi (Kishapu) na Mrisho Gambo (Uvinza).

Wakuu wa wilaya waliohamishwa vituo vya kazi ni Fadhili Nkurlu ambaye anatoka Mkalama, kwenda Wilaya ya Arusha, Wilson Nkambaku anahamishiwa Arumeru, kutoka Kishapu, Francis Miti ambaye anahama Hanang kwenda Monduli na Jowika Kasunga ambaye anahamia Mufindi kutoka Monduli.

Wengine waliohamishwa ni Muhingo Rweyemamu kutoka Makete kwenda Morogoro; Hadija Nyembo anayehamia Kaliua kutoka Uvinza na Benson Mpesya ambaye anahamia Songea Ruvuma kutoka Kahama. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...