Wananchi wa Brazil watakosa huduma
ya WhatsApp katika simu na vifaa vingine kwa siku tatu kufuatia kufungwa kwa
matumizi ya app hiyo ikiwa ni kama adhabu kwa mmiliki wa WhatsApp.
Hatua ya kufungiwa kwa WhatsApp
imetolewa na Jaji mmoja nchini humo, Marcel Montalvao kwa madai kuwa mmiliki wa
WhatsApp ambaye pia ndiyo mmiliki wa Facebook ameshindwa kutoa taarifa za
mtumiaji wa mtandao katika kesi iliyo mahakamani.
Kufungwa kwa huduma
hiyo kulianza jana 17:00 ambapo hakutakuwa na huduma hiyo kwa masaa 72 na baada
ya hapo huduma itarejea kama awali. Baada ya kufungiwa, WhatsApp nao wamejibu
kuwa wanashangazwa na jambo hilo kuwanyima wateja wao huduma yao kwa taarifa
ambayo wameshaitolea majibu.
“Haya maamuzi ya kuwaadhibu zaidi ya Wabrazil
milioni 100 ambao wanatumia huduma zetu kwa ajili ya kutulazimisha sisi kutoa
taarifa, tunarudia tena hatuna hiyo taarifa,” ilisema taarifa hiyo. Tangaza
biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo
Tz. tu-follow instagram @jambotz.