Sunday, October 25, 2015

UCHAGUZI WAHAIRISHWA KWA KUKOSA KARATASI ZA UDIWANI


Wakati zoezi la upigaji kura likiendelea nchi nzima wakazi wa kata ya Matongo, jimbo la Bariadi, mkoani Simiyu wameshindwa kupiga kura kwa nafasi ya udiwani kwa kile kinachodaiwa uhaba wa karatasi za kupigia kura.

Akiongea na waandishi wa habari Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo Abdallah Malela amesema kukosekana kwa karatasi ndicho chanzo cha uchaguzi kwa ngazi ya udiwani kusitishwa katika eneo hilo.

Alisema kuwa kata hiyo ina jumla ya wapiga kura 7500, na vituo 17 lakini karatasi ambazo zimetoka Tume ya ucHaguzi zilikuwa 3400 tu, huku zaidi ya wapigakura 4100 wakikosa karatasi hizo za kupigia kura.

RPC ARUSHA AONYA WANAOTAKA KUFANYA VURUGU


Kamanda wa Polisi mkoa Arusha, Liberatus Sabas .

Kamanda wa Polisi mkoa Arusha, Liberatus Sabas amesema jeshi hilo limebaini vikundi vilivyojipanga kufanya vurugu na akavitaka kuacha kutekeleza mpango huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda Sabas alisema wamebaini kuwa zaidi ya vijana 100 wamesambazwa mjini Arusha na Arumeru kwa ajili ya kufanya vurugu wakati wa uchaguzi. 

Alisema polisi wamejipanga kukabiliana na uhalifu au vurugu zozote zitakazotokea katika kipindi cha uchaguzi kwa kuwa tayari wamepokea tetesi za kuwapo kwa makundi hayo. “Natoa onyo kwa hayo makundi kuwa kama wanataka usalama waache mara moja kwa kuwa hawatakuwa salama,” alisema Liberatus.

Wednesday, October 14, 2015

RONALDO ATWAA KIATU CHA DHAHABU

Cristiano Ronaldo akiwa na buti za dhahabu 
 
Cristiano Ronaldo ametunukiwa kiatu cha Dhahabu kwa Ufungaji Bora huko Ulaya na kuweka rekodi kwa kutwaa kwa mara ya nne.

Katika msimu wa 2014/15, Ronaldo alifunga mabao 48 kwenye La Liga na kutwaa Buti ya Dhahabu kwa mara 3 akiwa na Real Madrid. Msimu wa 2007/08 akiwa na Manchester United alitwaa tena kiatu hicho baada ya kuwa mfungaji bora.

Hii ni mara ya kwanza katika Historia ya Miaka 47 ya Tuzo hii ya Buti ya Dhahabu kwa Mfungaji Bora wa Ligi za Ulaya kuichukua mara 4.

Ronaldo, ameifungia Real Jumla ya Mabao 323, na kufika Rekodi ya mabao mengi iliyokua imewekwa na mchezaji wa zamani wa timu hiyo Raúl González Blanco aliyekua kaifungia timu hiyo mabao 323. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

TAIFA STARS KUIVAA ALGERIA NOVEMBA 14

Kikosi cha Taifa Stars ya Tanzania 
 
Timu ya Taifa ya Tanzania itajitupa uwanja Novemba 14 kukipiga na timu ya taifa ya Algeria ikiwa ni hatua ya pili kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwaka 2018 nchini Urusi.

Katika mchezo huo Stars wataanzia nyumbani katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam.
Mchezo wa marudiano utakuwa huko nchini Algeria siku tatu baadae ambapo Mbweha hao wa Jangwani watakua ndio wenyeji wa mtanange huo.

Kikosi cha Stars chini ya Kocha Mkuu Charles Mkwasa kimefanikiwa kusonga hatua ya pili ya michuano hiyo baada ya kuiondosha Malawi (The Flames) kwa jumla ya mabao 2-1, nyumbani ikishinda 2-0, na kufungwa 1 – 0 jijini Blantyre. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

Monday, October 05, 2015

RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA 13





Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete
Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete 

Rais Jakaya Kikwete amewateua wakuu wapya 13 wa wilaya na kuwahamisha vituo vya kazi wengine saba.
Walioteuliwa ni Shaaban Ntanambe ambaye anakwenda Chato; Thabisa Mwalapwa (Hanang), Richard Kasesera (Iringa), Ruth Msafiri (Kibondo) na Abdallah Njwayo (Kilwa).

Wengine ni Asumpta Mshama (Wanging’ombe), Mohammed Utaly (Mpwapwa), Dauda Yasin (Makete), Honorata Chitanda (Ngara), Vita Kawawa (Kahama), Christopher Ng’ubyagai (Mkalama), Hawa Ng’humbi (Kishapu) na Mrisho Gambo (Uvinza).

Wakuu wa wilaya waliohamishwa vituo vya kazi ni Fadhili Nkurlu ambaye anatoka Mkalama, kwenda Wilaya ya Arusha, Wilson Nkambaku anahamishiwa Arumeru, kutoka Kishapu, Francis Miti ambaye anahama Hanang kwenda Monduli na Jowika Kasunga ambaye anahamia Mufindi kutoka Monduli.

Wengine waliohamishwa ni Muhingo Rweyemamu kutoka Makete kwenda Morogoro; Hadija Nyembo anayehamia Kaliua kutoka Uvinza na Benson Mpesya ambaye anahamia Songea Ruvuma kutoka Kahama. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

DEREVA BODABODA AUAWA NA KUNYOFOLEWA KICHWA NA SEHEMU ZA SIRI



 Waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda wakiwa katika kijiwe chao. PICHA NA MAKTABA

Watu wasiofahamika wamemuua kwa kumchinja mwendesha pikipiki maarufu kama bodaboda, Hosam Abdallahaman (18) na kutoweka na kichwa chake, sehemu zake za siri na pikipiki.   

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo juzi usiku katika Kijiji cha Silimka, Kata ya Itilo wilayani hapa.



Kamanda Issa alisema kabla ya mauaji hayo, saa moja usiku, Hosam alikodiwa na abiria ampeleke eneo la Silimka na hakurudi kwenye kituo chake cha kazi hadi alipokutwa akiwa ameuawa majira ya saa 4 asubuhi siku iliyofuata. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

KIKWETE NA UHURU WAZINDUA BARABARA MUHIMU

Barabara hiyo ni ya pili kufadhiliwa na AfDB baada ya ile ya Arusha-Namanga / Namanga - Athi River
 
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Tanzania Jakaya Kikwete wamezindua mradi wa ujenzi wa barabara ya Taveta-Mwatate ambayo inatarajiwa kurahisisha uchukuzi kati ya kataifa hayo mawili.

Barabara ya Arusha-Holili upande wa Tanzania pia inakarabatiwa. Rais Kikwete yumo nchini Kenya kwa ziara rasmi ya siku tatu na Jumanne anatarajiwa kuhutubia kikao cha pamoja cha mabunge mawili ya Kenya.

Mradi wa ujenzi wa barabara hizo mbili umefadhiliwa kwa pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika na serikali za Kenya na Tanzania. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

WENGER AFURAHIA USHINDI DHIDI YA MAN UTD

Arsene Wenger
 
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameeleza furaha yake baada ya klabu hiyo kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya mahasimu wao wa jadi Manchester United katika Ligi Kuu ya Uingereza Jumapili.

Wenger amesema alifurahishwa sana na uchezaji wa timu yake na kueleza kuwa walishangaza Manchester United kuanzia mwanzo wa mechi.

“Kuanzia kwa Petr Cech hadi kwa Theo Walcott wote walicheza vyema. Nimenoa timu nyingi kali lakini hakuna hata moja iliyoweza kucheza mechi 60 katika kiwango sawa. Lazima ukubali kwamba sisi ni binadamu,” alisema.

“Tuko kwenye kinyang’anyiro (cha kushindania taji), tuko alama mbili nyuma ya viongozi Manchester City na natumai matokeo ya leo yatatupa imani ya kuendelea kupigania taji.” Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

TP MAZEMBE KUKUTANA NA ALGER FAINALI

Timu ya TP Mazembe 
 
Klabu ya TP Mazembe ya Congo DRC, Itakutana na klabu ya Algeria USM Alger katika hatua ya fainali ya klabu bingwa barani Afrika.

Mazembe ilijihakikishia nafasi yake siku ya jumapili yaani jana baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya El Merrekh ya Sudan mjini Lubumbashi.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta alifunga mara mbili katika ushindi huo huku Muivarycoast Roger Assale akifunga goli la tatu. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMATATU OKTOBA 05, YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

Sunday, October 04, 2015

LUBUVA: MABADILIKO YA WATENDAJI NEC NI YA KAWAIDA

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Mstaafu Damian Lubuva ametetea uteuzi wa viongozi wapya ndani ya tume huku akisema wanasiasa hawatakiwi kuingilia mambo hadi jikoni.

Jaji Lubuva alisema hayo leo wakati wa mahojiano kwenye kipindi cha Funguka kilichorushwa moja kwa moja na televisheni ya Azam.

"Kuhamishwa au kuteuliwa kwa kiongozi ni jambo la kawaida kwenye taasisi yoyote...uteuzi unaweza kutokea wakati wowote,"alisema Jaji Lubuva. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

MAMA NA MWANA WAUAWA KWA MAPANGA

Kaimu kamanda wa polisi wa Mkoa wa Geita, Peter Kakamba . 

Mkazi wa Kijiji cha Saragulwa, Kata ya Nyamwilolela mkoani hapa na mwanaye wameuawa kwa kukatwa mapanga na watu ambao hawajajulikana. 

Tukio hilo lilitokea juzi usiku wakati mwanamke huyo, Mageni Hongera (25) akiwa amembeba mgongoni mwanaye, Joyce Ndarusanze (1), akitokea kwenye kibanda chake cha biashara kwenda nyumbani kwake. 

Kaimu kamanda wa polisi wa Mkoa wa Geita, Peter Kakamba alisema jana kuwa askari wa jeshi hilo wanaendelea kufuatilia chanzo cha mauaji hayo. “Ni kweli tukio limetokea, bado sijakusanya vizuri taarifa zake,” alisema Kakamba.  Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

TANESCO: UZALISHAJI WA UMEME UMESHUKA


Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) limesema kuwa mgao wa umeme unaoendelea nchini umesababishwa na kushuka kwa uzalishaji wa umeme katika mabwawa ya maji kwa asilimia 81.3. 

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema leo jijini dar es Salaam kuwa uwezo wa juu wa mitambo yote ya kuzalisha umeme wa maji ni megawati 561, lakini kwa sasa uzalishaji wote wa umeme wa maji ni megawati 105 ambazo ni sawa na asilimia 18.7. 

Kuhusu umeme wa gesi, TANESCO walisema kuwa uwezo wa kuzalisha umeme kupitia Kampuni ya Pan Africa ulishuka kutoka megawati 340 hadi kufikia megawati 260. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI OKTOBA 04, YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
.
.
.

Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

Monday, September 28, 2015

MGOMBEA UBUNGE WA CHADEMA DODOMA MJINI APATA DHAMANA

Mgombea ubunge wa jimbo la Dodoma mjini kupitia
Mgombea ubunge wa jimbo la Dodoma mjini kupitia Chadema, Benson Kigaila  

Ulinzi mkali leo umewekwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Dodoma ili kuzuia wafuasi wa Chadema waliokwenda kusikiliza kesi inayomkabili mgombea ubunge wa jimbo la Dodoma mjini Benson Kigaila na kusababisha lango la kuingilia lifungwe.

Kigaila na wenzake 10 wanakabiliwa na mashitaka matatu ikiwemo kumpiga na kumjeruhi polisi, kufanya maandamano bila ya kibali na pamoja na kutoa lugha za matusi katika kituo cha polisi makosa ambayo watuhumiwa hao waliyakana yote.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, James Karayemaha, Wakili wa Serikali Beatrice Nsana amesema kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa yote Septemba 25 mwaka huu majira ya jioni.
Nsana amesema kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba mahakama ipange tarehe ya kuanza kusikilizwa ambapo mahakama imekubali na kupanga Oktoba 12 mwaka huu huku dhamana ikiwa wazi.
Mara baada ya kutimizwa kwa masharti ya dhamana kwa washitakiwa wote, viongozi hao waliondoka chini ya ulinzi mkali wa polisi na kusindikizwa hadi katika ofisi za kanda za chama hicho ambako Kigaila alizungumza na waandishi wa habari. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...