Wafanyakazi wakiwa na bango wakiingia kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar
es Salaam palipofanyia maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Wafanyakazi
Duniani, jana.
Maandamano ya walimu
kuingia katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kuadhimisha Siku ya Walimu
Duniani, jana yalipata mtafaruku baada ya polisi kuyaingilia na kuchana
bango mojawapo lililohoji posho za wajumbe wa Bunge la Katiba.
Bango hilo la kitambaa cheupe lilikuwa na
maandishi yanayohoji posho ya Sh300,000 waliyokuwa wanapata wajumbe wa
Bunge la Katiba, yakilinganishwa na kazi kubwa wanayofanya walimu.
Ujumbe wenyewe ulisomeka hivi: “Haki iko wapi
usawa uko wapi, posho ya mjumbe wa Bunge la Katiba kwa siku shilingi
laki tatu, mshahara wa mwalimu shilingi 370 kwa mwezi. No big results
without big salary (Hakuna matokeo makubwa bila mshahara mkubwa)”.
Ujumbe huo ulikuwa ukifanya rejea ya viwango vya
malipo ya Sh300,000 kwa siku ambazo walikuwa wakilipwa wajumbe wa Bunge
Maalumu zikiwa ni Sh230,000 kama posho ya kujikimu na Sh70,000 ambazo ni
posho ya vikao. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz