LICHA ya kwamba uwepo wa wanawake katika sekta ya usafiri wa anga kuwa mdogo, uwezo wa kuwa viongozi katika usafiri wa anga hauna mwiko.
Akizungumza na gazeti hili, rubani mwanamke wa kwanza kuongoza ndege aina ya Airbus A380 inayomilikiwa na kampuni ya Fastjet Tanzania, rubani Anne-Marie Lewis anasema wanawake barani Afrika hawapaswi kuogopa kuwa sehemu ya sekta hii inayokua barani kote.
Anasema si kazi ngumu mwanamke kuwa rubani na kwamba yeye anajiamini na hana woga katika jambo lolote lile ndio maana akaaminiwa na kupata fursa ya kungoza ndege hiyo katika mikoa ya Tanzania na nchi nyingine za jirani.
“Wanawake wanapaswa kuelewa kwamba hakuna aina ya kazi ambayo ipo kwa ajili ya wanaume peke yao, bali wanawake wataleta katika sekta ya usafiri wa anga uwezo wao wa kufanya kazi kwa bidii, kulea na ujuzi wao wa usimamizi bora,” anasema.
Kwa mujibu wa Lewis, wanawake wa Afrika wanahitaji kuelewa kwamba nia na uamuzi wao utaondoa hofu au hasara ya kiuchumi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page yetu ya facebook bofya Jambo Tz sasa.