Shirikisho
la soka la Afrika CAF limeichagua na kuipatia nafasi Guinea ya Ikweta
kuandaa fainali za kombe la Afrika 2015 kuchukua nafasi ya Moroko
iliyojitoa wiki iliyopita. Awali Rais wa CAF Issa Hayatou alikuwa na
majadiliano yenye manufaa na Rais wa nchi hiyo tajiri ya mafuta Teodoro
Obiang Nguema mjini Malabo kabla ya kufikia hatua ya kuikabidhi nchi
yake dhamana hiyo.
Taarifa ya CAF imethibitisha leo ijumaa kuwa
Guinea ya Ikweta mojawapo ya nchi ndogo barani Afrika imepewa jukumu
hilo kubwa la kuokoa jahazi la michuano hiyo na itashiriki fainali hizo
kama ilivyo kawaida ya mwenyeji. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo TzSaturday, November 15, 2014
Friday, November 14, 2014
MCHUNGAJI AFARIKI AKIJARUBU KUTEMBEA JUU YA MAJI KAMA YESU
Mchungaji kutoka Nigeria, Frank Kabele akizama alipojaribu kutembea juu ya maji kama Yesu.
...Akiomba msaada kutoka kwa waumini wake bila mafanikio.
Mchungaji kutoka Nigeria, Frank Kabele (35) amesombwa na maji katika mto mmoja nchini hiyo na kufariki alipojaribu kutembea juu ya maji kama Yesu.
Frank Kabele aliwaambia waumini wake kuwa mtu mwenye imani anaweza kufanya miujiza yeyote ila tu uwe na imani.
Aliwaahidi wafuasi wake kuwa atatembea juu ya maji pindi tu atakapomaliza maombi yake.
Lakini mambo yalienda ndivyo sivyo baada ya mchungaji huyo kujaribu kutembea katika mto mkubwa, alididimia mtoni humo na ilikuwa vigumu kwa waumini wake kumsaidia kwani maji yalikuwa na nguvu nyingi na kufariki dunia. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
TAZAMA TASWIRA ZA MAZISHI YA MSANII MABOVU IRINGA JANA
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza la msanii Mabovu kutoka msikiti wa Mwangata kwenda makaburi ya Mlolo Iringa siku ya jana. |
Msafara wa magari kuelekea makaburini. |
Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
MOTO WAZUKA JENGO LA MACHINGA COMPLEX LEO
Moto waibuka jengo la Machinga Complex jijini Dar wazimwa kabla haujaleta madhara makubwa.
Moshi ukiwa umetanda angani. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
MBOWE AMTAKA KIKWETE AVUNJE BARAZA LA MAWAZIRI
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
amemtaka Rais Jakaya Kikwete kulivunja Baraza la Mawaziri na kuunda
jipya kutokana na tuhuma za ufisadi.
Katika taarifa yake aliyoitoa jana kwa vyombo vya
habari baada ya mikutano yake katika mikoa ya Magharibi alisema ni
lazima hatua hiyo kuchukuliwa ili kukabiliana na mafisadi ambao
hakuwataja, vinginevyo alisema Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
anayoiongoza, itaanza maandalizi ya kuwasilisha bungeni, hoja ya
kutokuwa na imani naye.
Alisema Serikali imekuwa ikishindwa kuchukua hatua
za ufisadi ambazo zinawakabili watendaji wake: “Kambi ya Upinzani
Bungeni inamtaka Rais Kikwete kumfukuza kazi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
na mawaziri wake na kuunda Serikali mpya.” Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
UTAFITI WA TWAWEZA WATIKISA NCHI
Mkurugenzi Mstaafu waTaasisi ya Utafiti ya Twaweza, Rakesh Rajan (kulia)
akiwaelezea jambo Mwenyekiti wa Bodi ya Uhariri ya Raia Mwema, Jenerali
Ulimwengu (kushoto) na Mkurugenzi wa Compass Communication Limited,
Maria Sarungi katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa kabla ya taasisi hiyo
kutangaza matoke ya utafiti wao kuhusu Tanzania Kuelekea 2015, jijini
Dar es Salaam juzi.
Utafiti uliofanywa na taasisi ya
Twaweza kuhusu maoni na matakwa ya wananchi juu ya uongozi wa kisiasa
nchini, umeibua madai mapya ambayo yanauhusisha na jitihada za
kukisaidia chama tawala CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwakani.
Ripoti hiyo iliyozinduliwa Dar es Salaam juzi,
inaonyesha kuwa kama Uchaguzi Mkuu ungefanyika sasa, Waziri Mkuu wa
zamani, Edward Lowassa angeshinda urais kwa asilimia 13, akifuatiwa na
Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa asilimia 12, huku Katibu Mkuu wa Chadema
Dk Willibrod Slaa akiibuka na asilimia kumi na moja.
Mbali na wanasiasa hao, wengine waliotajwa katika
ripoti hiyo na asilimia zao kwenye mabano ni Profesa Ibrahim Lipumba
(6%), Dk John Magufuli (3%), Freeman Mbowe (3%), Samuel Sitta (4%),
Bernard Membe (5%) na Zitto Kabwe (1%). Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
RAIS KIKWETE ATOKA WODINI, FAMILIA YA NYERERE YATUMA SALAMU
Rais Jakaya Kikwete akiagana na daktari bingwa, Edward Schaeffer baada
ya kuruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Johns Hopkins, Baltimore nchini
Marekani, alikofanyiwa upasuaji mwishoni mwa wiki iliyopita.
Rais Jakaya Kikwete ametoka
wodini katika Hospitali ya Johns Hopkins na kuhamishiwa kwenye hoteli
maalumu ambako ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.
Rais Kikwete alifanyiwa upasuaji wa tezi dume wiki iliyopita na afya yake imekuwa ikiimarika siku hadi siku.
Makundi mbalimbali ya wananchi yamekuwa yakimtakia
uponaji wa haraka kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu. Miongoni mwa
waliomtakia afya njema ni familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius
Nyerere ambayo imeeleza kupokea kwa masikitiko taarifa za kuugua kwake
na kumwombea apone haraka ili aendelee na majukumu yake kwa Taifa.
Chama cha RPP cha Rwanda kimemtumia salamu za pole
Rais Kikwete na kuungana na mamilioni ya Watanzania kumwombea ili
arejee katika afya yake na majukumu ya kila siku. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
WATOTO WAZUNGUMZA LUGHA YA AJABU
Watoto
watatu kutoka kijiji cha Barca katika kaunti ndogo ya Aber Wilayani
Oyam nchini Uganda wameanza kuzungumza lugha tofauti isiojulikana baada
ya kufungiwa katika nyumba kwa miaka saba.
Lugha hiyo mpya imetajwa kuwa Leb -adam ikimaanisha lugha ya ubongo na jamii ya eneo hilo.Inadaiwa kuwa baba ya watoto hao aliwafungia ili kuwalinda kutokana na hatari yoyote.
Kulingana ma gazeti la the monitor nchini Uganda,watoto hao hawajaathirika kiakili lakini hawawezi kuzungumza na watu wengine.Wanaamini tu kile baba yao anachowaambia.
Kulingana na mama yao watoto hao waliweza kuishi kwa kula mayai ya chura yaliochemshwa na majani,ambayo hula kila asubuhi na jioni na hutumia maji kutoka shimo lililochimbwa na baba yao.
Mama yao anasema kuwa baba ya watoto hao alimzuia kutozungumza nao hatua iliowafanya kutojifunza lugha ya kiluo wakati walipokuwa wadogo.
Mwanamke huyo amesema kuwa alionywa na baba huyo kutosema chochote kuhusu watoto hao. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC
NDEGE YA KIJESHI YAANGUKA
Helikopta
ya kijeshi ya Nigeria imeanguka katika eneo la kaskazini mashariki mwa
nchi hiyo , ikiwa ni helikopta ya pili kupata ajali kwa muda wa chini ya
wiki mbili .
Ajali ya hivi karibuni imetokea viungani mwa mji wa
Yola, mji mkuu wa jimbo la Adamawa ambako kwa sasa jeshi linahangaika
kukabiliana na uasi wa wanamgambo wa Jihad.Kuna taarifa kutoka jimbo hilo kuwa wapiganaji wa Boko Haram wamekuwa wakiwasukuma wanajeshi nje ya mji muhimu uliopo karibu na mpaka wa Cameroon . Wanafunzi katika chuo kikuu cha Modibbo Adama kilichopo katika mji wa Yola wanasema walisikia Helikopta ikianguka karibu na chuo chao .
Baada ya kuanguka ikafuatiwa na mfulurizo wa milipuko , kwani inaaminiwa kuwa ilikuwa inasafirisha silaha na zana nyingine za kijeshi kwa wanajeshi wanaopigana Boko Haram. Haijawa wazi ikiwa mtu yeyote aliekuwa ndani ya ndege hiyo amenusurika na kifo .
Baada ya kusikia kelele , baadhi ya wanafunzi walianza kukimbia wakihofia kuwa wapiganaji wa jihad walikuwa wakiwashambulia Hii ni helikopta ya pili ya kijeshi kuanguka katika mji wa Yola wiki hii.
Wakati huo huo katika eneo la kaskazini kuna taarifa kuwa mji wa Mubi hauko tena mikononi mwa Boko Haram baada ya askari na vikosi vya usalama vya eneo hilo, wakiwemo wawindaji kuurejesha tena.
Lakini katika sehemu hii ya kaskazini ya jimbo la Adamawa bado hali ni mbaya na watu wamekuwa wakiukimbia mji huo ambao makundi ya Jihad yamekuwa yakijaribu kuuteka. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
MWANAMKE MZAZI ABAKWA HOSPITALINI
Polisi
nchini Pakistan wanawashikilia wanaume watatu kwa kosa la utumizi dawa
za kulevya na ubakaji kwa mgonjwa aliyefuata matibabu katika hospitali
ya serikali.
Mwanamke huyo, ambaye alijifungua hivi
karibuni,alikwenda katika eneo la Burewala Mashariki ya jimbo la
Punjab,iliko hospitali hiyo na alikwenda hapo akiwa na mumewe pamoja na
mtoto wao mchanga kwa uchunguzi wa kitabibu.Mume wa mwanamke huyo alimwacha mkewe kitambo kifupi tu na aliporejea eneo alipokuwa ,hakumkuta ila mtoto na begi la mwanamke huyo vimetelekezwa.
Saa kadhaa baadaye,alimpata mkewe akiwa amelala katika chumba chenye kiza ,kilichomo katika hospitali hiyo na kuthibitika kuwa amebakwa .
baada ya fahamu kumrejea mwanamke huyo alisema kwanza alichomwa sindano na wanaume hao watatu kisha wakaanza kumbaka kwa zamu.Wanaume wote hao ni wanafanya hospitalini hapo. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC
UINGEREZA YAANDAA SHERIA KUDHIBITI IS
Uingereza inaandaa sheria kupambana na ugaidi, kuzuia ongezeko la Waingereza wanaokwenda kupigana nchini Syria na Iraq.
Waziri
Mkuu wa Uingereza David Cameron ameelezea kwa mara ya kwanza sheria
hiyo inayopendekezwa yenye lengo la kuzuia ongezeko la Waingereza wenye
itikadi kali wanaokwenda katika nchi hizo.Waziri mkuu wa Uingereza ametangaza pendekezo la muswada huo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye bunge la Australia mjini Canberra.
Katika sheria hiyo, amesema polisi wamepewa uwezo mpya kuweza kukamata hati za kusafiria za wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wapya walioandikishwa na kundi la Islamic State, ambao wanajaribu kuondoka nchini humo.
''... Uwezo mpya waliopewa polisi katika bandari kukamata hati za kusafiria, kuwazuia washukiwa kusafiri na kuzuia raia wa Uingereza wanaorejea nchini humo isipokuwa tu wamefuata masharti yetu. Sheria mpya kuyazuia mashirika ya ndege ambayo hayata tii hatua zetu za kuwachunguza wasafiri, kuingia nchini Uingereza. Alisema Cameron.
Sheria hiyo inayopendekezwa pia itayatoza faini mashirika ya ndege ambayo hayatachukua hatua zaidi kuchunguza orodha ya abiria inayowabeba.
Serikali ya Uingereza inatarajia mswada huo utapitishwa kuwa sheria ifikapo mwishoni mwa Januari mwakani. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Thursday, November 13, 2014
MWANAMKE AFUNGWA JELA KWA KUFADHILI ISIS
Mwanamke
mmoja nchini Uingereza aliyeshitakiwa kwa kumfadhili mumewe aliyejiunga
na vita nchini Syria, amefungwa jela kwa zaidi ya miaka miwili.
Amal
El-Wahabi, mwenye umri wa miaka 28, alijaribu kumhadaa rafiki yake
kumbebea pauni 15,800 hadi nchini Uturuki ambako mumewe angeweza
kuzichukulia.Jaji aliyetoa uamuzi katika kesi hiyo, Nicholas Hilliard, alimwambia El Wahabai kuwa alifahamu vyema kwamba mumewe Aine Davis alikuwa anapigana nchini Syria na kwa hivyo alikuwa anamsaidia katika harakati zake.
Davis, ambaye alikuwa mlanguzi wa dawa za kulevya pamoja na kushtakiwa kwa kosa la kumiliki silaha, aliondoka Uingereza mwaka 2013 kwenda Syria kupigana na kundi la Isis. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
SHELL YADAIWA ILIPUUZA ONYO NIGERIA
Mawakili
wanaoiwakilisha jamii ya watu walioathiriwa na uchafuzi wa mazingira
anasema wakuu wa kampuni ya mafuta ya Shell walijulishwa mapema kuhusu
kuchakaa kwa mabomba yake ya mafuta.
Hii ilikuwa kabla ya kutokea
kwa visa vya kumwagika mafuta mara mbili hivyo kuchafua pakubwa eneo
hilo Lagoniland Kusini mwa Nigeria mwaka 2008.Shell inakana kwamba ilikuwa na taariifa kuwa mabomba hayo yalihatarisha usalama.
Shell inadai mabomba hayo yalipasuliwa na wezi wa mafuta lakini mawakili hao wamejibu kwamba mabomba hayo yalikwa duni na yalimwaga mafuta hata kwenye ziwa la eneo hilo ambako sasa uvuvi haufanyiki tena. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Wednesday, November 12, 2014
MATUMIZI YA KONDOM YAPUNGUA NCHINI...!!!
Imeelezwa kuwa
maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), yanaweza kuongezeka nchini hasa
kwa vijana kutokana na kubainika kupungua kwa kasi ya matumizi ya mipira
(kondomu).
Hayo yalielezwa jana na Katibu Mkuu, Ofisi ya
Waziri Mkuu, Dk Florens Turuka katika mkutano wa sita wa kutathmini
maambukizi ya VVU nchini.
Dk Turuka alisema maambukizi mapya yameendelea kuwapo kwa sababu vijana hawatumii kondomu kujikinga.
“Matumizi ya kondomu katika jamii yamepungua na
kuwafanya watu wengi hasa vijana kupata maambukizi na zaidi ni kutokana
na mwamko mdogo kuhusu umuhimu wa kondomu kama kinga ya Ukimwi,”
alisema. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
SITTI MTEMVU KUVUA TAJI LA MISS TEMEKE NA MISS CHANG’OMBE
HAIJAKAA
sawasawa! Siku chache baada ya Sitti Abbas Mtemvu (25) kujivua taji la
Miss Tanzania 2014 kwa madai ya kusakamwa na vyombo vya habari kuhusu
umri wake, wadau wamemwangushia uwajibikaji mwingine wakimtaka avue
mataji mengine mawili.
Aliyekuwa Miss Tanzania 2014 Sitti Abbas Mtemvu.
Baadhi ya wadau wa sanaa waliozungumza na Risasi Mchanganyiko
Jumatatu iliyopita jijini Dar walisema kama kweli Sitti ana dhamira safi
ya kukwepa kusakamwa basi ni bora kwake akavua na mataji ya Miss
Chang’ombe na Miss Temeke ambayo ndiyo yaliyompa tiketi ya kwenda kambi
ya Miss Tanzania na kushinda. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Subscribe to:
Posts (Atom)